Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tovuti Bora za Kusaidia Kusoma Magazeti Leo Asubuhi

Kama unataka kusoma habari mpya za magazeti ya leo tembelea ukurasa huu
Tovuti Bora za Kusaidia Kusoma Magazeti Leo Asubuhi Tovuti Bora za Kusaidia Kusoma Magazeti Leo Asubuhi

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda kupata habari kupitia magazeti basi makala hii ni nzuri zaidi kwako, kwani kupitia hapa tutaenda kuangalia tovuti bora zinazoweza kusaidia kusoma magazeti ya leo asubuhi akila siku kupitia mtandao.

Kumbuka tovuti hizi nyingi zinakuruhusu kusoma vichwa vya habari pekee na sio habari nzima, pia kupitia makala hii nitaenda kujuza app ambayo pia inaweza kusaidia sana kusoma habari zote za magazeti ya leo kupitia simu yako ya mkononi bila matangazo. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie tovuti hizi.

Advertisement

Gazetiapp.one

Gazeti app ni tovuti ambayo inakupa uwezo wa kusoma magazeti mbalimbali kwa urahisi bila kutumia Internet, utaweza kutumia tovuti au utaweza kutumia apps ambazo zinapatikana kwenye soko la Play Store. Gazeti App ni tovuti bora ya habari na kusoma magazeti ya kila siku kwa urahisi na haraka.

Soma hapa magazeti kupitia Gazeti App

Millardayo.com

Tovuti Bora za Kusaidia Kusoma Magazeti Leo Asubuhi

Tovuti ya millardayo.com imekuwa ni moja kati ya tovuti bora za kupata habari mbalimbali, tovuti hii imekuwa ikichambua magazeti mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania kwa ustadi mkubwa. Mbali na hayo pia unaweza kuangalia video zenye kuonyesha uchambuzi wa magazeti ya leo asubuhi moja kwa moja kupitia tovuti hiyo.

Soma hapa magazeti kupitia Millardayo

Dar24.com

Tovuti Bora za Kusaidia Kusoma Magazeti Leo Asubuhi

Dar24 ni tovuti nyingine bora sana ya kusoma magazeti ya Tanzania, tovuti hii pia huweka habari kila siku zinazo onyesha picha za vichwa vya habari za magazeti mbalimbali ya hapa nchini Tanzania, kupitia tovuti hii kila siku utaweza kujua habari mpya kutoka kwenye magazeti mbali ya habari za kawaida, michezo na habari nyingine.

Soma hapa magazeti kupitia Dar24

Muungwana.com

Tovuti Bora za Kusaidia Kusoma Magazeti Leo Asubuhi

Muungwana ni moja kati ya tovuti kubwa sana za habari mchanganyiko tovuti hii pia inayo kipengele cha magazeti ya leo kipengelea ambacho hakikika kitakupa habari zote kwenye magazeti ya kila siku ndani na nje ya Tanzania. Hivyo kila siku asubuhi kama unataka kujua habari za magazeti kabla ya kwenda kununua gazeti lenyewe basi hakikisha unatembelea tovuti hiyo kwanza.

Soma hapa magazeti kupitia Muungwana

Michuzi.blogspot.com

Tovuti Bora za Kusaidia Kusoma Magazeti Leo Asubuhi

Michuzi ni moja kati ya tovuti za kuaminika sana za habari hapa Tanzania, tovuti hii pia inacho kipengele cha magazeti ambacho kinaweza kusaidia kupata habari mbalimbali za hapa Tanzania kwa urahisi sana. Kila siku asubuhi kama unataka kupata habari za magazeti ya leo hakikisha unatembelea tovuti hii.

Soma hapa magazeti kupitia Michuzi

Zanzibar24.co.tz

Zanzibar24 ni moja kati ya tovuti ambayo nayo pia ni bora sana inapkuja kwenye swala la kujua habari za magazeti, tovuti hii inakupa uwezo wa kujua yote yaliojiri kwenye magazeti yote ikiwa pamoja na magazeti ya udaku, magazeti ya michezo pamoja na magazeti ya habari za kitaifa na kimataifa.

Soma hapa magazeti kupitia Zanzibar24

Globalpublishers.co.tz

Tovuti Bora za Kusaidia Kusoma Magazeti Leo Asubuhi

Kama wewe ni mpenzi wa habari za ndani ya Tanzania basi ni vizuri kutembelea tovuti ya globalpublishers tovuti hii nayo inakuja na kipengele cha habari za magazeti na unaweza kusoma vichwa vya habari mbalimbali za Tanzania ikiwa pamoja na habari za udaku michezo na habari nyingine za muhimu kwenye magazeti.

Soma hapa magazeti kupitia GlobalPublisher

Gazeti App

Tovuti Bora za Kusaidia Kusoma Magazeti Leo Asubuhi

Sasa kama kwa namna yoyote unapendelea kusoma habari za magazeti kutoka kwenye tovuti zote hizi unaweza kufanya hivyo kupitia app ya Gazeti, App ya gazeti ni nzuri sana kwani inakusaidia kusoma habari kutoka kwenye tovuti zote hizo hapo juu ikiwa pamoja na kupata habari za magazeti kwa haraka zaidi, App hii inakuja na vipengele bora sana na mbali ya magazeti hutopitwa na habari yoyote ya hapa Tanzania.

Iwe unapenda udaku, michezo, biashara, teknolojia au habari yoyote ile app hii inayo habari zote za Tanzania. Pia mbali ya habari pia app hii inakupa uwezo wa kupakua nyimbo mpya za Tanzania, kuangalia filamu zilizo tafsiriwa pamoja na kutafuta ajira kwa haraka kabisa. Kifupi ni kuwa app ya Gazeti ndio app unayohitaji sasa kwenye simu yako kupata habari zote za Tanzania, mengine yaliyopo kwenye app ya Gazeti.

  • Utaweza kusikiliza Radio
  • Utaweza kuangalia Filamu
  • Utaweza kudownload Nyimbo Mpya
  • Utaweza kusikiliza idhaa za kiswahili kama BBC, DW na nyingine na mengine mengi.

Unaweza kupata app ya Gazeti kupitia soko la Play Store au kupakua kupitia link iko hapo chini, nakuahidi ndio app pekee ambayo utahitaji kuanzia sasa.

Na hizo ndio tovuti ambazo zinaweza kusaidia kusoma magazeti ya kila siku kupitia mtandao, kumbuka tovuti hizi zote zina aminika na unaweza kusoma vichwa vya habari za magazeti kila siku kwa kutembelea ukurasa huu au unaweza kutembelea tovuti husika moja kwa moja.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use