The LuDela Mshumaa Unaowashwa kwa Kutumia Programu

LuDela ni Mshumaa wa Kisasa unaotumia programu Maalumu ya Simu (App) ili kuwasha na kuzima
ludela-mshumaa-unaowashwa-kwa-programu ludela-mshumaa-unaowashwa-kwa-programu

LuDela ni mshumaa wa kisasa ambao si sawa na ile ambayo tumeshawahi kuiona yenye kutumia teknolojia ya LED, bali huu ni mshumaa kabisa unaotengenezwa na Nta halisi kabisa inayo tokana na nyuki kama ilivyo mishumaa mingine. Tofauti ya mshumaa huu ni kwamba una uwezo wa kutumia programu maalum kuwasha au ku-uzima mshumaa huu.

Mshumaa huu pia unao mfumo wa usalama ambayo ni pamoja na kuzima kwa muda maalum na pamoja na mfumo maalum wa kuzuia mshumaa huo kuleta majanga ya moto, pia wataalamu wa kutoka katika kampuni hiyo ya LuDela iliyotengeneza mshumaa huo wanasema kuwa wanao mpango wa kuongeza mfumo maalum wa sauti yani (voice recognition) kwenye mshumaa huo.

Advertisement

Mshumaa huo utaanza kuuzwa kwa maagizo ya awali yani (Pre Order) kwenye tovuti yao ya LuDela.com hapo mapema leo, Mshumaa huo unatarajiwa kuuzwa kwa dollar za marekani $100 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 218,735.00 bei hii ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya tarehe 21-09-2016.

Vipi je ungependa kuwa nao mshumaa huu ndani kwako.. ? tuandikie maoni yako hapo chini, pia usikuose habari zote za teknolojia kwa kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use