Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Ndio Njia Mtu Anazotumia Ku-Hack Akaunti Yako Ya WhatsApp

Kama ulisha wahi kuwa Hacked kwenye akaunti yako ya WhatsApp, hizi ndio njia hackers wengi wanazotumia kufanya hivyo
Whatsapp Whatsapp

Inawezekana kuna wakati akaunti yako ya whatsapp inakuwa hacked lakini kutokana na kuwa haujui inakuwa ni ngumu sana kuweza kuondoa tatizo hilo hivyo leo Tanzania tech tunakuletea baadhi ya njia mbazo hackers hutumia ku-hack akaunti ya mtu yoyote, vilevile tumeonyesha na njia za kufanya ili kujikinga na kuwa hacked kwenye akaunti yako ya WhatsApp.

Basi moja kwa moja twende tukaangalie ni namna gani hawa hackers hufanya ili kupata uwezo wa kusoma meseji pamoja na picha zako, kwaajili ya usalama makala hii haita fundisha namna ya ku-hack bali namna ya kuzui na kujua kama akaunti yako iko hacked.

Advertisement

  • Kwa Kutumia Backup Files za WhatsApp

kwa-kutumia-backup-files-za-whatsapp

Hatua hii ni pale hacker anapotumia database file ambazo hupatikana kwenye folder la WhatsApp na mara nyingi file hizi huwa zimewekewa ulinzi maalumu yani (encrypted). Lakini cha kusikitisha ni kwamba ulinzi huu unaweza kuondolewa kwa kutumia programu maalum ambapo hacker anapofanikiwa kufanya hivyo anapata huwezo wa kusoma meseji zako zote ambazo umeshawahi kutuma siku za karibuni. File hizi hupatikana kwenye sehemu ya File location – (/sd card/WhatsApp/Databases/msgstore.db.crypt)

  • Kwa Kutumia Programu Mbalimbali za Ku-Backup WhatsApp

kwa-kutumia-programu-mbalimbali-za-ku-back

Kuna baadhi ya programu ambazo zinauwezo wa kufanya backup ya meseji zote zilizoko kwenye programu ya whatsapp programu hizi hufanya ku-backup na baadae ku-restore. Hata hivyo Whatsapp yenyewe inayo sehemu ambapo unauwezo wa kufanya backup na backup hizi hutumika na hackers pamoja na programu maalumu ya android ambayo huamisha backup hizo kwa mfumo wa .txt file moja kwa moja kwenda kwenye simu ya hacker na kwa kufanya hivyo kunampa yeye uwezo wa kusoma meseji zako zote ulizotuma mpaka siku hiyo.

  • Kwa Kutumia Meseji Maalum za OTP SMS

kwa-kutumia-meseji-maalum-za-otp-sms

Kwa wale wasiojua OTP SMS hizi ndio zile meseji ambazo huwa zinazotumiwa kufanya uhakiki wa akaunti yako pale unapotaka kujisajili upya ili kutumia programu ya WhatsApp. Hacker hutumia meseji hiyo maalum kuhakiki akaunti ya whatsapp iliyoko kwenye simu yake ili kupata meseji zako pale unapochat kwenye programu yako ya WhatsApp. Ili kuwa salama ni vyema kutumia Antivirus nzuri kwenye smartphone yako, pia hakikisha unazima ujumbe mfupi unakuja kwenye screen yako pale simu yako inapokua iko kwenye lockscreen.

  • Kwa Kutumia MAC address na Njia ya Spoofing MAC address

kwa-kutumia-mac-address-na-njia-ya-spoofing-mac-address

Kila kifaa cha kompyuta kinayo MAC address ya kwake pekee na Whatsapp hutumia hizi MAC address kufanya uhakiki ya kuwa hautumii namba moja kwenye vifaa viwili, hivyo hacker kutumia simu iliyoko rooted pamoja na ujuzi wa kutumia command prompt  za linux kupata MAC address ya kifaa chako na baadae kuhamishia MAC address ya kifaa chako kwenye simu yake ili kusoma meseji zote zinazoingia au kutoka kwenye kifaa chako kitaalamu njia hii huitwa Spoofing MAC address. Jinsi ya kujikinga na njia hii ni ngumu kidogo kwani mtu yoyote mwenye ujuzi wa Linux pamoja na kuwa na simu yoyote iliyoko rooted anaweza kufanya hivyo, kizuri ni kwamba sio rahisi kufanya hatua hizo kwani zinaweza kutumia muda mtu kupata MAC address pamoja na kuiamishia kwenye simu yake.

  • Kwa Kutumia njia ya WhatsApp Web

kwa-kutumia-njia-ya-whatsapp-web

Hapa hacker hutumia njia ambayo iko kwenye programu ya whatsapp kuweka whatsapp yako kwenye kompyuta na baada ya hapo hacker anapata uwezo wa kuona meseji zako zote unazochati kwenye  programu yako. Ili kujikinga na njia hii pendelea kutumia pattern lock na badilisha password za wifi ya simu yako mara kwa mara hata kama hautumii.

Na hizo ndio njia mtu yoyote au hacker anazotumia ku hack programu yako ya whatsapp. Bila shaka sasa utakua makini kabla ya kumpa mtu yoyote simu yako. Basi ili kujifunza haya na mengine mengi endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

6 comments
  1. Tanzania tech nilikuwa naomba msaada kuhusu kufungua Account ya ngu ya face book iliyo fungiwa miezi mitatu Nyuma hivyo nilikuwa naomba msaada

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use