Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa programu ya WhatsApp basi habari njema kwako kwani sasa unaweza kujaribu muonekano wa giza (Dark Mode) kwenye programu ya WhatsApp.
Njia hii ni hatua ya awali kabla sehemu hii haijatoka rasmi, kama unataka unaweza kuendelea kusubiri mpaka sehemu hiyo itakapo zinduliwa rasmi au kama wewe huna subira kama mimi basi unaweza kujaribu sehemu hiyo kwa kutumia njia hii nitakayo kuonyesha hapa. Njia hii ni fupi na haito kupotezea muda mrefu hivyo bila kupoteza muda wako basi moja kwa moja twende tukajifunze njia hii rahisi.
Kwa kuanza Bofya HAPA kupakua apk ya WhatsApp Beta, kisha moja kwa moja install kwenye simu yako na fungua na moja kwa moja app hiyo itafunguka na endelea kwenye hatua zinazofuata. Kumbuka app hii haito ondoa kitu chochote kwenye app yako ya WhatsApp bali itaweka app ya WhatsApp beta ambayo huwa ni programu halisi ya WhatsApp ya majaribio.
- Fungua App ya WhatsApp
- Bofya vitufe vitatu vilivyopo juu upande wa kulia
- Kisha chagua Settings.
- Bofya Chats.
- Bofya Theme alafu chagua Dark.
Kwa kufanya hivyo utaweza kupata muonekano wa Giza moja kwa moja kwenye simu yako ya Android. Kumbuka njia hii ni njia ya awali hivyo kama unataka kusubiri sehemu hii itakapo fika kwenye programu ya WhatsApp ya kawaida basi huna haja ya kufanya njia hii.
Kama unataka kujifunza maujanja zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutuma meseji zinazo jifuta kupitia programu ya Facebook Messenger. Pia hakikisha una ungana nasi kupitia YouTube kwani huko tunajifunza mambo mengi sana yanayohusu teknolojia.