Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Vodacom Tanzania Kupitia M-pesa Yaja na Huduma Mpya ya Songesha

Sasa malizia miamala ya kupitia M-Pesa hata kama huna Salio la kutosha
Vodacom Tanzania Kupitia M-pesa Yaja na Huduma Mpya ya Songesha Vodacom Tanzania Kupitia M-pesa Yaja na Huduma Mpya ya Songesha

Miezi kadhaa iliyopita kulikuwa na habari kuwa kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania inajiandaa kuja na huduma mpya ambayo itasaidia wateja wake wa M-Pesa kupata mkopo wa haraka pale wanapokuwa wamepungukiwa fedha wanapofanya miamala kupitia huduma ya M-pesa. Hivi leo hatimaye huduma hiyo imewezeshwa na itakuwa inajulikana kama SONGESHA.

Advertisement

M-Pesa Songesha ni Nini

Songesha ni huduma mpya ya (Overdarft) kutoka Vodacom Kupitia M-pesa, huduma hii itawezesha watumiaji wa M-Pesa kukamilisha miamala mbalimbali pale pesa zinapo pelea kwenye akaunti zao.

Unajiungaje na Songesha

Ili kujiunga na huduma hii ya Songesha mteja wa Vodacom anatakiwa kubofya Menu ya M-Pesa *150*00# kisha baada ya hapo anatakiwa kuchagua Namba 6 ambayo ni Huduma za Kifedha, kisha bofya namba 5 ambayo ni SONGESHA. Baada ya hapo unatakiwa kusoma vigezo na masharti kisha kubali vigezo hivyo na moja kwa moja utakuwa umejiungana huduma hiyo mpya ya Songesha.

Kupitia Songesha Hadi Kiwango Gani Unaruhusiwa Kutumia

Kwa mujibu wa maelezo yaliopo kwenye Menu ya huduma hiyo, kiwango cha mwisho kina tofautiana baina ya mteja na mteja na pia kiwango hicho kinaweza kubadilika mara kwa mara. Kwa maoni yangu binafsi kama ilivyo huduma za Overdraft za mabenki, matumizi ya huduma za Vodacom hasa M-Pesa ndio yanayo tabiri kiwango chako cha salio kupitia huduma hiyo ya Songesha.

Huduma Zinazowezeshwa na Songesha

Sio kila miamala inaweza kuwezeshwa kwa huduma hiyo ya Songesha, kupitia Menu ya huduma hiyo Vodacom imeainisha miamala ifuatayo ndio itaweza kupata mkopo au Overdraft pale unapokuwa una salio la kutosha.

  • Kutuma Pesa kwa wateja wa M-Pesa
  • Kulipa Bili Mbalimbali kwa kutumia M-Pesa (Luku, Usafiri, Visimbusi, Ada za Serikali n.k)
  • Pale unapotumia M-Pesa kulipia vitu mbalimbali (Lipa kwa M-Pesa)

Makato ya Kutumia Huduma ya Songesha

Kutakuwa na makato au ada ambayo utalipia kwa kila mkopo wa Songesha unaomba, Kama ilivyo huduma za Overdraft za mabenki mara nyingi kiasi cha ada kinategemeana na kiasi ulichoomba au ulichotumia kupitia huduma hiyo. Ada huwa kidogo pale unapo kopa Overdraft au pesa kidogo na Ada huwa juu pale unapo Overdraft pesa nyingi. Vilevile Ada hutozwa kila siku kadri pesa hiyo inapokaa bila kulipwa.

Jinsi ya Kutumia Huduma ya Songesha

Kama wewe ni mteja wa Vodacom unaweza kujinga kwanza na huduma hii kwa kutumia Menu ya M-Pesa kisha chagua Namba 6 kisha Chagua Namba 5, Baada ya kujiunga unaweza kupata mkopo au Overdraft pale unapofanya miamala inayoruhusiwa. Sasa ili kupata mkopo huo unatakiwa kufanya muamala wakati huna salio la kutosha kwenye akaunti yako ya M-Pesa, hakikisha unafuata hatua zote na pale unapo maliza kudhibitisha subiri kidogo utaletewa Ujumbe ambao unakutaka kujua kama una salio lakini unaweza kupata mkopo huo wa Overdraft.

Meseji hiyo ni kama zile meseji za kufanya miamala ambazo zinahitaji kujaza chaguo lako, hivyo baada ya kudhibitisha muamala wako endelea kusubiria hapo hapo bila kuzima simu wala kubofya kitufe chochote kwenye simu yako. Baada ya kudhibitisha kwa kubofya 1 na moja kwa moja muamala uliokuwa unafanya utawezesha na utaletewa meseji ya kiwango unachotakiwa kulipa kwa siku.

Kwa sasa hayo ndio machache kuhusu huduma ya Songesha ya Vodacom kupitia M-Pesa, yapo mambo mengi sana ya muhimu ya kufahamu kupitia huduma hii hivyo kama unataka kujua zaidi kuhusu huduma hii tembelea tovuti ya Vodacom Tanzania hapa, pia unaweza kutembelea maduka ya Vodashop au piga 100 kupata msaada zaidi.

13 comments
  1. Mwanzoni nilikuwa natumia huduma ya songesha ila kwasasa naambiwa “songesha haiwezi kukamilisha muamala huu” nimetoa taarifa na nikaambiwa within 48 hrs nitapewa majibu lakini naelekea kumaliza wiki kimya kimya.

    1. songesha niliwapenda ila duuuh safar hii mmenifanyia kitu hadi nikilala naskia naumwa yaan elfu 13 mmekata 17 wakat deni hata wiki halijamaliza asee nyie mungu anawaona

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use