Madaktari Kenya Washirikiana Kutengeneza Application ya Kugundua Upofu

Madaktari Kenya Washirikiana Kutengeneza Application ya Kugundua Upofu Madaktari Kenya Washirikiana Kutengeneza Application ya Kugundua Upofu

Wakati technolojia ikiendela kukua kote duniani madaktari huko kenya wameungana na kutengeneza application ya smartphone iliyopewa jina la PEEK yani kwa kirefu (Portable Eye Examination Kit), application hiyo itatumika kujua mapema dalili za upofu kwa wanafunzi na walimu pamoja na watu mbalimbali.

Application hiyo iliyotengeneza kwa ushirikiano wa London School of Hygiene  na Tropical Medicine, pamoja na madaktari nchini kenya imetengenezwa maalumu kwaajili ya mfumo wa smartphone ambao utamsaidia daktari kufanyia uchunguzi wa jicho la mwanadamu ili kujua dalili za mapema za upofu, application hii inawezesha mtu kufanya testi mabalimali za jicho lake ili kujua dalili hizo kwa mojibu wa London School of Hygiene pamoja na Tropical Medicine test hizi ni pamoja na kuchunguza kutoona vizuri, pia kuchunguza kutoona rangi vizuri pamoja na tatizo la za lensi za kwenye macho pamoja na matatizo mangine yahusuyo macho.

Advertisement

Taarifa kutoka katika blogu ya IT News Africa zimeandikwa kuwa pindi mgonjwa atakapo julikana na ugonjwa ama dalili za ugonjwa wa macho application hiyo itatuma meseji kwa mfumo wa SMS kumtaka mgonjwa kufika kwenye kituo cha afya ili kupata matibabu. Pia blog hiyo iliendelea kuandika kuwa “kutokana na taarifa zilizotolewa na mtandao wa  Business Daily Africa Application hiyo ya PEEK imesha tumika kuangalia dalili za upofu kwa watoto zaidi ya 21,000 huko Trans Nzoia, Kenya ambao baina yao watoto 900 waliochunguzwa kwa apllication hiyo walijulikana na dalili za ugonjwa wa macho ambapo watoto hao waliwaishwa kupewa huduma za afya katika Hosptali ya macho ya Kitale County Hospital Eye Unit ya huko nchini Kenya.

Daktari bingwa wa macho Dr Hilary Rono katika hospitali ya Kitale County Hospital Eye Unit iliyoko nchini Kenya aliendelea kusema katika ripoti hiyo kuwa “katika kila watu 1,000 katika mji wa Trans Nzoia watano kati yao wana matatizo ya macho” hivyo application hiyo ya PEEK ni mwamko mpya ulioletwa na madaktari nchini Kenya kwa ushirikiano na London School of Hygiene pamoja na Tropical Medicine ili kufanikisha smartphone kutumika katika kuokoa uwezo wa kuona baina ya watoto wa shule pamoja na watu mbalimbali.

Soma zaidi kuhusu application hiyo ya PEEK  Bofya Hapa, Pia unaweza kupakua application inayofanya kazi sawa na application ya PEEK kwa wanaotumia mfumo wa iOS pakua app hiyo hapo chini. Kumbuka application hiyo sio PEEK bali inaweza kufanya kazi sawa na applicatio hiyo ya PEEK.

[appstore id=380288414]

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use