Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Achana na Internet ya Wi-Fi Sasa Kuna Internet Mpya ya Li-Fi

Inasemekana Internet ya Li-Fi ina speed zaidi kuliko Internet ya Wi-Fi
Teknolojia Mpya ya Li-Fi Teknolojia Mpya ya Li-Fi

Teknolojia inaendelea kukuwa kila siku na kila siku wataalamu wa mambo haya hufanya maboresho ya teknolojia zilizpo sasa na kufanya maboresho ambayo huweza kuleta aina mpya za teknolojia.  Hivi karibuni wataalamu kupitia mkutano wa CES 2019 wameonyesha aina mpya ya teknolojia ya Li-Fi ambayo huenda ikaja kuwa mbadala wa teknolojia ya Wi-Fi.

Tofauti na Wi-Fi, Li-Fi hufanya kazi tofauti kabisa na teknolojia ya Wi-Fi kwani hii hutegemea zaidi mwanga wa balb (Taa) ya LED kuliko mawimbi ambayo hutegemewa na teknolojia ya Wi-Fi. Mfumo mzima wa Li-Fi ni tofauti kabisa kwani mwanga wa LED unao tengenezwa na build ya LED ndio hutoa mawimbi ya internet ambayo huwa na kasi zaidi kuliko Wi-Fi.

Advertisement

Sasa kampuni moja ya Oledcomm, kupitia mkutano wa CES 2019 imefanikiwa kuleta teknolojia hii ikiwa kwenye hatua za awali na kuweza kuonyesha jinsi ilivyo weza kuunganisha watu zaidi ya 5 kwenye internet ya Li-Fi ambayo ilikuwa inatoka kwenye taa ya LED iliyokuwa imefungwa kwenye chumba hicho.

Li-Fi mfano

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu ili kutumia Internet hiyo mpya ya Li-Fi, inakuhitaji kuwa na aina mpya ya Moderm ambazo pia zitakuwa na uwezo wa kuchukua Internet kutoka kwenye mwaka huo wa LED ambao hauonekani kwa macho.

Japo kuwa teknolojia hii bado iko kwenye hatua za awali sana lakini tegemea kuona teknolojia hii kwenye miaka inayokuja, kwani teknolojia hii inauwezo wa kuongeza kasi zaidi ya Internet na kufanya watu kuwasiliana kwa urahisi zaidi na kwa haraka. Kwa sasa bado teknolojia hii haina vitu vingi bora kama ilivyo Wi-Fi, kwani hata speed ya Internet hiyo bado haijafikia malengo yaliyotakiwa.

Kwa habari zaidi kuhusu mkutano wa CES 2019 ambao umanza rasmi siku ya leo, endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, Pia unaweza kutembelea ukurasa wetu wa CES 2019 kujua zaidi kuhusu teknolojia nyingine mpya zilizo zinduliwa kwenye mkutano huo.

4 comments
  1. Happy new year Wadau hongereni kwa kazi nzri ya kutujuza mambo yaliojicha na kutuoa elimu kwa mapana na marefu hongereni sana

    Naomba msaada katika hili suala cm Yang ya IOS inachemka sana napo tumia internet naombeni msaada

    Wako mwanafamilia wa TANZANIATECH.ONE

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use