Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Laptop Mpya Zilizozinduliwa Hivi Karibuni (2018)

Hizi hapa laptop mpya zilizo zinduliwa hivi karibuni
Dell Inspiron 13 7000 2-in-1 Dell Inspiron 13 7000 2-in-1
Dell Inspiron 13 7000 2-in-1

Mkutano wa IFA 2018 umekaribia kufunga milango yake hivi karibuni, Mkutano huu hufanyika kila mwaka na umekuwa ni sehemu ya muhimu kwa makampuni mbalimbali ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki, kwani kupitia mkutano huo kampuni hizo hupata nafasi ya kuonyesha bidhaa zao mpya.

Baada ya kuona uzinduzi wa simu za Sony Xperia XZ3 na HTC U12 hebu sasa tuangalie upande mwingine na tuende kutazama laptop mpya 5 ambazo zilizinduliwa kwenye mkutano huo wa IFA mwaka huu 2018.

Advertisement

  • Asus ZenBook Inch 13, Inch 14,  Inch 15

Kampuni ya Asus nayo pia ikuwa kwenye mkutano wa IFA, kwenye mkutano huo kampuni hiyo ilipata nafasi ya kuonyesha laptop zake mpya za Asus ZenBook ambazo zinakuja na ukubwa tofauti. ZenBook (UX333) ya Inch 13, ZenBook (UX433) ya Inch 14 na ZenBook (UX533) ya Inch 15. Laptop hizi hazina tofauti sana na zinakuja na processor ya Core i8, GPU ya Nvidia GeForce GTX 1050 pamoja na RAM ya GB 16 na Hard Disk ya SSD. Laptop hizi zinatarajiwa kuingia sokoni kuanzia mwezi October.

  • Acer Swift 5

Kwenye mkutano huo wa IFA 2018, Kampuni ya Acer ilipata nafasi ya kuonyesha laptop yake mpya ya Acer Swift 5. Kama ilivyo laptop nyembamba kuliko zote duniani (Acer Swift 7), Kampuni ya Acer inadai kuwa Acer Swift 5 nayo pia inakuja na taji lake la kuwa laptop nyepesi ya kuliko zote ya Inch 15. Laptop hii inauzito wa gramu 22 na inakuja na procesor za kuchagua kati ya Core i5 na Core i7 pamoja na RAM hadi ya GB 16. Vilevile laptop hii inakuja na Hard Disk ya TB 1 ya SSD. Laptop hii inategemewa kupatikana kuanzia mwezi ujuo kwa dollar za marekani $1,099 sawa na Tsh 1,514,000.

  • Dell Inspiron 13 7000 2-in-1 (2018)

Kampuni ya Dell nayo ilikuwa kwenye mkutano wa IFA 2018. Kwenye mkutano huo kampuni hiyo ilitangaza laptop yake mpya ya 2 in 1, Laptop hiyo ya Dell Inspiron 7000 inakuja na ukubwa wa kioo wa Inch 13, mbili kati ya processor ya Core i5 na Core i7 pamoja na RAM kati ya GB 8 na GB 16 Huku ikiwa na Hard Disk ya kati ya TB 1 na GB 128 zote zikiwa ni SSD. Kama ilivyo maana ya laptop ya 2 in 1, laptop hii inakuja na uwezo wa Touchscreen hivyo unaweza kuitumia kama tablet na pia unaweza kuitumia kama Laptop. Dell Inspiron 13 7000 2-in-1 inategemea kupatikana kuanzia mwezi October tarehe 2.

  • Acer Predator Triton 900

Kwenye mkutano wa IFA 2018, kampuni ya Acer ilitawala sana kwani ilizindua zaidi ya laptop nne na Hii hapa ndio laptop nyingine ya Acer Predator Triton 900. Kama ilivyo jina lake Acer Predator ni laptop maalum kwaajili ya Game. Laptop hii bado haijatangazwa bei wala sifa kamili ila inatagemewa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao.

  • Lenovo Yoga Book C930

Kama wewe ni mpenzi wa laptop za 2 in 1 basi lazima utaipenda laptop mpya ya Lenovo Yoga Book C930. Laptop hii inakuja na processor ya Core i5 ambayo inasaidiwa na RAM hadi ya GB 8 pamoja na Hard Disk ya GB 256 ya aina ya SSD. Laptop hii kama lilivyo jina lake inakuja na uwezo wa kutumika kama tablet pia unaweza kutumia kama laptop ya kawaida. Lenovo Yoga Book C930 inategemewa kuingia sokoni kuanzia mwezi ujao.

Na hizo ndio laptop bora ambazo zimezinduliwa kwenye mkutano wa IFA 2018, Mkutano wa IFA unatarajiwa kumalizika tarehe 5 ya mwezi huu huko nchini ujerumani.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use