Kama nilivyosema kwenye makala zilizopita instagram imekuwa ikifanya mabadiliko mapya kila siku, na kama ulisoma makala yetu iliyopita basi lazima utakuwa unajua kuwa, instagram inajiandaa kuja na magroup maalum ambayo yatakuwa ni kwaajili ya wanachuo. Lakini kama haitoshi instagram imefanya mabadiliko mengine matatu ambayo ni muhimu sana kwa watumiaji wote wa mtandao huo.
- Njia Rahisi ya Kuhakiki Unaetaka Kufuata (Follow)
Mabadiliko ya kwanza ambayo yametangazwa kuja hivi karibuni ni pamoja na njia rahisi ya kuweza kuhakiki unaetaka kumfuata (Follow). Sehemu hiyo itapatikana kwenye sehemu ya vidoti vitatu vinavyo patikana juu ya akaunti ya mtu unayetaka kumfuata. Utakapo bofya sehemu hiyo utaweza kuona sehemu mpya ya About This Account, ukibofya hapo utaweza kuona data za muhimu kuhusu akaunti hiyo ikiwa pamoja na tarehe akaunti hiyo ilipo tengenezwa, pia utaweza kuona majina ambayo akaunti hiyo ilishawahi kuyatumia, pia utaweza kuona akaunti hiyo inatumiwa na mtu kutoka nchi gani pamoja na mambo mengine mengi kama matangazo yanayoendelea kwenye akaunti hiyo na mambo mengine mbalimbali.
- Sasa Unaweza Kuomba Uhakiki ili Kupata Tiki ya Blue
Hatimaye sehemu ya kuomba uhakiki sasa itanza kupatikana hivi karibuni, sehemu hiyo ilikuwa ikifanyiwa majaribio siku za awali na hatimaye sasa sehemu hiyo inakuja rasmi hivi karibuni. Sehemu hiyo itapatikana kupitia sehemu ya Settings kisha mwisho kabisa utaona sehemu ya Request Verification, kupitia sehemu hiyo unatakiwa kujaza fomu ambayo itakuruhusu kuomba uhakiki wa akaunti yako kwa urahisi na haraka.
- Sasa Utaweza Kuweka Ulinzi Zaidi wa Akaunti Yako
Kama ulishawahi kusoma makala yetu ya jinsi ya kuweka ulinzi kwenye akaunti za mitandao ya kijamii utagundua kuwa instagram inatumia njia ya kutuma ujumbe mfupi kuweza kupokea code ambazo ndio utatumia kuweza kufungua akaunti yako. Sasa hivi karibuni mtandao wa Instagram unafanya mabadiliko na kuleta njia mpya ya kuweza kuweka ulinzi zaidi kwa kutumia App nyngine kama Google Authenticator na Authy 2-Factor Authentication ambazo hizi hutumika kuweka ulinzi zaidi kwenye akaunti mbalimbali.
Kupata sehemu hiyo unatakiwa kubofya kwenye sehemu ya Settings kisha bofya sehemu iliyo andikwa Two-Factor Authentication na hapo utaweza kuseti njia unayoitaka kutumia kuweka ulinzi ikiwa pamoja na njia ya kutumia App nyingine kuweka ulinzi kwa kubofya sehemu ya Authentication App.
Sehemu zote hizi zinatarajiwa kuanza kupatikana hivi karibuni kupitia App zote za Instagram, hivyo hakikisha unapakua toleo jipya la App ya Instagram kupitia masoko ya Play Store pamoja App Store.