Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Laptop za Zamani Bora kwaajili ya Wafanyakazi wa Ofisini

Laptop hizi zinauwezo wa kufanya kazi zozote ngumu za maofisini
Laptop za Zamani Bora kwaajili ya Wafanyakazi wa Ofisini Laptop za Zamani Bora kwaajili ya Wafanyakazi wa Ofisini

Ni ukweli usio pingika kuwa bado kompyuta mpakato au laptop zinayo nafasi kubwa sana, pamoja na kuwepo kwa simu zenye uwezo mkubwa bado laptop ni muhimu sana hasa kwa wafanyakazi ambao hufanya kazi ofisi.

Kuliona hili leo nimekuandalia list ya laptop ambazo pengine zinafaa sana kwa matumizi ya ofisi,lakini pia kumbuka laptop hizi zinaweza pia kufaa hata kwa matumizi mengine ambayo pia sio ya ofisi. Laptop hizi zote tayari zinapatikana hapa Tanzania hivyo hutopata shida hata kidogo kupata laptop hizi. Basi moja kwa moja twende tukangalie list hii.

Advertisement

Apple Macbook Pro with Touch Bar

Laptop za Zamani Bora kwaajili ya Wafanyakazi wa Ofisini

Ni wazi kuwa Macbook Pro yenye Touch Bar ni laptop bora sana ya kununua kwaaji ya kufanya kazi za ofisini, kama wewe ni mmoja ya watu ambao wanafanya kazi za Ubunifu wa michoro mbalimbali ya majengo au kazi za Graphics Design basi hii ni laptop muhimu sana kuwa nayo. Bei ya Laptop Hii ni kuanzia Milioni Tsh 3,500,000 mpaka milioni Tsh 5,000,000.

Sifa za MacBook Pro Yenye Touch Bar

  • CPU: Quad-core Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel Iris Plus Graphics
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.3-inch, 16.0-inch (2,560 x 1,600) IPS
  • Storage: 256GB – 1TB PCIe 3.0 SSD

Apple MacBook Pro 13-inch (2020)

Laptop za Zamani Bora kwaajili ya Wafanyakazi wa Ofisini

Kama wewe ni mwanafunzi au mfanyakazi ambaye unafanya kazi zako kwa kusafiri kila mara basi  Apple MacBook Pro 13-inch (2020) ni laptop bora sana kwako, Mbali ya laptop hii kuwa na uwezo mkubwa sana pamoja na kuwa nyepesi kuibeba, vilevile laptop hii ina uwezo mkubwa sana wa kudumu na chaji hivyo inakupa uwezo wa kuendelea kufanya shuhuli zako za kila siku bila kuwa na wasiwasi wa kuisha chaji kwa haraka. Bei ya laptop hii inaanzia Tsh 3,000,000 hadi Tsh 5,500,000

Sifa za Apple MacBook Pro 13-inch (2020)

  • CPU: Quad-core Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel® Iris Plus Graphics
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.0-inch, (2560 x 1600) IPS 16:10
  • Storage: 256GB – 1TB SSD

Acer Switch 5

Laptop za Zamani Bora kwaajili ya Wafanyakazi wa Ofisini

Kama wewe ni mpenzi wa laptop zenye uwezo wa touchscreen basi ni vyema ufahamu laptop hii, Laptop hii ni moja kati ya laptop yenye nguvu zaidi na kizuri zaidi ni kuwa laptop hii inapatikana kwa bei rahisi. Bei ya Laptop hii inaanzia Tsh 1,000,000 hadi Tsh 2,500,000.

Sifa za Acer Switch 5

  • CPU: Quad-core Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel® UHD Graphics –  Intel® Iris Plus Graphics
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 14-inch, 1920 x 1080 IPS LCD touchscreen
  • Storage: 128GB – 512GB SSD

Dell XPS 13

Laptop za Zamani Bora kwaajili ya Wafanyakazi wa Ofisini

Hii ni moja kati ya laptop bora sana, Kama wewe ni Mfanyakazi wa ofisi au mfanyakazi wa maswala ya ubunifu au mtengenezaji wa Video laptop hii inauwezo wa kukuhudumia Vizuri, Laptop hii ni moja kati ya laptop zenye nguvu na zinazo sifika kuwa laptop bora sana. Kama ukituuliza Tanzania Tech ni laptop gani nzuri inayo tumia Windows ambayo unaweza kununua ambayo itakusaidia hata kwa miaka ya mbeleni, basi Dell XPS 13 ni moja ya Laptop hizo ambazo tungekushauri kununua. Bei ya Laptop Hii ina anzia Tsh 5,000,000 hadi Tsh 6,000,000.

Sifa za Dell XPS 13

  • CPU: 8th generation Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel UHD Graphics 620
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) – 4k (3840 x 2160)
  • Storage: 256GB – 1TB SSD

Lenovo Yoga 920

Japo kuwa hii ni laptop ya siku nyingi kidogo, lakini hii pia ni moja kati ya laptop zenye uwezo mkubwa sana. Laptop hii inakuja na uwezo wa kuzunguka nyuzi 360 na kukupa uwezo wa kufanya laptop hiyo kuwa tablet. Kama wewe ni mwanafunzi au mfanyakazi wa ofisini laptop hii itakufaa sana. Bei ya laptop hii inaanzia Tsh 4,500,000 hadi Tsh 3,500,000.

Sifa za Lenovo Yoga 920

  • CPU: Intel Core i7
  • Graphics: Intel UHD Graphics 620
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.9-inch 1920 x 1080 – 13.9-inch 3840 x 2160
  • Storage: 256GB – 1TB SSD
  • Connectivity: 802.11ac Wi-Fi; Bluetooth 4.1
  • Camera: 720p front-facing

Dell XPS 15 (2020)

Sasa hapa naomba niwe wazi, Laptop hii ni moja kati ya laptop ninayo ipenda sana kwani ni moja kati ya laptop ambayo hadi sasa natumia toleo la mwaka 2017, hivyo basi inawezekana mapenzi yangu ni moja kati ya sababu ya laptop hii kuwepo hapa lakini pia ni sababu ya kukwambia kuhusu laptop hii. Pamoja na hayo nikisema laptop bora basi hii ni moja kati ya laptop bora sana na yenye uwezo mzuri sana. Laptop hii ipo kwenye list ya laptop bora kutoka Dell Mpaka Sasa. Bei ya Laptop Hii ina anzia Tsh 2,500,000 hadi Tsh 5,500,000.

Sifa za Dell XPS 15 (2020)

  • CPU: Intel Core i5 – i7
  • Graphics: NVIDIA® GeForce GTX 1650
  • RAM: 8GB – 64GB
  • Screen: Up to 15.6-inch Ultra 4K (3840 x 2160) InfinityEdge Touch screen
  • Storage: 512GB – 2TB

Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch)

Kama wewe ni mmoja ya watu ambao wanapenda laptop inayoweza kubadilika na kuwa Tablet basi laptop hii ya Microsoft Surface Book 2 (yenye inch 13.5) ni chaguo zuri sana kwako. Mbali na uwezo wa laptop hii kuwa Tablet, laptop hii inauwezo mkubwa sana na ni nzuri sana kwa wafanyakazi wa ofisini pamoja na wanafunzi. Bei ya Laptop hii inaanzia Tsh Milioni 2,500,000 mpaka Tsh Milioni 3,500,000.

Sifa za Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch)

  • CPU: Intel Core i5-7300U – Intel Core i7-8650U 1.9GHz
  • Graphics: Intel UHD Graphics 620; Nvidia GeForce GTX 1050 (2GB GDDR5 VRAM)
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 3,000 x 2,000 (267 ppi) PixelSense display, 3:2 aspect ratio
  • Storage: 256GB – 1TB SSD

Na hizo ndio laptop bora sana ambazo unaweza kuzitumia ofisini, kumbuka kuwa laptop hizi zinaweza kutumika mbali na ofisini lakini naposema ofisini nina maana sehemu yoyote ya ndani ambapo laptop inaweza kutumia. Laptop hizi zinaweza kufanya kazi ngumu zenye uwezo mkubwa.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu laptop nyingine nzuri, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia tembelea tovuti yetu ya Price in Tanzania kwaajili ya kupata sifa pamoja na bei ya laptop mpya pamoja na simu zina zotoka kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use