Wakati ikiwa ni tarehe ya kwanza ya mwaka mpya 2018, teknolojia nayo inazidi kusonga mbele na kukua kila mwaka. Kampuni ya LG imeuanza mwaka 2018 kwa kuonyesha teknolojia mpya ya TV ambayo pengine siku za usoni ndio itakuwa gumzo na kuwa moja ya teknolojia za TV zinazoitajika na watu wengi zaidi.
Hivi karibuni kampuni hiyo imetangaza kuwa kuptia mkutano wa vifaa vya kieletroniki wa CES ambao unafanyika kila mwaka, kampuni hiyo itaruhusu wateja wake kwa mara ya kwanza kuona TV ya kwanza kubwa kuliko zote na yenye teknolojia kubwa kuliko zote yaani uwezo wa 8K.
Wakati mwanzo TV kubwa kuliko zote duniani ilikuwa na inch 77 pamoja na teknolojia ya 4K, sasa kampuni ya LG imesema imefanikiwa kuvunja rekodi hiyo na kuja na TV hiyo ambayo itakuwa ya kwanza duniani yenye ukubwa wa inch 88 na yenye teknolojia hiyo ya 8K.
Kwa sasa tumefanikiwa kupata muonekano wa mbele wa TV hiyo, lakini endelea kuwa nasi tutakuwa tukikuletea matukio yote yanayojiri kwenye mkutano wa CES 2018 bila kusahau picha na video za TV hiyo kubwa kuliko zote duniani.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.