Baada ya kampuni ya Huawei kupitia kampuni yake ya Honor kuzindua simu ya Honor 10, sasa Huawei imeamua kupanua uzalishaji wa kampuni hiyo kwa kuja na laptop ya kwanza kabisa kutoka kampuni hiyo inayoitwa Honor MagicBook.
Laptop hiyo inakuja ikiwa inafanana sura na Mackbook Pro ikiwa pamoja na kava lake la nje ambalo limetengenezwa kwa Aluminium kama vile ilivyo laptop ya MacBook Pro.
Mbali na kuja na muonekano kama MacBook Pro laptop hii mpya ya honor inakuja na kwa aina mbili tofuati za processor aina hizo ni processor ya Intel Core i7-8550U pamoja na processor ya Intel Core i5-8250U, Laptop yenye Processor ya Core i7 yenyewe itakuja ikiwa na RAM ya GB 8 pamoja na ukubwa wa HardDisk ya SSD ya GB 256, huku ile yenye processor ya Core i5 yenyewe itakuja na RAM ya GB 4 na ukubwa wa HardDisk ya SSD ya GB 256. Laptop zote hizi zinakuja na Graphics ya NVIDIA GeForce MX150.
Laptop hii ya Honor MagicBook inakuja na kioo cha inch 14 chenye teknolojia ya IPS Display Panel chenye uwezo wa resolution ya 1080p pamoja na uwezo wa rangi kwa asilimia 45% NTSC color, 800:1 contrast pamoja na 250 za brightness.
Mbali na hayo Honor MagicBook inakuja na sehemu ya USB-A 3.0 na USB-A 2.0, pamoja na sehemu ya HDMI port ikiwa sambamba na sehemu ya headphone ya 3.5mm headphone jack yenye uwezo wa kutumika kuchomeka headphone pamoja na kuchomeka MIC. Kwa upande wa spika laptop hii inakuja na spika 4 zenye teknolojia ya Dolby Atmos na dual mics, huku kwa pembeni laptop hii ikiwa inakuja na kitufe cha kuwasha ambacho kinakuja na uwezo wa ulinzi wa Fingerprint.
Battery ya laptop hii ya Honor MagicBook inasemekana kuja na uwezo wa 57Wh ambayo inayo uwezo wa kudumu na chaji kwa muda wa masaa 12 au 13 pale itakapo chajiwa na kujaa vizuri.
Kuhusu Bei laptop ya Honor MagicBook yenye processor ya Core i7 itakuja ikiwa inauzwa kwa Yuan ya china CNY 5,700 sawa na Tsh 2,075,000 na Honor MagicBook yenye processor ya Core i5 yenyewe itauzwa Yuan CNY 5,000 sawa na Tsh 1,820,000. Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kwa hapa Tanzania.
Iko poa sana
Nimeipenda