Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hii Ndio Laptop Nyembamba Kuliko Zote Duniani Kwa Sasa

Kama ulikua unajiuliza sana laptop gani ni nyembamba basi kwa sasa hii ndio laptop nyembamba kuliko zote duniani
laptop-nyembamba laptop-nyembamba

Linapokuja swala zima la kuangalia ni laptop gani ya kununua najua lazima utakua unajua kwa kupitia makala zetu zilizopita, lakini linapokuja swala la kununua laptop yenye muundo wa kisasa pamoja na teknolojia ya hali ya juu basi na hakika makala hii itakusaidia kujua hilo kwani leo tunaenda kuangalia kwa undani laptop nyembamba kuliko zote duniani.

Ukweli ni kwamba kuna laptop za aina nyingi sana zenye sifa na miundo tofauti tofauti lakini unapokuja kwenye swala la laptop nyembamba kuliko zote duniani mwaka 2016 lazima utaitaja laptop mpya ya Acer Swift 7, laptop hii ndio inayo shikilia rekodi ya kuwa laptop nyembamba kuliko zote duniani.

Advertisement

Ili kuifahamu vizuri laptop hii mpya nimepanga makala hii kwenye vipengele ili uweze kujua vizuri sifa mpaka muundo wa laptop hii kwa ujumla, basi kwa kuanza twende tukaangalie –

  • Muundo na Kioo cha Acer Swift 7

Acer Swift 7 imetengenezwa kwa rangi mbili rangi nyeusi pamoja na rangi ya gold trim ambayo inafanya laptop hii kuwa na mvuto wa hali ya juu sana, pia laptop hii inayo kioo cha inch 13 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya Full HD (1920 x 1080) pamoja na IPS display ikiwa na aspect ratio ya 16:9. Kioo hicho kimewekewa uliza na Glass ya Corning Gorilla ambayo inafanya kioo cha laptop hii kuwa kigumu zaidi, lakini laptop hii haina teknolojia ya Touch Screen kwenye kioo hicho hivyo ni vyema kukumbuka hilo.

  • Nguvu na Battery ya Acer Swift 7

Laptop ya Acer Swift 7 inatumia processor ya kizazi cha saba cha processor za intel yani 7th generation Intel Core processor, processor hizi zinasifika sana kwa kuwa na nguvu na kasi ya hali ya juu sana hivyo Acer Swift 7 imefanikiwa kuwa na nguvu ya hali ya juu kwa kuwa na processor ya Intel Core i5 chip yenye uwezo wa 1.2GHz, najua utakuwa unajiuliza kwanini processor hii ina uwezo wa 1.2GHz pekee.? kwa kifupi ni kwamba processor hii inapewa nguvu kubwa na RAM ya GB 8 inayo fanya laptop hii kuwa na kasi kubwa unapokua unafanya shughuli mbalimbali. Pia haija ishia hapo laptop hii ya Acer Swift 7 inauwezo wa kukaa na chaji kwa masaa tisa (9 hours) mpaka masaa kumi (10 hours) pale inapochajiwa ikajaa kabisa.

  • Ukubwa (Storage) na Port za Acer Swift 7

Katika upande wa ukubwa au Storage laptop ya Acer Swift 7 inatumia hard disk yenye ukubwa wa GB 256 ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya SSD. Ndio najua lazima utakuwa umeshangazwa na kiasi cha storage cha laptop hii pamoja na kuwa ni laptop yenye sifa ya kuwa ni laptop nyembamba kuliko zote duniani, Pia pengine Acer wangeangalia kwenye hili kwa kuongeza Storage zaidi pamoja na kuweka port za USB za kawaida kwani laptop hii haitumii port za kawaida za USB bali inatumia USB 3.1 Type-C ports ambazo hizi sio sawa na ambazo zimezoeleka na watumiaji wengi wa laptop hapa Tanzania.

Basi hayo ndio machache ambayo ni muhimu kuyajua kuhusu laptop hiyo mpya ya Acer Swift 7 ambayo inashikilia rekodi ya kuwa laptop nyembamba kuliko zote duniani kwa kuwa na wembamba wa millimeter 9.98 sawa na inch 0.39-inch. Pia laptop hii imetengenezwa maalum kwa Windows 10 na inauza kwa dollar za marekani $999 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 2,200,000.

Je unasemaje kuhusu laptop hii ya Acer Swift 7.? pamoja na kuwa na sifa ya kuwa laptop nyembamba kuliko zote duniani je sifa zake ni sawa na taji iliyojiapatia..? basi tuandikie maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use