Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Laptop 10 Bora Kununua Mpaka Sasa Mwezi May Mwaka 2017

Kama unataka kununua laptop mwezi huu basi hizi ndio laptop 10 bora
laptop kumi 10 bora laptop kumi 10 bora

Linapokuja swala zima la kununua laptop wengi wetu tumekuwa tumekuwa tukitafuta ushauri mbalimbali kutoka kwa watu au hata tovuti mbalimbali ili kujua laptop ambayo ingekufaa kuwa nayo kwa kipindi kirefu, kama wewe ni mmoja wa watu ambao bado wanatafuta ushauri basi umefika mahali sahihi kwani leo tutaenda kuangalia laptop 10 bora za kununua mwezi huu may mwaka 2017.

  • Dell XPS 13

Sifa za Dell XPS 13

Advertisement

  • CPU: Intel Core i3 – i7
  • Graphics: Intel HD Graphics 620
  • RAM: 4GB – 16GB
  • Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3,200 x 1,800)
  • Storage: 128GB – 512GB SSD

Laptop hii ni bora sana kuwa nayo na imekuwa kwenye chat kwa muda mrefu na inaongoza kwa kudumu na chaji kwa muda mrefu sana, kiukweli kama unatafuta laptop ngumu na ya kudumu Dell XPS 13 ni chaguo bora sana.

  • Asus ZenBook UX305

Sifa za Asus ZenBook UX305

  • CPU: Intel Core Intel Core m3 – m7 |
  • Graphics: Intel HD Graphics 515 |
  • RAM: 8GB |
  • Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3200 x 1800) IPS display |
  • Storage: 256GB – 512GB SSD

Kwa mujibu wa tovuti ya techradar laptop hii ni bora kuliko hata Macbook na laptop hii imekua ni bora zaidi hasa kwa upande wa bei, chaji na uwezo wa laptop hii bado ni mkubwa sana na unakupa uwezo wa hali ya juu sana.

  • Razer Blade Stealth

Sifa za Razer Blade Stealth

  • CPU: Intel Core i7
  • Graphics: Intel HD Graphics 620
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 12.5-inch, QHD+ (2,560 x 1,440) – 4K (3,840 x 2,160) IGZO LED-backlit multi-touch
  • Storage: 128GB – 1TB SSD

Kama unatafuta laptop bora yenye uwezo wa kucheza game vizuri pamoja na uwezo wa kufanya kazi zako za kila siku basi Razer Blade Stealth ni laptop bora sana kwako.

  • Asus Chromebook Flip

Sifa za Asus Chromebook Flip

  • CPU: Intel Pentium – Core m3
  • Graphics: Intel HD Graphics 515
  • RAM: 4GB
  • Screen: 12.5-inch, FHD (1,920 x 1,080) LED backlit anti-glare
  • Storage: 32GB – 64GB eMMC

Kama unataka laptop yenye uwezo wa kuinstall app kama vile kwenye simu yako ya Android basi hii ni laptop bora sana kwako, laptop hii ni moja kati ya laptop zenye chrome OS na ambazo zinasifika sana kwa sasa, hivyo kama unataka laptop simple na ya kisasa Asus Chromebook Flip ni laptop bora sana kununua kwa sasa.

  • HP Spectre x360

Sifa za HP Spectre x360

  • CPU: Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel HD Graphics 620
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.3-inch FHD 1,920 x 1,080 – UHD 3,840 x 2,160 IPS multi-touch
  • Storage: 256GB – 1TB SSD

Kama unatafuta laptop bora yenye uwezo wa kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja basi HP Spectre x360 ni laptop bora sana, laptop hii inauwezo wa kuwa tablet na uwezo wa kuwa laptop vyote kwa pamoja uku ikiwezeshwa na processor bora zenye nguvu pamoja na battery yenye nguvu ya kudumu hadi masaa 24 ikiwa inatumika mfululizo.

  • Razer Blade

Sifa za Razer Blade

  • CPU: Intel Core i7
  • Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060
  • RAM: 16GB
  • Screen: 12.5-inch, FHD (1,920 x 1,080) matte – UHD (3,840 x 2,160) IGZO
  • Storage: 256GB – 1TB SSD

Kama wewe unafanya maswala ya Graphics au animation laptop hii ni bora sana kwako kwani laptop hii inauwezo mkubwa sana kwenye upande wa grahics pamoja na uwezo wake wa kudumu na chaji. Kama unataka laptop kwaajili ya kazi za Graphics basi Razer Blade ni laptop bora sana kwako.

  • Samsung Notebook 7 Spin

Sifa za Samsung Notebook 7 Spin

  • CPU: 2.5GHz Intel Core i7-6500U
  • Graphics: Nvidia GeForce 940MX (2GB DDR3L); Intel HD Graphics 520
  • RAM: 12GB – 16GB
  • Screen: 15.6-inch Full HD (1,920 x 1,080) LED with touch panel
  • Storage: 1 TB HDD – 1TB HDD; 128GB SSD

Kama unataka latop bora yenye sifa bora na yenye uwezo mkubwa lakini yenye bei ndogo basi laptop hii ya Samsung Notebook 7 Spin ni laptop bora sana kwako, laptop hii inauwezo mkubwa sana na inaweza kufanya karibia kazi zote hivyo kama unataka laptop ya kudumu nayo na yenye uhakika basi Samsung Notebook 7 Spin ni laptop bora sana kwako.

  • Acer Aspire S 13

Sifa za Acer Aspire S 13

  • CPU: Intel Core i3 – i7
  • Graphics: Intel HD Graphics 520 – 620
  • RAM: 4GB – 8GB
  • Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) anti-glare touchscreen IPS
  • Storage: 128GB – 512GB SSD

Kama unataka kupata laptop yenye nguvu zaidi ya MacBook Air basi laptop hii ni bora sana kwako na inakupa uwezo wa hali ya juu pamoja na uwezo wa hali ya juu vyote vikiwa vinaendeshwa na processor kubwa kuliko hata umbo la laptop hii.

  • Samsung Notebook 9

Sifa za Samsung Notebook 9

  • CPU: 2.3GHz Intel Core i5-6200U
  • Graphics: Intel HD Graphics 520
  • RAM: 8GB
  • Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) LED anti-reflective display
  • Storage: 256GB

Kutokana na bei yake unaweza kushtuka kidogo lakini naamini mtu yoyote anaetraka kitu kizuri hato ona aja ya kuogopa baei ya laptop hii bora yenye nguvu na uwezo wa kudumu na chaji kwa masaa mengi pengine kuliko laptop nyingine kwenye list hii, hivyo kama unataka laptop yenye uwezo wa juu na kudumu na chaji basi Samsung Notebook 9 ni laptop bora sana kwako.

  • Surface Book

Sifa za Surface Book

  • CPU: Intel Core i5 – i7
  • Graphics: Intel HD graphics 520 – Nvidia GeForce graphics
  • RAM: 8GB – 16GB
  • Screen: 13.5-inch, 3,000 x 2,000 PixelSense Display
  • Storage: 128GB – 256GB PCIe3.0 SSD

Kama unatafuta laptop bora ya windows yenye kukupa uwezo wa kutumia programu zote kwa umakini na ufani wa hali ya juu basi laptop hii ni bora sana kwako. Nunua laptop hii mana inakupa uwezo bora wa kisasa kabisa.

Basi hizo ndio laptop ambazo kwa sasa zinaweza kufanya kazi zako kuwa rahisi na pengine kudumu kwa muda mrefu kutokana na utunzaji wako. Kumbuka list hii inaweza kubadilika muda wowote maana laptop zinatoka kila mwezi na pia bado tunasubiri Macbook ya mwaka 2017 hivyo usikae mbali na Tanzania Tech.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video. 

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use