Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Laptop za Zamani Bora Kununua kwa Sasa

Soma hapa kuweza kujua makadirio ya Bei za laptop hizi
Laptop 10 bora na bei zake mwaka 2018 Laptop 10 bora na bei zake mwaka 2018

Ni mda mrefu sana umepita toka tuongele kuhusu laptop, pengine hii ni kutokana na uwepo wa laptop mpya chache sana kwenye miaka ya karibuni au ni kwa sababu simu zimekuwa zikishika chati zaidi kwa sasa pengine kuliko laptop, Lakini kama ulikua mmoja wa watu ambao wanatamani kujua kuhusu laptop bora za bei nafuu kwa mwaka huu (2021) basi hii hapa ndio list ya laptop bora ambazo unaweza kununua kwa sasa.

Kumbuka laptop hizi nyingi zinapatikana hapa Tanzania hivyo tutajitahidi kuweka na bei za laptop hizi ili uweze kujua angalau kwa makadirio ni kiasi gani cha fedha unachotakiwa kuwa nacho ili uweze kupata aina flani ya laptop. Basi bila kupoteza muda twende tuka angalie list hii, Kumbuka list hii haijapangwa kwa namba hivyo laptop zote hapa ni bora sana kuwa nazo.

Advertisement

Apple Macbook Pro with Touch Bar

Ni wazi kuwa Macbook Pro yenye Touch Bar ni laptop bora sana ya kununua kwa sasa, kama wewe ni mmoja ya watu ambao wanafanya kazi za Ubunifu wa michoro mbalimbali (Graphics Design) basi hii ni laptop muhimu na nzuri sana kwako. Bei ya Laptop Hii ni kuanzia Milioni Tsh 2,000,000 mpaka milioni Tsh 2,500,000.

Sifa za MacBook Pro Yenye Touch Bar

  • CPU: Dual-core Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel Iris Plus Graphics 640 – 650
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.3-inch, (2,560 x 1,600) IPS
  • Storage: 256GB – 1TB PCIe 3.0 SSD

Mazuri Kuhusu Laptop Hii

  • Hii ndio Laptop bora kwa sasa kutoka Apple
  • Processory ya Laptop hii inafanya kazi Haraka

Mabaya Kuhusu Laptop Hii

  • Chaji yake Haidumu Sana
  • Ni Bei Ghali Sana

Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch)

Kama wewe ni mmoja ya watu ambao wanapenda laptop inayoweza kubadilika na kuwa Tablet basi laptop hii ya Microsoft Surface Book 2 (yenye inch 13.5) ni chaguo zuri sana kwako. Mbali na uwezo wa laptop hii kuwa Tablet, laptop hii inauwezo mkubwa sana na ni nzuri sana kwa wafanyakazi wa maofisini pamoja na wanafunzi. Bei ya Laptop hii inaanzia Tsh Milioni 2,000,000 mpaka Tsh Milioni 2,500,000.

Sifa za Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch)

  • CPU: Intel Core i5-7300U – Intel Core i7-8650U 1.9GHz
  • Graphics: Intel UHD Graphics 620; Nvidia GeForce GTX 1050 (2GB GDDR5 VRAM)
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 3,000 x 2,000 (267 ppi) PixelSense display, 3:2 aspect ratio
  • Storage: 256GB – 1TB SSD

Kizuri Kuhusu Laptop Hii

  • Battery Yake Inadumu na Chaji
  • Laptop Hii ina nguvu Sana

Kibaya Kuhusu Laptop Hii

  • Bei Ghali
  • Haiji na Kalamu

Acer Switch 3

Kama wewe ni mpenzi wa laptop zenye uwezo wa kubadilika na kuwa Tablet basi ni vyema ufahamu laptop hii, Laptop hii ni moja kati ya laptop yenye nguvu zaidi na kizuri zaidi ni kuwa laptop hii inapatikana kwa bei rahisi. Bei ya Laptop hii inaanzia Tsh 800,000 hadi Tsh 1,000,000.

Sifa za Acer Switch 3

  • CPU: 1.10GHz Intel Quad Core N4200 – Intel Core i3 7100U
  • Graphics: Intel HD Graphics 505
  • RAM: 4GB
  • Screen: 12.2-inch, 1920 x 1200 IPS LCD touchscreen
  • Storage: 64GB – 128GB eMMC

Kizuri Kuhusu Laptop Hii

  • Kwa Sura ni Nzuri Sanaa
  • Bei Yake ni Rahisi

Kibaya Kuhusu Laptop Hii

  • Sio Nzuri kwa Game

Apple MacBook 12-inch (2017)

Kama wewe ni mwanafunzi au mfanyakazi ambaye unafanya kazi zako kwa kusafiri kila mara basi  Apple MacBook 12-inch (2017) ni laptop bora sana kwako, Mbali ya laptop hii kuwa na uwezo mkubwa sana pamoja na kuwa nyepesi kuibeba, vilevile laptop hii ina uwezo mkubwa sana wa kudumu na chaji hivyo inakupa uwezo wa kuendelea kufanya shuhuli zako za kila siku bila kuwa na wasi wasi wa kuisha chaji kwa haraka. Bei ya laptop hii inaanzia Tsh 1,800,000 hadi Tsh 2,000,000

Sifa za Apple MacBook 12-inch (2017)

  • CPU: Intel Core M3 1.2GHz – Intel Core i7 1.4GHz
  • Graphics: Intel HD Graphics 615
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 12-inch, (2,304 x 1,440) IPS 16:10
  • Storage: 256GB – 512GB SSD

Kizuri Kuhusu Laptop Hii

  • Processor Yenye Nguvu Zaidi
  • Battery Inadumu na Chaji Zaidi

Kibaya Kuhusu Laptop Hii

  • Inayo Sehemu Moja ya USB-C port
  • Ni Bei Ghali

Lenovo Yoga 920

Laptop hii pia ni moja kati ya laptop zenye uwezo wa kubadilika na kuwa tablet, lakini utofauti wa laptop hii ni kuwa, Laptop hii haitoki kama zilivyo laptop nyingine kwenye list hii, Laptop hii yenyewe inazunguka nyuzi 360 na kukupa uwezo wa kufanya laptop hiyo kuwa tablet. Kama wewe ni mwanafunzi au mfanyakazi wa ofisini laptop hii itakufaa sana. Bei ya laptop hii inaanzia Tsh 3,000,000 hadi Tsh 3,500,000.

Sifa za Lenovo Yoga 920

  • CPU: Intel Core i7-855OU
  • Graphics: Intel UHD Graphics 620
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.9-inch 1920 x 1080 – 13.9-inch 3840 x 2160
  • Storage: 256GB – 1TB SSD
  • Connectivity: 802.11ac Wi-Fi; Bluetooth 4.1
  • Camera: 720p front-facing

Kizuri Kuhusu Laptop Hii

  • Inayo nguvu Sana ya Processor
  • Ni nyembamba

Kibaya Kuhusu Laptop Hii

  • Bei Ghali
  • Haina Uwezo Mzuri wa Graphics
  • Feni za Laptop Hii Zinatabia ya Kutoa Sauti

Asus Transformer Mini T102HA

Kama wewe unatafuta laptop ya bei rahisi yenye uwezo wa kawaida basi laptop hii ni bora sana kwako, Laptop hii ni nzuri sana kwa kufanya kazi ndogo ndogo za kila siku huku ikikupa uwezo wa kufungua kurasa mbalimbali za tovuti pamoja na kazi zingine za kawaida. Bei ya Laptop Hii ina anzia Tsh 800,000 mpaka Tsh 1,300,000.

Sifa za Asus Transformer Mini T102HA

  • CPU: Intel Atom x5-Z8350
  • Graphics: Intel HD Graphics – Intel HD Graphics 400
  • RAM: 2GB – 4GB
  • Screen: 11.6-inch 1,366 x 768 HD IPS touchscreen
  • Storage: 32GB

Kizuri Kuhusu Laptop Hii

  • Laptop Hii ni Ndogo kwa Umbo na Nyepesi
  • Inayo Uwezo Mkubwa wa Kudumu na Chaji

Kibaya Kuhusu Laptop Hii

  • Haina Uwezo Mkubwa Sana

Asus Zenbook UX310UA

Kama wewe ni mtu unae hitajika kufanya kazi kwa haraka kama vile mwandishi wa habari au watu walioko kwenye kazi kama hizo, basi laptop hii ni bora sana kuwa nayo. Laptop hii inasifika sana kwa tabia yake ya kuweza kuwaka kwa haraka na uwezo wake mzuri wa Processor. Bei ya Laptop Hii ina anzia Tsh 1,700,000 hadi Tsh 2,000,000.

Sifa za Asus Zenbook UX310UA

  • CPU: Intel Core i3 – i5
  • Graphics: Intel HD Graphics 620
  • RAM: 8GB
  • Screen: 13.3-inch up to QHD+ (3,200 x 1,800)
  • Storage: 256GB SSD

Kizuri Kuhusu Laptop Hii

  • Inauwezo wa Kuwaka na Kutumika Haraka

Kibaya Kuhusu Laptop Hii

  • Battery Yake Haina Uwezo wa Kudumu Sana

Dell XPS 13

Hii ni moja kati ya laptop bora sana, Kama wewe ni Mfanyakazi wa ofisi au mfanyakazi wa maswala ya ubunifu au mtengenezaji wa Video laptop hii inauwezo wa kukuhudumia Vizuri, Laptop hii ni moja kati ya laptop zenye nguvu na zinazo sifika kuwa laptop bora sana. Kama ukituuliza Tanzania Tech ni laptop gani nzuri inayo tumia Windows ambayo unaweza kununua ambayo itakusaidia hata kwa miaka ya mbeleni, basi Dell XPS 13 ni moja ya Laptop hizo ambazo tungekushauri kununua. Bei ya Laptop Hii ina anzia Tsh 2,000,000 hadi Tsh 3,000,000.

Sifa za Dell XPS 13

  • CPU: 8th generation Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel UHD Graphics 620
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) – 4k (3840 x 2160)
  • Storage: 256GB – 1TB SSD

Kizuri Kuhsu Laptop Hii

  • Inayo Uwezo wa 4K
  • Uwezo Mzuri wa Gharphics (Japo Sio Sana)

Kibaya Kuhusu Laptop Hii

  • Bei Ghali Sana

Lenovo Yoga Book

Kama wewe unatafuta laptop ya bei nafuu na yenye uwezo wa tofauti kidogo basi Laptop Hii ni moja kati ya laptop zitakazo kufaa sana. Laptop hii inauwezo mzuri sana wa kioo pamoja na uwezo wake wa kubebeka kirahisi kutokana na uzito wake mdogo. Bei ya Laptop Hii Inaanzia Tsh 600,000 hadi Tsh 1,000,000.

Sifa za Lenovo Yoga Book

  • CPU: Intel Atom x5-Z8550
  • Graphics: Intel Atom
  • RAM: 4GB
  • Screen: 10.1-inch full HD IPS touchscreen
  • Storage: 64GB SSD, up to 128GB microSD

Kizuri Kuhusu Laptop Hii

  • Laptop Hii ni Nyepesi na Nyembamba
  • Kioo Kizuri
  • Bei Rahisi

Kibaya Kuhusu Laptop Hii

  • Inatumia Processor Yenye Uwezo Mdogo

Dell XPS 15

Sasa hapa naomba niwe wazi, Laptop hii ni moja kati ya laptop ninayo ipenda sana na kuitamani sana kuwa nayo, hivyo basi inawezekana mapenzi yangu ni moja kati ya sababu ya laptop hii kuwepo hapa. Pamoja na hayo nikisema laptop bora basi hii ni moja kati ya laptop bora sana na yenye uwezo mzuri sana. Kwa mujibu wa tovuti ya Techradar Hii ndio laptop bora kutoka Dell Mpaka Sasa. Bei ya Laptop Hii ina anzia Tsh 2,000,000 hadi Tsh 3,000,000.

Sifa za Dell XPS 15

  • CPU: Intel Core i5-7300HQ – i7-7700HQ
  • Graphics: NVIDIA® GeForce GTX 1050 with 4GB GDDR5
  • RAM: 8GB – 16GB DDR4
  • Screen: Up to 15.6-inch Ultra HD (3840 x 2160) InfinityEdge touchscreen
  • Storage: 1TB HDD – 512GB SSD

Kizuri Kuhusu Laptop Hii

  • Inadumu na Chaji
  • Kioo Bora
  • Uwezo Mzuri wa Processor

Kibaya Kuhusu Laptop Hii

  • Kamera Yake (Web Cam) Imekaa Mahali Pabaya

Na hiyo ndio list ya Laptop bora ambazo unaweza kununua kwa sasa na vilevile hizi ndio laptop bora mpaka sasa mwaka huu 2020 – 2021. Kama ulikuwa unatafuta laptop Bora kwaajili ya Wanafunzi unaweza kusoma list nyingine ya laptop bora kwaajili ya Mwanafunzi Hapa.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use