Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tafuta Kazi kwa Urahisi Kupitia App Mpya ya Loko Find

Unao ujuzi wako binafsi..? Jaribu app ya Loko Find Sasa
Tafuta Kazi kwa Urahisi Kupitia App Mpya ya Loko Find Tafuta Kazi kwa Urahisi Kupitia App Mpya ya Loko Find

Tanzania Tech Media tunakuleta app mpya ya Loko Find. Kama wewe umekuwa ni mmoja wa watu wenye ujuzi wa kufanya mambo mbalimbali basi naku karibisha sasa ujaribu kutumia ujuzi wako kupitia app mpya ya Loko Find, app hii ni tofauti na app nyingine kwani inakupa uwezo wa kutafuta kazi na kutangaza kazi na mambo mengine mbalimbali kwa urahisi zaidi.

Loko Find

Tafuta Kazi kwa Urahisi Kupitia App Mpya ya Loko Find

Advertisement

Loko Find ni App inayo kusaidia kupata huduma kupitia fundi au watoa huduma walio karibu na wewe. Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotaka kupata huduma kwa haraka basi jaribu app ya Loko Find. Kupitia App ya Loko Find utaweza kuona mafundi au watoa huduma mbalimbali na utaweza kuwapa kazi zako moja kwa moja. Pia unaweza kutangaza kazi kwa mafundi au watoa huduma mbalimbali na utaweza kupata huduma kutoka karibu na eneo ulilopo.

App ya Loko Find ni rahisi kutumia na kitu cha msingi unacho hitaji ni kutengeneza akaunti kwa kutumia barua pepe yako na baada ya hapo unatakiwa kuhakiki akaunti yako kwa kubofya link iliyopo ndani ya barua pepe tutakayo kutumia. App hii ya Loko Find ni kwa ajili ya wateja wanao tafuta kupata huduma mbalimbali, kama wewe ni mtoa huduma kwa namna moja ama nyingine unaweza kujisajili na toleo leo Loko Find kwa ajili ya Watoa huduma.

Sifa za App ya Loko Find

  • Utaweza kutangaza kazi kwa watoa huduma mbalimbali walio karibu na wewe, hii ikiwa ni bila kujali eneo ambalo utakuwa baadae.
  • Chat na watoa huduma walio karibu na wewe kabla ya kuwapa kazi yoyote.
  • Angalia malipo pamoja na madeni mbalimbali unayo daiwa na fundi au mtoa huduma.
  • Angalia muda wa kazi kwa kutazama kazi zinazo endelea, hii ni muhimu kama umetoa kazi kwa mtoa huduma au fundi ambaye amechagua kulipwa kwa saa.
  • Angalia wasifu wa mtoa huduma kabla ya kukupa huduma, hii itakusaidia kuona uwezo wa mtoa huduma, kazi za awali alizofanya na mambo mengine mbalimbali.
  • Fanya booking ya huduma au fundi kwa haraka kisha fanya malipo pale kazi itakapo fanyika, kumbuka pia ni muhimu kuangalia gharama za booking za mtoa huduma.

Loko Find Business

Tafuta Kazi kwa Urahisi Kupitia App Mpya ya Loko Find

Kama wewe ni mmoja wa watoa huduma wa kitanzania basi jaribu app ya Loko Find Business, app hii inakupa nafasi ya kuweza kupata kazi kupitia eneo ulilopo bila ya kuwa na wasi wasi kama haupo kwenye ofisi yako au eneo lako la kazi.

App ya Loko Find Business inafanya kazi vizuri kwa kutumia mfumo wa ramani ambayo huonyesha wateja kama upo karibu na yeye hivyo huweza kuwasiliana kwa ajili ya kutoa huduma. Kupitia app ya Loko Find Business utaweza kufanya mambo mengi sana ikiwa pamoja na kupokea booking, kupokea meseji kutoka kwa mteja, utaweza kuona kazi zote zinazo lingana na wasifu wako pamoja na mambo mengine mengi.

Sifa za Loko Find Business

  • Utaweza kuomba kazi moja kwa moja kutokana na ujuzi wako
  • Utaweza kupokea booking moja kwa moja
  • Utaweza kuchat na mteja
  • Utaweza kuona kazi zinazoendelea na mambo mengine mengi

App ya Loko Find Business ni kwa ajili ya watoa huduma, kama unataka app ya Loko Find kwaajili ya wateja unaweza kupakua app hiyo hapo juu.

App za Loko Find na Loko Find Business zote zinafanyakazi kwa pamoja, app hizi kwa sasa zipo kwenye hatua ya majaribio na tuna kukaribisha kutoa maoni kuhusu app hizi pamoja na kuuliza maswali mbalimbali juu ya utumiaji.

Wasiliana Nasi

Kwa maelezo zaidi kama unataka kujua zaidi au kujua jinsi ya kutumia app ya Loko Find basi hakikisha una wasiliana nasi hapa

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use