Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

Fahamu maana ya alama hizi zinazopatikana kwenye vifaa vya elektroniki
Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

Mara nyingi pale unapo nunua kifaa kipya cha eletroniki tunakutana na vitu mbalimbali vya kueleza jinsi ya kutumia vifaa hivyo, lakini ni watu wachache sana ambao huwa na muda wa kusoma vielelezo hivyo ambavyo huonyesha matumizi sahihi ya vifaa hivyo.

Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo itakujulisha angalau kidogo kuhusu alama ambazo mara nyingi zinapatikana nyuma au ndani ya kifaa chako cha electroniki, alama hizi huwa na maana mbalimbali na nyingine ni muhimu sana wewe kuzijua kama mtumiaji. Basi kabla ujachoka basi twende tukangalie alama hizi.

Advertisement

WEEE (Waste Electric & Electronic Equipment)

Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

Alama ya WEEE au (Taka Umeme na Vifaa vya Elektroniki) inaashiria kuwa bidhaa imekidhi mahitaji yaliyowekwa na Umoja wa ulaya ya utupaji wa taka za kieletroniki. Alama hii inaonyesha kuwa kifaa hicho kinapo isha muda wake kinapaswa kutupwa kwenye vituo maalum vya kukusanya taka za eletroniki na sio kwenye sehemu za kawaida za takataka.

FCC (Federal Communications Commission)

Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

Alama ya FCC ni alama inayo onyesha tume maalum ya marekani ya udhibiti wa vifaa vya elektroniki vinavyotumia wireless. Jukumu la tume ya FCC ni kuhakikisha kuwa kifaa chenye uwezo wa wireless kinafanya kazi kama inavyotarajiwa na haisababishi shida zozote za muingiliano na kifaa kingine ambacho pia kinatumia wireless. Ikiwa kifaa hakina alama hii, basi hakita ruhusiwa kuuzwa au kuingia katika soko la Marekani.

Conformité Européenne

Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

Alama hii inatumika zaidi kwenye vifaa mbalimbali vinavyo tumika au kuuzwa kwenye nchi za umoja wa ulaya, alama hii pia ina maana ya kuwa kifaa hicho kimekidhi vigezo vya usalama wa afya, pamoja na kukidhi viwango vya usalama wa mazingira kwa bidhaa zinazouzwa katika eneo la Umoja wa Ulaya au EU.

China Compulsory Certificate

Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

Alama ya CCC ni alama inayojulikana kama cheti cha ubora na usalama kwa bidhaa mbalimbali za kieletroniki zilizoingizwa, kuuzwa au kutumiwa katika soko la China. Alama hii Ilianza kutekelezwa Mei 1, 2002 na ikaanza kutumika kwa ulazima mnamo Agosti 1, mwaka 2003.

CE R&TTE Directive

Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

Alama hii inaonyesha kuwa kifaa kinakiuka kanuni teknolojia ya wireless kwa nchi moja au zaidi. Kwa mfano iPhone inakiuka kanuni ya Ufaransa ambayo inataka vifaa vyote vinavyo tumia teknolojia ya wireless, wakati vikiwa vinatumika kwenye mazinhira ya wazi ni lazima vifanye kazi ndani ya vipimo vya wireless vya GHz 2.4 hadi GHz 2.454. Kama kifaa hicho kitakuwa kina uwezo zaidi ya huo huwekewa alama kama kifaa cha hatari kwa daraja la II. Hii utofautiana kwa kila nchi.

China RoHS

Fahamu Maana ya Alama Hizi Kwenye Vifaa vya Elektroniki

RoHS ni kifupi cha Kizuizi cha Mazingira Hatari, na hii ni kanuni ya serikali ya China kudhibiti vifaa vya kielectroniki vyenye madini hatarishi kwa afya ikiwa pamoja na vifaa vyenye madini ya risasai au Lead. Bidhaa ambazo zina alama moja kati ya hizo huwa na maana ya tathimini ya Matumizi ya Kirafiki ya Mazingira (EFUP) kwa kifaa husika kwa miaka.

Alama hii huonyesha kipindi cha miaka ambapo kifaa hicho kinatakiwa kutumiwa bila kuwa na uwezekano wa madini hayo hatarishi kuvuja, na kusababisha madhara kwa afya na mazingira. Kwa mfano kama alama hiyo ina ishara ya mishale iliyozunguka yenye 10 ndani yake basi maana yake ni kuwa kifaa hicho kinapaswa kuwa salama kwa matumizi katika miaka 10 ijayo toka kilipo tengenezwa rasmi.

Na hizo ndio maana za baadhi ya alama ambazo zinapatikana kwenye vifaa mbalimbali vya kielekrtoniki, kumbuka bado zipo alama nyingi sana zenye maana tofauti hivyo hakikisha unakuwa na mtindo wa kusoma vitabu vya maelekezo vinavyokuja na kifaa chochote cha elektroniki unacho nunua kwani unaweza kupata maelezo ya muhimu sana ambayo ni vyema kutambua kuhusu kifaa chako. Kwa makala nyingine kama hizi unaweza kutembelea kipengele cha je wajua.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use