Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

LG Yatangaza Rasmi Kusitisha Biashara ya Smartphone

LG inatarajia kukamilisha kusitishwa kwa biashara yake ya smartphone ifikapo Julai 31
LG Yatangaza Rasmi Kusitisha Biashara ya Smartphone LG Yatangaza Rasmi Kusitisha Biashara ya Smartphone

Kampuni ya LG hivi karibuni imetangaza kuwa inajitoa rasmi kwenye biashara ya smartphone duniani kote, kwa mujibu wa tovuti ya LG kampuni hiyo inatarajia kusitisha biashara yake ya smartphone kuanzia  mwaka huu huku ikitangaza kuwa bidhaa zilizopo sokoni zitaendelea kuuzwa hadi hapo stock itakapo kwisha.

LG inasema katika tangazo lake, lililo chapishwa kwenye tovuti ya LG Newsroom, kwamba bodi yake ya wakurugenzi imeidhinisha uamuzi wake wa kutoka kwenye soko la simu janja. Huku idai kuwa huo ni uamuzi wa kimkakati wa LG kutoka kwenye “sekta ya simu janja ambayo kwa sasa ina ushindani mkubwa zaidi.”

Advertisement

LG imeandika kuwa hatua hii itaruhusu kuelekeza rasilimali zake kwenye masoko mengine na uwezo mkubwa wa ukuaji kwenye masoko mengine kama vile, vifaa vya magari ya umeme, Smart Home, AI, na huduma nyingine mbalimbali.

LG Yatangaza Rasmi Kusitisha Biashara ya Smartphone

LG inatarajia kukamilisha kusitishwa kwa biashara yake ya smartphone ifikapo Julai 31. Kampuni hiyo pia itafanya kazi na wasambazaji wake na washirika wa biashara kufunga biashara yake ya smartphone.

Hata hivyo kampuni hiyo imetangaza kuwa, Watumiaji wa simu za LG kwa sasa wataendelea kupata huduma kwa wateja na update au sasisho kwenye simu zao “kwa muda wa kipindi maalum” kulingana na mahali mtumiaji alipo.

Kwa mujibu wa tovuti ya LG Korea, LG inasema kuwa itatoa sasisho la Android 12 kwa vifaa vilivyo chaguliwa na sasisho za usalama, ingawa mipango yake inaweza kubadilika katika siku zijazo. Kampuni hiyo pia itaendelea na utoaji wa sasisho la Android 11 kwa simu zake za zilizopo, kama ilivyotangazwa hapo awali.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use