Niwazi kuwa karibia asilimia 80 ya wanafunzi na wafanyakazi wote wanamiliki laptop hii inatokana na umuhimu wa vifaa hivi hasa katika kutimiza majukumu ya kila siku ya wanafunzi au wafanyakazi.
Kuliona hilo leo nimekuletea makala hii ambayo itakusaidia kujua makosa mbalimbali ambayo inawezekana ulikuwa huyajui yanayoweza kuchangia laptop yako kuharibika kwa haraka. Natumaini makala hii itakuwa msaada kwa wanafunzi na wafanyakazi pamoja na wamiliki wote laptop.
TABLE OF CONTENTS
Kutumia Laptop Kwenye Sehemu Zinazozuia Laptop Kutoa Hewa
Asilimia kubwa ya wanafunzi huwa na tabia ya kufanya kazi kwenye sehemu ambazo sio rafiki na laptop, sehemu hizi ni pamoja na kitandani au sehemu ambazo zinazuia sehemu za kupitisha hewa kwenye laptop kushindwa kufanya kazi, hii husababisha laptop kupata joto sana na hivyo kushindwa kufanya kazi vizuri na matokeo yake kuharibika hasa kwenye maeneo ya processor.
Ni muhimu kutumia laptop yako sehemu ambayo itakaa juu na itaweza kupitisha joto na hatimaye kupoa haraka. Unaweza kutumia laptop yako sehemu ambayo ni ngumu na ipo sawa kama dawati au meza, hii itaweza kusaidia kupunguza joto kwenye laptop yako kwa urahisi na haraka.
Kutokujali Kuhusu Vumbi na Maji Kwenye Laptop Yako
Watu wengi hutumia muda mwingi kufanya kazi kwenye laptop zao bila kujali kuhusu vumbi na maji kwenye laptop. Vumbi ni adui mkubwa sana wa laptop na vumbi likiwa limejaa sana linaweza kusababisha processor ya laptop yako kushindwa kufanya kazi vizuri na hatimaye kuharibika. Kwa upande wa maji watu wengi hutumia maji kufuta au kupunguza vumbi kwenye baadhi ya sehemu za laptop bila kujali kuwa sehemu hizo huadhiriwa na maji kwa kiwango kikubwa.
Kufuta na maji sehemu za kioo cha laptop yako au kwenye sehemu za kupitisha hewa (ventilation) kwenye laptop yako ni hatari sana na hii inaweza kufanya laptop yako kupiga shoti au kupata tatizo lingine ambalo lina sababishwa na maji.
Kushika Laptop Yako Vibaya
Ni kweli kwamba kutokana na kutumia laptop zetu kila siku basi wakati mwingine tunajisahau na kuona kama laptop hizo ni ngumu kupitiliza. Mbali na hayo, laptop nyingi zimetengenezwa zikiwa na sehemu maalum za kushika na mara nyingi sehemu hizi huwa ngumu na imara kuliko sehemu nyingine ambazo sio zakushika laptop.
Sehemu ambazo sio za kushika laptop mara nyingi huwa zinateleza sana na kuwa ni laini, ni muhimu kushika laptop yako kwa mikono miwili na hakikisha unashika laptop yako ikiwa imefunikwa na siko ikiwa iko wazi kwani mara nyingi laptop nyingi huangushwa zikiwa zipo wazi au zime funguliwa na hayo yakiwa ni matokeo ya kushika laptop kwa mkono mmoja.
Kushindwa Kuchaji Laptop kwa Usahihi
Ni wazi kuwa kadri muda unavyokwenda ndipo battery za kifaa chochote cha kielektroniki inapo endelea kupungua nguvu, hii ni sawa kwa kifaa chochote kinacho tumia battery za kuchaji ikiwa pamoja na laptop. Lakini wakati mwingine mtumiaji huchangia kwa kiasi kikubwa kwa battery kupungua nguvu kwa haraka na kuharibika kwa haraka.
Ni muhimu kujua kuwa unatakiwa kuhakikisha laptop yako haitumiki chaji hadi mwisho na hakikisha unachaji laptop yako kabla ya kufika asilimia sifur. Hii ni muhimu sana kuweza kutunza ubora wa battery yako kwa muda mrefu. Kuacha hadi ifike asilimia sifuri mara moja moja sio mbaya lakini hakikisha hatua hii haiendelei mara kwa mara.
Na hayo ndio makosa makubwa ambayo yanaweza kuchangia laptop yako kuharibika kwa haraka. Kumbukua ni muhimu pia kuhakikisha laptop yako inapitia marekebisho ya mara kwa mara ya mfumo kama vile kuhakikisha programu zako zipo salama kwa kutumia programu za Antivirus na kutumia programu muhimu ambazo pia ni salama.
Kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua kuhusu sheria ya 20 20 20 ambayo ni muhimu sana kwa watumiaji wote wa kompyuta hasa kama unataka kutumia laptop ukiwa salama kwenye afya yako.