Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Post za Instagram (2022)

Njia hii inafanya kazi kwa asilimia 100 bila kujali unao followers wangapi
Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Post za Instagram (2022) Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Post za Instagram (2022)

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Instagram basi ni wazi kuwa ulishawahi kujaribu kuweka link kwenye post zako za Instagram bila mafanikio, lakini hivi karibuni Instagram imeleta njia mpya ya kuweka link kwenye post zako kwa urahisi na haraka.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia hii ambayo unaweza kutumia kuweka link kwenye post zako kwenye mtandao wa Instagram. Njia hii ni rahisi na inafanya kazi kwa mtu yoyote bila kujali kiasi cha follower ulichonacho.

Advertisement

Kwa kuanza moja kwa moja unatakiwa kuingia kwenye soko la Play Store au App Store, kisha moja kwa moja hakikisha una update au una sasisha toleo jipya la app ya Instagram.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Post za Instagram (2022)

Baada ya ku-update app yako ya Instagram, moja kwa moja endelea kwa kufungua app ya Instagram kisha moja kwa moja bofya sehemu ya Stories ili kuweka Storie.

Unaweza kupata sehemu hii kwa kutembelea profile yako kwa kubofya chini upande wa kulia, kisha moja kwa moja bofya profile picture yako na utaona sehemu ya Stories imefunguka moja kwa moja.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Post za Instagram (2022)

Baada ya sehemu ya Stories kufunguka chagua picha unayotaka kuweka au video, kwa kubofya chumba kilichopo upande wa kushoto chini, au unaweza kurekodi video fupi kwa kubofya kitufe cha kurekodi.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Post za Instagram (2022)

Baada ya kuweka picha au video moja kwa moja bofya sehemu ya Sticker kisha moja kwa moja chagua sticker ya link ambayo inapatikana kwa picha iliyo chorwa link, kama hujaona sticker hii endelea kupitia ukurasa huo kwa kushuka chini.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Post za Instagram (2022)

Baada ya kuchagua sticker ya link moja kwa moja endele kwa kuandika link yako kwenye sehemu iliyo wazi kisha moja kwa moja bofya Done iliyopo juu upande wa kulia juu, kisha weka stika yako mahali unapotaka kwenye picha yako.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Post za Instagram (2022)

Baada ya hapo moja kwa moja post storie yako kwenye ukurasa wako wa Instagram na link yako itaweza kuonekana kwa watumiaji wako kwenye sehemu hiyo. Kumbuka Stories hudumu ndani ya masaa 24 hivyo ni vizuri kujua kuwa link yako itakuwa inaonekana ndani ya masaa 24.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Post za Instagram (2022)

Kwa sasa hiyo ndio njia ambayo unaweza kutumia kuweka link kwenye post zako za Instagram, kwa mujibu wa habari mbalimbali instagram imetangaza kuwa haina mpango wa kuweka link kwenye post za kawaida kwani hadi sasa unaweza kuweka link kwenye bio, kwenye video za IGTV, pamoja na sehemu ya Stories.

Kama kwa namna yoyote hujaona link ya Sticker kwenye hakikisha una update app ya Instagram na pia hakikisha unafungua app ya Instagram na kufungua baada ya ku-update. Kama bado hujaona sehemu hiyo basi subiria ndani ya siku chache utaona sehemu hii mpya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use