Kama wewe ni mtumiaji wa app ya WhatsApp lazima utakuwa umesha kutana na usumbufu kwa kualikwa kwenye magroup ya WhatsApp bila hata kujua nani ametengeneza group lenyewe. Sasa hivi karibuni WhatsApp inakuja suluhisho la tatizo hili kwani inakuja na njia mpya ya kuweza kukusaidia kuzuia mtu asikualike kwenye magroup ya WhatsApp bila ruhusu yako.
Kwa mujibu wa tovuti ya venturebeat, inasemekana sehemu hiyo mpya itakuwa inapatikana kwenye sehemu ya Settings alafu kwenye Menu mpya ambayo itakuwa inaitwa Group Menu. Ili kupata sehemu hiyo unatakiwa kubofya sehemu ya Settings > Account > Privacy > kisha chagua menu mpya iliyoandikwa Groups menu.
Kwenye menu huyo ukibofya sehemu ya Everyone utakuwa umeruhusu watu wote hata wasiokuwa na namba yako kukualika kwenye magroup ya WhatsApp bila ruhusa yako, lakini kwa kubofya sehemu ya My contact utaweza kuruhusu watu ambao wewe unazo namba zao kwenye simu yako ndio wakualike kwenye magroup ya WhatsApp na pia kwa kubofya Nobody utawezesha kuzuia kabisa mtu yoyote kukualika kwenye group lolote la WhatsApp.
Hata hivyo kwa wale ambao hawawezi kukualika kwenye group lolote watakuwa na uwezo wa kutumia ujumbe wa mualiko ambao utadumu ndani ya masaa 72 na baada ya hapo ujumbe huo utapotea wenyewe ikiwa pamoja na link ya kujiunga kwenye group hilo.
Kwa sasa sehemu hii inasemekana tayari imesha anza kuwafikiwa watu mbalimbali na kwenye programu za WhatsApp hivyo inawezekana kabisa sehemu hii kufikia watu wote siku chache zinazokuja. Ili kupata sehemu hii hakikisha una update app yako ya WhatsApp pale unapo ona toleo jipya kupitia Play store au App Store. Tofauti na hapo unaweza kuendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku na tutakuhabarisha pale sehemu hii itakapo fika kwa watumiaji wote.
Kwa habari zaidi kuhusu ujio wa sehemu mpya za WhatsApp unaweza kusoma hapa, kujua kuhusu sehemu mpya ya Dark Mode ambayo nayo pia inatarajiwa kuwafikia watumiaji wote hivi karibuni.