Bado teknolojia inaendelea kukua kila siku, Kudhihirisha hilo wataalamu kutoka Amsterdam, huko nchini Netherlands wamefanya ugunduzi wa shati la kwanza lenye material ya pamba ambalo halichafuki wala halishiki kabisa madoa.
Labfresh ndio jina la shati hilo ambalo limetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ambayo inasaidia shati hilo kuzuia kushika madoa, bacteria pamoja na uchafu wowote naotokana na mafuta, rangi na vitu vingine kama hivyo.
Shati hilo ambalo hali itaji kupigwa pasi mara kwa mara , linategemewa kutoka hivi karibuni wakati sasa wataalamu hao wakiomba support kutoka kwa watu mbalimbali ili kukamilisha hatua za mwisho za kuanza kuuza shati hilo.
Unaweza kutoa support yako pamoja na kuangalia material yaliyotengeneza shati hilo kupitia ukurasa wa kampuni hiyo kwenye tovuti ya Kickstarter.