Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hatua za Jinsi ya Kuweka Link Kupitia Mtandao wa TikTok

Utaweza kuwa link kwenye akaunti yako kupitia mtandao wa Tiktok
Hatua za Jinsi ya Kuweka Link Kupitia Mtandao wa TikTok Hatua za Jinsi ya Kuweka Link Kupitia Mtandao wa TikTok

Tiktok ni moja ya mtandao maarufu kwa sasa, mtandao huu kwa sasa una zaidi ya watumiaji Bilioni 1 kila mwezi, takwimu hizi ni hadi kufikia mwezi January mwaka huu 2022.

Hatua za Jinsi ya Kuweka Link Kupitia Mtandao wa TikTok

Advertisement

Kutokana na mtandao wa Tik Tok kutumiwa na watu wengi zaidi ni wazi kuwa kila mtumiaji anatakiwa kuwa kwenye mtandao huu. Kama bado huja download app ya Tiktok, basi huu ni muda sahihi wa kufanya hivyo.

Kupitia makala ya leo nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kuweka link kwenye bio yako moja kwa moja kwenye mtandao wa Tiktok. Njia hii ni rahisi na unaweza kufanya moja kwa moja kwenye simu yako.

Badilisha Akaunti Kuwa ya Kibiashara

Kwa kuanza unatakiwa kupakua app ya Tiktok, kisha tengeneza profile. Kumbuka hutoweza kuweka link kwenye bio yako hadi utakapo badilisha ukurasa wako kuwa ukurasa wa kibiashara.

Unaweza kubadilisha profile yako ya Tik Tok kuwa ya kibiashara kwa kufuata maelezo marahisi yafuatayo.

Baada ya kutengeneza kurasa yako moja kwa moja bofya kwenye profile yako kisha vitufe vitatu vya menu vilivyopo juu upande wa kulia.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Video Kupitia Mtandao wa TikTok

Baada ya hapo moja kwa moja utaona Settings mbalimbali na chagua sehemu ya Manage account ambayo ni ya kwanza kabisa.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Video Kupitia Mtandao wa TikTok

Baada ya hapo moja kwa moja bofya sehemu ya Switch to Business Account. Baada ya hapo bofya Next kuendelea na fuata maelekezo yote ili kukamilisha hatua zote.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Video Kupitia Mtandao wa TikTok

Weka Link Kwenye Bio TikTok

Baada ya kuchagua Category na kufanya setup ya ukurasa wako moja kwa moja hatua ya mwisho bofya Edit Profile.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Video Kupitia Mtandao wa TikTok

Baada ya kubofya hapo sasa unaweza kuendelea kwa kuweka link kwenye bio kwa kupitia sehemu ya Bio kama unavyoweza kuona hapo chini.

Jinsi ya Kuweka Link Kwenye Video Kupitia Mtandao wa TikTok

Baada ya hapo moja kwa moja unaweza kuendelea kwa kutengeneza bio yako kupitia hapa, unaweza kutengeneza bio yenye mitandao yako ya kijamii, biashara au hata kitu chochote ambacho unataka kuonyesha watu.

Kwa kufuata hatua hizi utakuwa umeweza kuweka link kwenye akaunti yako ya TikTok, pia bila shaka utakuwa umeweza kubadilisha akaunti yako kuwa akaunti ya kibiashara.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use