Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Makava Haya ya Simu Yanauwezo wa Kugundua Saratani

Sasa unaweza kupima sratani kwa kutumia simu ya mkononi
Saratani Saratani

Makava ya simu yanasaidia kutunza simu zetu zisipate matatizo mbalimbali, mara nyingine makava haya husaidia kuongeza kiasi cha memory kwenye simu zetu na kufanya simu zetu kuwa bora zaidi. Vile vile makava hayo husaidia pia kuchaji simu zetu na kufanya tuweze kudumu na simu zetu kwa muda mrefu, lakini pia wakati mwingine makava hayo hayo yakiongezewa teknolojia ya kisasa huweza kusaidia kulinda Afya yako na sio simu yako pekee.

Kundi la watafiti wa sayansi wa nchini marekani wakiwa wanafanya utafiti wa namna mpya ya kutambua vina saba (DNA), wamefanikiwa kugundua na kutengeneza kifaa kipya kinacho weza kurahisha mapambano dhidi ya saratani. Kifaa hicho kilicho tengenezwa na team hiyo ikiongozwa na professor wa chuo cha UCLA Aydogan Ozcan kimetengenezwa kwa kutumia simu, ambazo zinafanya kazi kama 3D printer ambazo ndio hutumika kama microscope kuchukua picha ambazo baadae huangaliwa ili kutambua vina saba (DNA).

Advertisement

Baada ya makava yalio kwenye simu hizo hutoa tafsiri maalum ya ambayo baadae wanasayansi huongeza kiasi flani cha tishu maalumu kwenye vipimo hivyo ili kugundua mahali kwenye uvimbe wa saratani.

Kwa mujibu wa UCLA kifaa hicho kinaweza kuanza kwa kutengezwa kwa kiasi cha chini kuanzia dollar za marekani $500 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,130,000. Wakati gharama ya kutengeneza kifaa ambacho kinatumika kwa sasa ni dollar za marekani $10,000 mpaka dollar $50,000 au zaidi, Hivyo wanasayansi hao wanasema sasa hii ndio njia mpya ya kupambana na saratani kwa haraka bila kutumia gharama kubwa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use