Siku hizi mtandao wa Instagram umekuwa ndio mtandao muhimu kwa ajili ya kutafuta masoko mbalimbali hasa kwa wafanya biashara wakubwa na hata wale wadogo. Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa mtandaoni na unayo akaunti ya instagram ya kibiashara basi makala hii ni kwa ajili yako.
Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia ambayo unaweza kuitumia ili kuweza kufanya akaunti yako kuwa maarufu. Kumbuka njia hii ni tofauti kwa kila akaunti hivyo ni vyema kufuata hatua hizi kwenye akaunti yako ili kuweza kufanya akaunti yako kuwa maarufu kwenye mtandao wa Insta.
Mbali na hayo, kupitia makala hii utaweza kujifunza ni siku gani katika wiki ambayo unaweza kuwa maarufu zaidi, hii itakusaidia kuweza kupanga post za kupost siku hiyo na kuweza kuwafikia wateja wako wengi zaidi na kuwa maarufu kupitia mtandao wa Instagram, basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia hii rahisi.
Mahitaji
Kwanza kitu cha muhimu unachohitaji ni akaunti ya Instagram ambayo inatumika au ilikuwa inatumika kwa muda mrefu kidogo, kitu kingine unatakiwa kuhakikisha akaunti yako ni ya kibiashara yaani (Business Account), kama akaunti yako bado ni personal account unaweza kubadilisha na kuwa akaunti ya kibiashara kwa kufuata maelezo kwenye ukurasa huu hapa.
Jinsi ya Kuwa Maarufu Instagram
Instagram inakuja na vitu ambavyo vinaweza kusaidia sana akaunti yako kuwa maarufu, kitu kimoja wapo ni sehemu ya Insights, sehemu hii inakuja na data ambazo zinaweza kusaidia kujua muda wa kupost kwenye akaunti yako ya Instagram na hivyo kufanya watu wengi zaidi kuona post zako.
Sehemu hii inaweza kuonyesha kuanzia muda hadi siku ambayo watu wengi kutoka sehemu uliyopo wanapo kuwa hewani kwenye mtandao wa Instagram. Hii itakusaidia kujua ni muda gani ambao unatakiwa kupost zaidi ili kufanya akaunti yako kuwa maarufu zaidi na post zako kusomwa na watu wengi. Unaweza kupata sehemu hii kwa kufuata hatua hizi zifuatazo
Baada ya kubadilisha akaunti yako ya kawaida kuwa ya kibiashara sasa endelea kwa kufungua akaunti yako ya Instagram kisha bofya mishale mitatu iliyopo juu upande wa kulia, baada ya hapo chagua sehemu iliyo andikwa Insights.
Baada ya kufungua sehemu hiyo sasa utapelekwa kwenye ukurasa wenye data za muhimu ambazo zitaenda kusaidia wewe kujua ni muda gani wa kupost kwenye akaunti yako ya Instagram, pia data hizi zitakusaidia kujua siku nzuri za kupost kwenye akaunti yako ili kufanya akaunti yako kuwa maarufu.
Kwanza tuangalie jinsi ya kujua watu wanao tembelea akaunti yako ya Instagram, hapa unaweza kuangalia kati ya wanaume au wanawake, pia unaweza kuangalia ni mkoa gani ambao watu wana angalia akaunti yako zaidi. Hii itakusaidia kupanga post zako kwa kuangalia jinsia zaidi.
Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye ukurasa wa insight kama nilivyo kuonyesha hapo juu, kisha chagua sehemu ya Audience ndani ya ukurasa wa insights.
Baada ya kubofya hapo sasa uko kwenye ukurasa ambao tutakuwa tunazungumzia kwa siku ya leo hivyo kila kitu ambacho tunahitaji kufanya akaunti yako kuwa maarufu kitakuwa kwenye ukurasa huu. Soma data hizo kwa makini na utaweza kupata mwanga ni nini uweze kufanya.
Basi baada ya hapo sasa ni wakati wa kuangalia ni mkoa gani watu wanao tembelea zaidi akaunti yako ya Instagram.
Kwa kushuka chini kidogo sehemu ya Top locations utaona data zinazo kuonyesha ni mkoa gani ambao watu wengi zaidi huangalia au kutembelea ukurasa wako wa Instagram. Hii itakusaidia wewe kama mfanya biashara kujua ni sehemu gani ambayo ina wateja zaidi wa bidhaa yako.
Kwa kubofya sehemu ya Countries utaweza kuona nchi ambazo watu wengi zaidi hutembelea ukurasa wako. Kumbuka, mkoa au nchi illiyotangulia juu na yenye mstari wa blue mrefu zaidi ndio mkoa au nchi inayoongoza kwa watu kutembelea akaunti yako ya Instagram.
Kwenye umri au Age Range pia ni hivyo hivyo unaweza kuona umri wa watu wanaotembelea zaidi akaunti yako ya Instagram, hii itakusaidia zaidi kujua ni kitu gani cha kupost kwa ajili ya watu hao.
Pia unaweza kuangalia idadi hiyo kwa jinsia kwa kuchagua sehemu ya Men au Women iliyoko pembeni ya sehemu ya Age Range kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu.
Jinsi ya Kujua Muda Gani wa Kupost
Sasa kama unataka kujua ni muda gani wa kupost ili kufanya post zako ziangaliwe na watu wengi zaidi au kama unataka kujua siku gani ni nzuri kwa kupost zaidi basi hii ni hatua muhimu kwako.
Unacho takiwa kufanya kupitia ukurasa wa Insight, shuka chini kabisa kisha utaona sehemu iliyo andikwa Most Active Times.
Kwa kubofya sehemu ya Hours utaweza kuona msaa ambayo ni mazuri zaidi kwa wewe kupost, hii ni muhimu kwani itakuwa inaonyesha data ambazo zinaonyesha muda ambao watu wengi zaidi wanao kufuata wanakuwa online. Hii itakusaidia sana kufanya akaunti yako kuwa maarufu.
Kama ilivyo kwenye hatua ambazo zimepita kwa kuangalia mstari wa blue uliozidi ndio masaa mazuri ya kupost na ndipo muda ambao follower wako wengi zaidi huwa online.
Kama unavyoweza kuona muda ambao watu followers wengi wa tanzania tech huwa hewani ni kati ya saa kumi na mbili ya jioni hadi saa tatu ya usiku ambapo watu wengi ndio huwa hewani zaidi.
Hivyo basi kama unavyoweza kuona hii itakusaidia kuweza kupost muda ambao watu wengi zaidi huwa hewani na kufanya akaunti yako kuwa maarufu, unaweza kuangalia data hizi kila mwezi ili kuweza kujua mabadiliko ya tabia za watu walio kufuata kwenye akaunti yako ya Instagram.
Kwa upande wa siku nayo ni hivyo hivyo, unaweza kuona siku ambayo watu wengi zaidi walio kufuata wako hewani kama inavyoweza kuonekana kwenye picha hapo chini.
Kama unavyoweza kuona hapo juu, siku ambayo wafuasi wengi wa Tanzania Tech wapo hewani, unaweza kuona kwa kuangalia mstari ulio kolea blue ambao unaonyesha siku kwa chini. Kwa upande wetu siku zote huwa na karibu idadi sawa ya watu.
Kwa kutumia njia hizi utaweza kufanya akaunti yako kuwa maarufu sana kwenye mtandao wa Instagram bila kufanya matangazo yoyote. Kumbuka njia hizi ni tofauti kwa kila mtumiaji hivyo ni vyema kuangalia data zako sasa kuweza kujua zaidi.
Pia njia hii ni nzuri zaidi kama ukitumia kuongeza nguvu kwenye kupost siku na masaa usika na sio kuacha kupost kabisa kwenye siku ambazo hakuna watu wengi.
Hadi hapo natumaini njia hii itaendelea kusaidia kukuza biashara yako na kufanya upate wateja zaidi kwa kupost kwa muda sahihi pale watu wanapo kuwa online. Kama kuna mahali ujaelewa au kama unayo maswali au maoni unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.
Nataka habari zenu