Kampuni ya Lenovo hivi karibuni imetangaza ujio wa laptop yake ya kwanza ambayo itakuwa ina kioo kinacho jikunja. Kama ilivyo simu ya Galaxy Fold, laptop hii nayo itakuwa ni kioo kitupu ambacho kitakuwa kinajikunja kwa katikati.
Laptop hiyo ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwanzoni mwa mwaka 2020, itakuja ikiwa na jina la Lenovo ThinkPad X1. Kwa mujibu wa tovuti ya Lenovo, inasemekana kuwa laptop hiyo itakuwa inatumia mfumo wa Android huku kioo chake cha inch 13 kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya OLED.
Mbali na hayo inasemekana kuwa kioo hicho kitakuwa na kimetengenezwa na kampuni ya LG ambapo kita kuwa na resolution ya 2k na kitakuwa hakina ukingo wa katikati. Vilevile inasemekana unapo ikuja laptop hiyo nusu ya kioo kilicho lala kitakuwa keyboard ambayo itakuwa ya touch na nusu ya pili iliyo simama itakuwa kioo.
Hata hivyo pia unaweza kutumia keyboard ya bluetooth ili kuepuka kuchafua kioo cha laptop hiyo ambayo ukweli kwa matumizi itakuwa ngumu sana kutumia ikizingatia ni lazima kuweka mikono juu ya laptop pale unapokua una andika kitu kwa kutumia keyboard hasa ya laptop.
Kwa sasa bado hakuna ripoti zaidi juu ya jinsi laptop hiyo itakavyo fanya kazi au ni mfumo gani wa Android laptop hiyo itakuwa inatumia, yote hayo pengine tutaenda kujua pale laptop hii itakapo zinduliwa hapo mwanzoni mwa mwaka 2020.