Linapokuja swala zima la laptop bora ukweli ni kwamba kila mtu anajua kile kilicho bora kwake kutokana na matumizi ya laptop au kompyuta hiyo, sababu hiyo ndio haswaa iliyo sababisha leo Tanzania tech kukuletea list ya laptop bora kwaajili ya game kwa mwaka huu wa 2017.
Asus ROG Strix GL502
Asus ROG Strix GL502 ni moja kati ya laptop ambayo ni bora sana tena sana kwako wewe mpenzi game kwani sifa pamoja na graphics za laptop hii hakika zina uwezo wa kuimili game yoyote ya kwenye kompyuta.
Sifa za Asus ROG Strix GL502
- CPU: Intel Core i7
- Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060 – 1070
- RAM: 16GB DDR4
- Screen: 15.6-inch full HD 1,920 x 1,080 IPS
- Storage: 128GB – 256GB SSD, 1TB HDD
Alienware 13 R3
Kuna laptop chache sana za game zenye uwezo wa Alienware 13 R3, laptop hii inauwezo mkubwa pamoja na kioo chenye teknolojia bora ya OLED. Hivyo kama unaitaji kompyuta bora ya kucheza game basi laptop hii ni bora sana kwako.
Sifa za Alienware 13 R3
- CPU: Intel Core i5 – i7
- Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060
- RAM: 8GB – 16GB DDR4
- Screen: 13.3-inch HD 1,366 x 768 TN – QHD 2,560 x 1440 OLED touchscreen
- Storage: 180GB – 512GB SSD
HP Omen 17
Laptop hii ni moja kati ya laptop bora na nzuri sana pia kama wewe ni mpenzi wa laptop zenye uzito kiasi HP Omen 17 ni laptop bora kwako, vile vile kizuri zaidi kuhusu laptop hii ni kioo chake kwani kinauwezo wa 1440p hii ni sawa na kusema laptop hii ina teknolojia ya 4K.
Sifa za HP Omen 17
- CPU: 6th gen Intel Core i7
- Graphics: Nvidia GeForce GTX 1070 (8GB GDDR5);
- Intel HD Graphics 530
- RAM: 16GB DDR4
- Screen: 17.3-inch 4K (3,840 x 2,160) IPS with G-Sync
- Storage: 1TB – 2TB HDD, 128GB SSD
Gigabyte Aero 14
Laptop hii ni moja kati ya laptop ambazo ni bora sana hasa kama unapenda laptop ambazo ni ndogo na zenye nguvu kubwa. Pia laptop hii ya Gigabyte Aero 14 ni moja kati ya laptop zenye bai nafuu sana kwenye masoko mbalimbali ya mitandaoni, ukilinganisha na laptop nyingine kwenye list hii.
Sifa za Gigabyte Aero 14
- CPU: Intel Core i7
- Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060 (6GB GDDR5)
- RAM: 16GB – 32GB
- Screen: 14-inch, QHD 2,560 x 1,440 anti-glare IPS
- Storage: 512GB – 1TB SSD
Razer Blade
Kwa wacheza game wengi laptop hii ni bora sana kwani inauwezo bora sana pamoja na kuchangiwa na uwezo wake wa kudumu na battery kwa masaa 3 na dakika 35 ukiwa unacheza game na masaa 6 kama una angalia video bila kupumzika. Kwa hakika Razer Blade ni moja kati ya laptop bora sana za game kwa mwaka huu 2017.
Sifa za Razer Blade
- CPU: 2.6GHz Intel Core i7-6700HQ
- Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060 (6GB GDDR5 VRAM)
- RAM: 16GB
- Screen: 14-inch FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3,200 x 1,800) IGZO (LED backlit, multi-touch)
- Storage: 256GB – 1TB PCIe SSD
Aorus X5 v6
Unaweza ukawa huijui sana laptop Aorus X5 v6 lakini hii ni moja kati ya laprop bora sana za game kwa mwaka huu, unaweza kutuia kompyuta hii kucheza game za aina yoyote ile ziwe zenye teknolojia ya HD.
Sifa za Aorus X5 v6
- CPU: Intel Core i7
- Graphics: Nvidia GeForce GTX 1070 (8GB GDDR5)
- RAM: 8GB – 16GB
- Screen: 15.6-inch, FHD 1,920 x 1,080 – WQHD+ 2,880 x 1,620 IPS
- Storage: 1TB HDD; 256GB SSD
Razer Blade Pro
Kama unatafuta laptop bora ya kucheza game yenye kioo cha inch 17 pamoja na teknolojia ya 4K basi Razer Blade Pro ni laptop bora sana kwako. Laptop hii ni moja kati ya laptop zilizongelewa sana kwa mwaka 2016 lakini pia mwaka huu bado laptop hii ni laptop bora sana kwa wapenda game kote duniani.
Sifa za Razer Blade Pro
- CPU: Intel Core i7
- Graphics: Nvidia GeForce GTX 1080 (8GB GDDR5)
- RAM: 32GB
- Screen: 17.3-inch, UHD (3,840 x 2,160) IGZO touchscreen with G-Sync
- Storage: 512GB – 2TB PCIe SSD
Origin EON17-X
Hii ni laptop nyingine ambayo kwa hakika ni moja kati ya laptop bora sana za kucheza game kwa sasa, laptop hii ina kioo chenye teknolojia ya 4K hivyo jiandae kucheza game zenye muonekano angavu pale unapokua na Laptop hii ya Origin EON17-X.
Sifa za Origin EON17-X
- CPU: Intel Core i5 – i7
- Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060 – 1080
- RAM: 8GB – 64GB
- Screen: 17.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – QFHD (3,840 x 2,160) Matte Display with G-Sync
- Storage: 120GB – 2TB SSD, 500GB – 2TB HDD, 1TB – 2TB SSHD
Acer Predator 17 X
Namba 9 kwenye list hii ni Acer Predator 17 X, laptop hii ni moja kati ya laptop za kisasa kabisa zenye uwezo wa kucheza game zenye kuitaji graphics card ya aina yoyote. Laptop hii ina tumia feni zenye teknolojia ya kisasa ili kufanya laptop yako kukaa kwa muda mrefu ikiwa imepoa. Hivyo laptop hii ni moja kati ya laptob bora ukizingatia laptop hii ni maalum kwa kucheza game.
Sifa za Acer Predator 17 X
- CPU: Intel Core i7
- Graphics: Nvidia GeForce GTX 980
- RAM: 32GB DDR4
- Storage: 1TB HDD, 512GB SSD
Origin EON17-SLX
Laptop ya mwisho ya kweli list hii ni Origin EON17-SLX laptop hii ni moja kati ya laptop za kisasa na zenye uwezo mkubwa hasa pale linapokuja swala zima la game. Laptop hii yenye inch 17 ni moja kati ya laptop ya yenye uwezo mkubwa sana.
Sifa za Origin EON17-SLX
- CPU: Intel Core i5 – i7 |
- Graphics: NVIDIA GeForce GTX 1070 – 1080 |
- RAM: 8GB – 64GB |
- Screen: 17.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – UHD (3840 x 2160) IPS Matte Display with G-SYNC
- Storage: 120GB – 4TB SSD, 500GB – 1TB HDD, 1TB SSHD
Na hizo ndio laptop bora kwaajili ya wapenda game wote kwa mwaka huu 2017, kama una maoni ushauri au hata kama unadhani kuna laptop tumeisahau tuandikie hapo chini ili tuweze kuiongeza kwenye list hii.
Kwa Habari zaidi za teknolojia kwa lugha ya kiswahili unaweza download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store na tutakupa habari zote pindi zitakapo toka. Zaidi pia kama unataka kujifunza na kupata habari za teknolojia kwa njia ya video unaweza kujiunga nasi kupitia Channel yetu ya Youtube ya Tanzania Tech.
Source : Tech Radar
Bei ya hzo laptop ni shngapi
je dell e6400 sio nzuri kwa games kubwa