Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta na umekuwa ukiona kompyuta yako inaiishiwa na nafasi au storage mara kwa mara basi makala hii ni kwa ajili yako.
Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi na ya haraka ambayo itakusaidia sana kuweza kujua ni file gani au programu gani ambayo inachukua nafasi zaidi kwenye kompyuta yako. Njia hii ni rahisi na haitaji utaalamu wa aina yoyote zaidi ya kufuata hatua hapo chini.
Njia hii pia inaweza kusaidia kujua mafaili ambayo yana chukua nafasi kubwa kwenye kompyuta yako ambayo pia hujificha na ambayo huwezi kuyaona kwa kawaida. Basi baada ya kusema hayo twende kwenye njia hii rahisi.
Kwa kuanza kwa kutumia kompyuta yako download programu hapo chini, baada ya kudownload install vizuri kwenye kompyuta yako. Programu hii ni ndogo sana kiasi cha MB 9.81 hivyo usiwe na wasiwasi kuhusu bando lako.
Baada ya kuinstall programu hii kwenye kompyuta yako, moja kwa moja nenda kwenye My Computer, kisha moja kwa moja right click na chagua jina la app hii kwenye Menu.
Baada ya hapo moja kwa moja itafunguka sehemu mpya ambayo itakuonyesha moja kwa moja idadi ya mafile yaliyopo ikiwa pamoja na size ya kila file. Programu hii itaonyesha file kubwa zaidi likiwa juu na mafile yenye size ndogo yakiwa chini.
Kama unavyoweza kuona hapo juu, file lenye size kubwa kwenye kompyuta hii ni file la My other codes, kupitia programu hii unaweza kufungua file hilo au unaweza kufuta file hilo moja kwa moja.
Kwa kutumia njia hii moja kwa moja unaweza kujua programu au file ambalo linachukua nafasi kubwa ndani ya kompyuta yako. Kumbuka kama unataka kufungua file ambalo umeliona ndani ya programu hii unaweza kubofya right click kwenye mause yako kisha chagua Open. Kwa kufanya hivyo utaweza kujua file lina nini ndani yake kabla ya kuamua kufuta.
Bila shaka kwa kutumia njia hii utakuwa umeweza kuondoa mafile makubwa ambayo hayana maana kwenye kompyuta yako. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua programu za kompyuta za kusaidia kutafuta mafile kwa haraka zaidi.