Kampuni maarufu kwa utengenezaji wa magari ya kutoka British, hivi karibuni imevunja mipaka na kuja na simu yake ya kwanza iliyopewa jina la Land Rover Explore, simu hii ambayo imezinduliwa leo kwenye mkutano wa MWC 2018, inakuja ikiwa na sifa za simu ngumu na yenye kuweza kudumu kwenye hali yoyote.
Simu hii ambayo ni maalum kwa wasafiri pamoja na watalii inakuja ikiwa na uwezo mkubwa sana wa kupitia vikwanzo mbalimbali ambavyo ni ngumu sana kwa simu ya kawaida kuweza kupitia, Simu hii imejaribiwa kwa kila namna ikiwa pamoja na kuangushwa kwa umbali mrefu kiasi cha mita 1.8 na simu hii iliweza kupona.
Vilevile simu hii inauwezo wa kudumu na chaji karibia siku tatu kutona na battery yake yenye nguvu ya 4,370mAh hii ikiwa unaweza kuongezea battery nyingine kwa nyuma yenye uwezo wa 3,600mAh ambayo kwa ujumla inaweza kufanya simu yako kudumu na chaji zaidi ya wiki moja inategemea na matumizi yako.
Vilevile unaweza kuongeza vitu kama Antena ya GPS pamoja na kifaa cha kuongeza mawasiliano ya Network hii ikiwezesha simu hii kutumika hata sehemu zisizo na network kubwa. Mbali na hayo simu hii inakuja na sifa zifuatazo –
Sifa za Land Rover Explore
- Mfumo wa Uendeshaji – Android Nougat, inayo tegemewa kuwekewa toleo la Android Oreo
- Uwezo wa RAM – GB 4
- Ukubwa wa Ndani – GB 64 yenye uwezo wa kuongezwa kwa kutumia MicroSD
- Uwezo wa Processor – Deca-core 2.6GHz 64 bit MTK Helio X27 chipset
- Uwezo wa Kamera – Kamera ya nyuma ina Megapixel 16, Kamera ya mbele ina Megapixel 8, yenye uwezo wa 4x digital zoom
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5, chenye teknolojia ya FHD display, Corning Gorilla Glass 5 protected, chenye uwezo wa kuhimili hali ngumu.
- Uwezo wa Battery – Battery kubwa yenye uwezo wa (4000mAh) pamoja na uwezo wa kuongezea battery nyingine kwa juu.
- Uwezo wa Network – LTE Cat 6
- Mengineyo – Inatumia line mbili au Dual SIM, Inauwezo wa kuzuia maji na vumbi IP68 splash, water and dust resistance
Simu hii inategemewa kuuzwa kwa dollar za marekani $799 ambayo ni sawa na shilingi ya Tanzania 1,800,906.05 (hii ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo) kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania. Land Rover Explore inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia mwezi wa nne mwaka huu 2018.