Weka App Play Store kwa Gharama ya TZS 30,000

Pia tutakutengenezea Screenshot kwaajili ya kuweka kwenye listing ya app yako
Weka App Play Store kwa Gharama ya TZS 30,000 Weka App Play Store kwa Gharama ya TZS 30,000

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kufikisha huduma zako kwa watumiaji wa simu za Android basi karibuni sasa uweke mawazo yako kwa watumiaji wa simu za Android kwa gharama ndogo ya TZS 30,000.

Kama unavyojua siku za karibuni watu wengi wamekuwa wakijaribu kupeleka mawazo yako kwa jamii kupitia mtandao, mawazo haya yamekua pia ni huduma ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kusaidia watu mbalimbali kurahisisha kazi au mambo mbalimbali.

Advertisement

Ndio maana leo tumekuja na huduma mpya kabisa ambayo itasaidia watu kama wewe kuweka App kupitia soko la Play Store, huduma hii itakusaidia wewe mbunifu kuweza kufikia watumiaji zaidi ya milioni 10 wanaotumia simu za Android duniani kote.

Kupitia huduma hii utaweza kupata mambo mbalimbali kama kusaidiwa kutengeneza Screenshot za kuweka kwenye listing ya app yako kupitia Play Store. Pia tutakusaidia kuandika maelezo mafupi ya app yako kama app yako iafuata vigezo na masharti yetu. Vigezo hivyo na masharti ni kama vifuatavyo.

Vigezo na Masharti

  • App yako inatakiwa kufuata maadili ya kitanzania yani haitakiwi kuwa na maudhui yoyote ambayo hayaendani na desturi za kitanzania kwa mfano, hatupokei app ambazo zinakiuka vigezo na masharti ya Google ambayo yameandikwa hapa.
  • App yako iwe haina virus au malware za aina yoyote, mara zote huwa tuna scan app yako kabla ya kuweka Play Store hivyo hakikisha app yako haina virus au malware.
  • Hakikisha app yako inafanya kazi vizuri kabla ya kuweka kupitia Play Store, mara nyingi kila unapotuma app yako tunaangalia app yako kabla ya kuweka app hiyo kupia soko la Play Store
  • Hatukubali app ambazo zinazotumia permission ambazo zimekatazwa na Google.
  • App yako inatakiwa kutengenezwa kwa ubora na inatakiwa kufanya kazi vizuri kwa aslimia 100.

Hivyo ndio baadhi tu ya vigezo na masharti, kumbuka masharti haya yanaweza kuongezeka bila ya wewe kupewa taarifa yoyote, App yako haita onekana kwenye akaunti ya Tanzania Tech bali itaonekana kwenye akaunti inayoitwa App Nzuri, unaweza kuona akaunti hiyo kupitia link hapa.

Huduma hii ni kwaajili ya App za kitanzania hivyo hakikisha app yako inakuwa na lugha ya rahusu kutumia app inakuwa na lugha ya kiswahili. Kama app yako ni nzuri basi tunaweza kutangaza hapa Tanzania Tech kwenye kipengele cha app nzuri bila gharama yoyote.

Kama unataka huduma hii unaweza kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wa mawasiliano hapa au unaweza kuandika kupitia forum yetu hapa.

1 comments
  1. Habari..

    Kuna ile taarifa jinsi ya kuwin $5 kila siku… Ukiregister inakuandikia huwezi kufungua account zaidi ya moja..(your cannot open more than one account) na hakuna njia ..mbadala tupostie video ya kusolve hilo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use