Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook (2020)

Zifahamu sifa za MacBook Air (2020) na MacBook Pro (2020) zote za Inch 13
Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook (2020) Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook (2020)

Kampuni ya Apple hapo jana ilizindua laptop zake mpya ambazo pia ni laptop za kwanza kabisa kwa kampuni ya Apple kutumia processor ambayo imetengenezwa na kampuni hiyo kwa asilimia 100.

Tofauti na laptop nyingine ambazo tayari zimezinduliwa na Apple, laptop hizi mpya za MacBook Air ya Inch 13 na MacBook Pro ya Inch 13 zote zinakuja na uwezo mkubwa wa processor ikiwa pamoja na uwezo wa kutumia nguvu kidogo kuendesha processor hiyo.

Advertisement

Kifupi ni kuwa laptop hizi mpya zinakuja na nguvu zaidi ya processor huku zikitumia battery kidogo kuwezesha laptop hii kufanya kazi kubwa zaidi.

Sifa za MacBook Air 13-Inch (2020)

Tukianza na MacBook Air, laptop hii imeboreshwa na inakuja na processor mpya ya Apple M1, processor inayo kuja na uwezo wa hadi 8-core CPU, mbali na hayo processor hiyo pia inawezesha GPU ya MacBook Air (2020) kuwa na uwezo wa GPU yenye uwezo wa hadi 8-core

Kwa upande wa RAM, laptop hii mpya ya MacBook Air inakuja na RAM ya GB 8 huku ikiwa na uwezo wa kuongezewa hadi kufikia GB 16. Mbali na hayo, laptop hii pia inakuja na uhifadhi wa SSD ya hadi GB 256 huku kukiwa na toleo lingine lenye uhifadhi wa GB 512 ambayo pia ni SSD.

Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook (2020)

Kwa upande wa kioo laptop hii inakuja na kioo cha inch 13, kioo ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya Retina display huku kikiwa na uwezo wa resolution ya hadi pixel 2560 kwa 1600.

Kwa upande wa battery, MacBook Air 13-inch (2020) inakuja na battery yenye uwezo wa hadi watt 49.9 huku ikiwa na uwezo wa kudumu na chaji kwa muda wa hadi masaa 15 kama unatumia internet kupitia wireless, na hadi masaa 18 kama unaangalia movie.

Laptop hii pia inakuja na viunganishi mbalimbali kama vile port tatu 3 za Thunderbolt zenye speed ya hadi Gb40 kwa sekunde na USB 2 mbili za 3.1 Gen zenye speed ya hadi Gb10 kwa sekunde.

Bei na Upatikanaji

Laptop hii mpya tayari imeanza kupatikana kuanzia leo tarehe 11/11/2020 huku ikitegemewa kuwafikiwa wateja hivi karibuni. Kujua zaidi unaweza kusoma hapo chini kujua sifa kamili na bei ya MacBook Air 13-inch (2020) kwa hapa Tanzania.

Bei ya MacBook Air 13-inch (2020) Tanzania

Sifa za MacBook Pro 13-Inch (2020) ARM-Based

Kampuni ya Apple pia ilizindua laptop mpya ya MacBook Pro 13-Inch (2020) ambayo nayo pia inakuja na processor mpya ya Apple M1. Kwa upande wa sifa laptop hii haina tofauti sana na MacBook Air isipokuwa laptop hii inakuja na Touch Bar kwenye Keyboard yake.

Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook (2020)

Tofauti nyingine ni upande wa kioo ambapo MacBook Pro yenyewe inakuja na brightness ya hadi nits 500 wakati MacBook Air yenyewe inakuja na uwezo wa brightness ya hadi nits 400.

Pia vilevile laptop hii inakuja na uwezo mkubwa wa battery ambapo battery hiyo ina uwezo wa kudumu na chaji kwa muda wa hadi masaa 17 ukiwa unatumia internet kupitia wireless. Uwezo huo unawezeshwa na battery ya watt 58.2.

Mbali na hayo kila kitu kwenye laptop hiyo kinafanana kuanzia kioo, uwezo wa RAM, uwezo wa storage pamoja na sehemu za kuchomeka viunganishi mbalimbali. Kama unataka kujua tofauti za laptop hizi unaweza kusoma zaidi hapa.

Bei na Upatikanaji

Kama ilivyo laptop mpya ya MacBook Air 13-inch (2020), laptop hii pia tayari imeanza kupatikana kuanzia leo tarehe 11/11/2020 huku ikitegemewa kuwafikiwa wateja hivi karibuni. Kujua zaidi unaweza kusoma hapo chini kujua sifa kamili na bei ya MacBook Pro 13-inch (2020) ARM-Based kwa hapa Tanzania.

Bei ya MacBook Pro 13-inch (2020) ARM-Based Tanzania

Mac Mini (2020)

Mbali na hayo pia kampuni ya Apple hapo jana ilizindua toleo jipya la Mac Mini, desktop kompyuta ambayo nayo pia inakuja na processor mpya ya Apple M1.

Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook (2020)

Kompyuta hii pia inakuja na sifa zinazo fanana na sifa za MacBook Air huku yenyewe tofauti yake ikiwa ni dektop kompyuta hivyo unahitaji kuchomeka laptop hii direct kwenye umeme kuweza kutumia. Soma zaidi sifa za Mac Mini Hapa.

Kampuni ya Apple Yazindua Laptop Mpya za MacBook (2020)

Na hizo ndio bidhaa zote zilizo zinduliwa hapo jana kwenye tamasha la Apple “One More Thing” kama tamasha hilo lilikupita unaweza kuangalia hapa yote yaliyojiri ndani ya dakika 10 tu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use