Lenovo Yazindua Laptop Mpya za ThinkPad X1 Carbon (2018)

Laptop nyingine ni X1 Yoga, X280, T480 pamoja na L Series.
Thinkpad X1 Carbon (2018) Thinkpad X1 Carbon (2018)

Kampuni ya Lenovo hapo jana imetangaza ujio wa matoleo yake mapya ya laptop za Lenovo ThinkPad X1 Carbon (2018) pamoja na laptop nyingine za Lenovo X1 Yoga, Lenovo X280, Lenovo T480 pamoja na toleo jipya la Lenovo L Series.

Kama ilivyo kawaida ya kampuni ya Lenovo, laptop hizi zime tengenezwa zaidi kwaajili ya biashara au wafanyabishara na mwaka huu laptop hizi zimekuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na kuwekewa processor mpya za Intel Core 8th-Gen CPU, kioo cha HDR displays, USB-C power adapters pamoja na sehemu za USB za Thunderbolt ikiwa pamoja na mabadiliko mbalimbali ya ulinzi.

Advertisement

ThinkPad X1 Carbon (2018)

Lenovo ThinkPad X1 Carbon (2018) inakuja ikiwa inasemekana kuwa ndio laptop nyepesi zaidi ya inch 14, Laptop hii imetengenezwa kwa kutumia advanced carbon fiber maalum ambazo ndio zinasemekana kufanya ThinkPad X1 Carbon kuwa nyepesi zaidi. Laptop hii inakuja na machaguo mbalimbali ya teknolojia za Vioo, yaani kuna laptop ya ThinkPad X1 Carbon yenye kioo chenye teknolojia ya Full HD IPS Display, kuna chaguo lingine la kioo cha Full HD IPS Display chenye uwezo wa Touchscreen.

Vilevile kuna ThinkPad X1 Carbon (2018) yenye vioo vyenye teknolojia za WQHD IPS pamoja na nyingine yenye teknolojia ya kioo ya WQHD IPS HDR yenye uwezo wa Dolby Vision. Laptop hii inaendeshwa na Processor ya 8th-Gen Intel Core processor, ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 16 na Hard Disk kubwa ya SSD yenye ukubwa wa Terabyte 1 (TB1).

Laptop hii pia inakuja na kamera mpya ya IR camera ambayo inaweza kutumika kwenye ulinzi wa kutambua uso au (facial recognition) pamoja na ulinzi wa kufuatilia macho au (eye tracking). Vilevile pia ThinkPad X1 Carbon (2018) inasemekana kuja na battery yenye uwezo mkubwa wa kudumu na chaji hadi masaa 6 pale inapo chajiwa na kujaa. Laptop hii pia inakuja na kava maalum linaloitwa ThinkShutter kwaajili ya kufunika kamera ya laptop hiyo pale inapokua haitumiki.

Lenovo ThinkPad X1 Yoga

ThinkPad X1 Yoga inakuja na uwezo wa kuzunguka kwa nyuzi 360° ambayo inaweza kufanya laptop hiyo kubadilika na kuwa tablet. Laptop hii pia inakuja na processor ya 8th-Gen Intel CPUs huku ikiwa na sifa nyingine kama zile za laptop ya X1 Carborn. Tofauti ya ThnkPad X1 Yoga na ThinkPad X1 Carborn ni kuwa, X1 Yoga inakuja na kioo chenye uwezo wa kuzunguka nyuzi 360 pamoja na uwezo wa kutumika kwa kutumia pen maalum pamoja na uwezo wa Mtandao wa Advanced LTE. Kwenye sifa zingine laptop hizi zinafanana.

Lenovo ThinkPad X280 na Lenovo X380 Yoga

Mbali na laptop za Lenovo X1, Lenovo pia imezindua laptop nyingine za ThinkPad X280 na Lenovo X380 Yoga ambapo Lenovo X280 inakuja na kioo cha inch 12.5 chenye teknolojia za kuchagua kati ya kioo chenye teknolojia ya HD, TN, FullHD IPS, pamoja na kioo chenye teknolojia ya FullHD IPS chenye uwezo touchscreen. Lenovo X280 pia inakuja na Processor ya Intel 8th-Gen Core i7 processor yenye kusaidiwa na RAM ya GB 16 pamoja na Hard Disk ya SSD ya Terabyte 1 (1TB).

Lenovo X380 Yoga na yenyewe inakuja ikiwa na uwezo wa kioo kuzunguka nyuzi 360, hivyo kufanya laptop hiyo kuweza kuwa tablet. Laptop hii inakuja na kioo cha inch 13 chenye teknolojia ya Full HD IPS display, kwa upande mwingine laptop hii ya Lenovo X380 Yoga inakuja na Hard Disk, RAM na Processor sawa na laptop ya Lenovo X280 lakini tofauti ni kuwa, Lenovo X380 Yoga inakuja na uwezo wa kutumia pen maalum pamoja na teknolojia ya kutambua uso (facial recognition) kwa kutumia kamera ya IR camera.

Lenovo ThinkPad T Series

Kwenye upande wa T Series, Lenovo imezindua laptop mpya za ThinkPad T480, T480s, na T580. Thinkpad T480 inakuja na kioo cha inch 14 ambacho kinakuja na teknolojia za kuchagua kati ya teknolojia ya HD,TN, pamoja na teknolojia ya Full HD yenye uwezo wa touchscreen. Vilevile laptop hiyo inakuja na processor ya Intel 8th-Gen Core i7 CPU yenye kusaidiwa na RAM ya GB 32 pamoja na ukubwa wa Hard Disk ya SSD wa Terabyte 1 (TB1). Vilevile wateja wataweza kuchagua laptop hii yenye uongezeko la Graphics ya Nvidia GeForce MX150 discrete GPU.

Matoleo ya ThinkPad T480s na T580 yenyewe yatakuja na vioo vya inch 15 yenye teknolojia za vioo za kuchagua kati ya kioo chenye teknolojia ya HD,TN, Full HD IPS, pamoja na Full HD IPS yenye uwezo wa touchscreen. ThinkPad T480s inakuja na RAM ya GB 24 wakati Thinkpad T580 inakuja na RAM ya GB 32. Laptop zote zinakuja na Hard Disk ya SSD yenye ukubwa wa 1TB, Kwa upande wa processor laptop zote zinakuja na processor ya Intel 8th-Gen Core i7 processors, ambayo unaweza kuchagua Graphics ya Intel UHD Graphics 620 au Graphics ya Nvidia GeForce MX150.

Lenovo ThinkPad L Series

Kwa wateja wanao hitaji laptop za bei nafuu lenovo imezindua laptop za bei nafuu za L series, ThinkPad L380, L380 Yoga, L480, pamoja na L580. Thinkpad L380 na L380 Yoga zinakuja na kioo cha inch 13.3 wakati Thinkpad L480 na L580 zinakuja na vioo vya inch 14 na inch 15. Kwa upande wa teknolojia za vioo hivyo wateja wanaweza kuchagua aina za teknolojia kama ilivyo kwenye laptop nyingine hapo juu. Laptop hizi kwa ujumla wake zinakuja na RAM ya GB 32 pamoja na Hard Disk ya GB 512. Wateja pia wataweza kuchagua kati ya laptop hizo zenye Graphics ya AMD Radeon 530 graphics card pamoja na Intel 620 integrated graphics.

BEI

Kuhusu bei Lenovo ThinkPad X1 Carbon itakuja ikiwa inauzwa kwa rupee za india ₹1,21,000 sawa na Tsh 4,210,000 na Lenovo ThinkPad X1 Yoga itakuja ikiwa inauzwa kwa rupee za india ₹1,26,000 sawa na Tsh 4,400,000 wakati ThinkPad X280 na Thinkpad X380 Yoga zitakuwa zina anzia rupee ya india ₹73,000 sawa na Tsh 2,600,000. Kwa upande wa ThinkPad T Series bei yake itanzania rupee za india ₹69,000 sawa na Tsh 2,400,000 huku ThinkPad L Series ikianzia rupee ₹54,000 sawa na Tsh 1,900,000. Kwa sasa laptop hizi zinapatikana nchini india na zitakuja nchi nyingine siku za karibuni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use