Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kumzuia Mtu Asitembele Tovuti Flani Kwenye Simu Yake

Njia hii inaweza kusaidia kumzuia mtoto kutembelea tovuti fulani kwenye simu au kompyuta
Jinsi ya Kumzuia Mtu Asitembele Tovuti Flani Kwenye Simu Yake Jinsi ya Kumzuia Mtu Asitembele Tovuti Flani Kwenye Simu Yake

Ukweli ni kwamba ulimwengu wa teknolojia unakuwa kwa kasi sana kwani sasa kila kitu kinapatikana mtandaoni kiwe kizuri au kibaya vyote unaweza kuvipata mtandaoni. Ndio maana wote tunaitaji ulinzi zaidi hasa kwa watoto na watu wengine ambao ungependa wajifunze mambo mazuri mtandaoni kupitia tovuti nzuri pekee.

Kuliona hili leo tumekuletea njia ambayo unaweza kuitumia kuweza kumzuia mtu asiweze kutumia tovuti au app fulani kwenye simu yake ya Android, Njia hii inafanya kazi vizuri kama unataka kumzuia mtoto au kama unataka kuongeza usalama kwenye simu yako hasa kama mahali ulipo watu wana tabia za kushika simu yako.

Advertisement

Kumbuka njia hii inaweza kufanya kazi kwenye simu na inaweza kufanya kazi kwenye kompyuta hivyo kama unatumia kompyuta na ungependa kufanya hatua hizi unaweza kusoma makala hii hadi mwisho kuweza kujua jinsi ya kufanya hivyo.

Kwa kuanza unatakiwa kudownload app inayoitwa BlockSite, app hii inapatikana Play Store na pia unaweza kuipata kwa kubofya hapo chini. Baada ya hapo hakikisha una install app hiyo kwenye simu ya mtu ambaye unataka kumzuia kutembelea tovuti fulani.

Baada ya kuinstall app hiyo, ruhusu permission zote kisha unatakiwa kuwezesha app hii kwenye sehemu ya Accessibility kwenye simu yako ya Android. Hakikisha unawasha sehemu hiyo kwani ndio inayofanya app hii kuweza kufanya kazi vizuri.

Baada ya kuwasha sehemu hiyo, utapelekwa kwenye uwanja ambapo sasa unatakiwa kuweka link ya website ambayo hutaki mtu kutembelea kwenye simu yake, bofya kitufe cha jumlisha kilichopo chini upande wa kulia andika link ya website kisha bofya alama ya tiki iliyopo juu upande wa kulia.

Jinsi ya Kumzuia Mtu Asitembele Tovuti Flani Kwenye Simu Yake

Baada ya hapo utakuwa umemaliza na unaweza kuweka password kama unataka au kama unataka tovuti hiyo kufungwa kwa muda flani pia unaweza kufanya hivyo kwa kubofya kitufe cha saa kilichopo juu upande wa kulia, kama inavyowezekana kwenye picha ya kwanza kushoto.

Pia unaweza kufungia app yoyote kwenye simu kwa kutumia sehemu ya App iliyopo upande wa kulia kwenye app ya Block site.

Mbali na hayo unaweza kufungia tovuti yoyote kwenye kompyuta kwa kutumia njia hii, unacho takiwa kufanya ni kuinstall Extension ya Block site kwenye kivinjari cha Google Chrome kisha fuata hatu akama hizo nilizo kuonyesha hapo juu. Unaweza kupakua extension hiyo kupitia link hapo chini.

Nadhani mpaka hapo utakuwa umeweza kuzuia baadhi ya tovuti kupitia simu ya Android pamoja na kompyuta. Kama kuna mahali popote umekwama usisite kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini, na kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku pia usisahau kutembelea channel yetu ili kujifunza kwa vitendo.

3 comments
  1. Maoni*yani apo inaleta utata sana yani kufanya hii app iwe complete mpaka ukaiweke kwenye simu ya mwingine pia
    hii imekaa vipi!

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use