Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Madhara ya Usalama Sababu ya Kusahau Kuzima Bluetooth

Ni muhimu kupunguza matumizi ya bluetooth hasa kwenye mkusanyiko
Madhara ya Usalama Sababu ya Kusahau Kuzima Bluetooth Madhara ya Usalama Sababu ya Kusahau Kuzima Bluetooth

Bluetooth ni moja ya teknolojia ya zamani sana, kama kwa namna moja ama nyingine hujui historia ya Bluetooth basi unaweza kusoma historia nzima hapa. Sasa kutokana na uzamani wa teknolojia hii sasa imeonekana kuwa na matatizo mengi sana ya kiusalama kiasi kwamba wataalam wa teknolojia wanadai kuwa, huna haja ya kutumia bluetooth kabisa kama unataka kuwa salama.

Kwa mujibu wa mtandao wa Mashable, inasemekana kuwa Bluetooth ni hatari sana kwa usalama na ni vyema kuacha kutumia teknolojia hiyo mara kwa mara hasa kwenye kwenye simu za mkononi.

Advertisement

Hayo yamegundulika kwenye mkutano wa wadukuzi unaofanyika kila mwaka unaojulikana kama DEF CON, mkutano ambao unakutanisha wadukuzi mbalimbali kujadili maswala mbalimbali ya usalama wa mtandaoni. Kwa mwaka huu mkutano huo umefanyika huko Las Vegas, Nevada kwa siku nne mfululizo kuanzia tarehe 8 mwezi wa nane hadi tarehe 11.

Sasa kwa mujibu wa Mashable, kupitia mkutano huo wadukuzi hao walionyesha jinsi wanavyoweza kutumia Bluetooth kuweza kudukua kifaa kama spika zenye kutumia teknolojia hiyo na kucheza nyimbo ambazo zinaweza kufanya mtu yoyote aliye karibu na spika hizo kupoteza uwezo wa kusikia.

Mbali na hayo, pia wadukuzi hao walionyesha jinsi wanavyoweza kuingilia mawasiliano yanayo fanyika kwa kutumia Bluetooth na kuweza kubadilisha data zozote zinazotumwa baina ya vifaa viwili vilivyo unganishwa kwa pamoja kwa kutumia Bluetooth. Vilevile pia kupitia Airdrop ambayo ni teknolojia ya bluetooth ya Apple wadukuzi hao wanaweza kupata data za muhimu kama vile namba kamili za simu za watumiaji wote wanaotumia sehemu hiyo.

Kwa sasa unachotakiwa kufanya ni kuwa muangalifu na matumizi ya bluetooth na pengine tumia sehemu hiyo pale unapokuwa sehemu salama na sio kwenye mkusanyiko wa watu wengi. Kujua zaidi kuhusu usalama mtandaoni unaweza kusoma hapa kujua mambo ambayo utakiwi kufanya unapo tumia Internet. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use