Kama wewe ni mmoja wa watu ambao kwa namna moja ama nyingine unatamani kumiliki biashara mtandaoni basi huu ndio wakati wako, kupitia makala hii nitashare na wewe njia rahisi ambayo unaweza kutengeneza tovuti bora ya kuuza na kununua bure kabisa.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu tovuti hii basi unaweza kubofya link hapo chini kuangalia mfano halisi wa tovuti hii ambayo leo nitaenda kuonyesha jinsi ya kutengeneza bure kabisa.
Baada ya kuridhika na mfano hapo juu na kama umeona hiki ni kitu ambacho unataka kuwanacho basi hakikisha unafuata hatua zote zilizopo kwenye makala hii kama navyo elekeza.
Mahitaji ya Muhimu
Hatua ya kwanza unahitaji kuwa na domain pamoja na hosting, hii ni muhimu kwa kuwa tovuti hii itahitaji sehemu ya kuhifadhi picha na mafile ya tovuti hii. Unaweza kupata hosting ya TZS 70,000 ambapo utapata domain yoyote ya .COM bure pamoja na hosting ya GB 100 kwa mwaka mzima.
Naposema mwaka mzima maana yake ni kuwa unapo lipia kuanzia tarehe, 19 mwezi huu 11 mwaka 2020, basi utakuja kulipia tena mwakani tarehe kama ya leo ambapo itakuwa tarehe 19 mwezi wa 11 mwaka 2021. Unaweza kuwasiliana nasi kama unataka huduma hii.
Baada ya kuwa na domain pamoja na hosting, basi upo kwenye hatua za mwisho kabisa za kuanza kumili tovuti yako ya kuuza na kununua bure kabisa.
Hatua za Kufuata
Baada kuwa na domain na hosting basi moja kwa moja unaweza kudownload file za tovuti hii hapo chini kisha upload kwenye server yako na endelea kwa kufuata hatua hizi fupi na rahisi.
Baada ya ku-upload file zote sasa tembelea link ya tovuti yako, kwa mfano kama tovuti yako inaitwa jumaali.com basi andika jumaali.com/install kwenye browser yako. Moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa kama unao onekana hapo chini.
Kama maelekezo yanavyo elekeza kwenye picha hapo juu basi moja kwa moja unachotakiwa kufanya ni kufuata maelekezo hayo, unatakiwa kujaza namba yoyote ya siri kwenye hatua hii kisha bofya endelea.
Baada ya hapo hakikisha kila kitu kipo sawa kwenye server yako na sifa zinazo hitajika zinapatikana kwenye server yako. Kwenye hatua hii hakikisha sehemu zote zina tiki ya kijani. Kama zinayo tiki ya kijani basi bofya endelea.
Hatua hii pia hakikisha kuwa kama file zote zipo kwenye server yako hivyo hakikisha file zote zinapatikana na zimewekewa tiki ya kijani. Kama sehemu hii inatatizo basi hutoweza kuendelea ni lazima kuhakikisha tovuti yako inayo kila file linalo hitajika, baada ya hapo bofya endelea.
Sehemu hii ni muhimu sana kwani hapa unatakiwa kuunganisha tovuti yako pamoja na database, unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza database kwenye server yako. Baada ya kutengeneza database basi jaza data hizo kwenye vyumba hivyo kisha bofya endelea.
Kwenye hatua hii baada ya kubofya Next au endelea, moja kwa moja utaweza kuona database yako ikiwa inatengenezwa, subiri baada ya muda mfupi na utapelekwa kwenye hatua inayofuata.
Kwenye hatua hii ni muhimu sana ambapo hapa ndipo unatakiwa kutengeneza akaunti yako kama admin, akaunti hii ndio inayo kusaidia wewe kuweza kuendesha tovuti hii, bila kuwa na akaunti hii hutoweza kuendesha tovuti hii au hutoweza kuwa mmiliki wa tovuti hii.
Hakikisha unajaza username yako utakayo ikumbuka, pia jaza barua pepe na neno la siri ambalo likuwa ni siri kwako na ambalo utalikumbuka. Baada ya hapo hakikisha kila kitu kipo sawa kisha bofya Malizia.
Baada ya hapo subiria kidogo na utapelekwa kwenye ukurasa mkuu ambapo sasa utaweza kuingia kwenye tovuti yako na tayari kuanza kubadilisha kila kitu kilichopo kwenye tovuti hii.
Bofya sehemu ya login iliyopo juu upande wa kulia kama unatumia kompyuta, kama unatumia simu bofya alama ya menu kisha chagua login kisha moja kwa moja andika email yako na password wewe kama admin uliyo tengeneza kwenye hatua ya mwisho kisha bofya login.
Moja kwa moja bofya alama ya mtu au profile kisha chagua sehemu ya Admin panel, kama unatumia simu alangalia kwenye Menu karibia na alama ya mtu au profile bofya hapo na utaweza kuona Menu hiyo ya admin panel.
Hongera sanaa! kama umefika hatua hii basi moja kwa moja utaweza kuingia kwenye ukurasa wa Admin ambapo hapa ndipo utaweza kubadilisha kila kitu ambacho kitakuwa kwenye tovuti yako mpya ya kuuza na kununua.
Uwezo wa Tovuti Hii
Tovuti hii inao uwezo wa kuuza na kununua kama ilivyo kupatana, lakini pia tovuti hii inayo uwezo wa kuwa kama tovuti ya KIKUU na unaweza kusajili wauzaji na ukawa unachukua kiasi fulani kwa kila bidhaa, lakini sehemu hii inahitaji kuwezesha njia ya malipo ya kupitia website ambayo kwa sasa njia hiyo ipo kwenye mfumo wa Paypal na stripe mifumo ambayo yote haipatikana kwa Tanzania.
Mbali ya hapo unaweza kutumia tovuti hii kuweza kuonyesha bidhaa zako moja kwa moja na mteja anapotaka kununua bidhaa basi hutumia kitufe cha kutoa oda na moja kwa moja unaweza kupokea oda ya mteja kupitia email na atalipa pale atakapo fikishiwa mzigo wake.
Unaweza kutengeneza pesa kupitia tovuti hii kwa njia nyingi.
- Watu wanao uza na kununua wanaweza kupromote matangazo yako ili yaonekane zaidi.
- Pia unaweza kuweka matangazo ya Adsense kwani kuna sehemu za matangazo ndani ya tovuti hii
- Pia unaweza kuchukua kamisheni kwa kila bidhaa itakayo uzwa kwenye tovuti yako.
- Pia utaweza kutengeneza vifurushi maalum ambapo watumiaji watachagua aina ya kifurushi wakati mtu anapo post tangazo lake au bidhaa yake.
- Na njia nyingine nyingi.
Mengine Muhimu
Kama unataka kusaidiwa kufanya kuinstall website hii pamoja na kupata domain pamoja na hosting basi unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja na sisi tutaweza kukusaidia. Pia kumbuaka tovuti hii haija tengenezwa na sisi kwa asilimia 100 hivyo kumbuka vigezo na masharti kuzingatiwa. Pia unaweza kutengeneza website hii kupitia hosting ya bure ambapo unaweza kuipata kupitia hatua zinazo patikana kwenye makala hii hapa.
Kama unalo swali au unayo maoni au kuna mahali umekwama unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini na sisi tutaweza kukujibu moja kwa moja. Kujifunza njia zaidi za kutengeneza pesa mtandaoni endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
Habar,hongera kwa kazi nzuri,Nmeinstall file la kuuza na kununua ila server yangu imeshindwa kufika mwisho,je naweza kujua kama kuna admin default email na password?
Hapana hakuna ni lazima kutengeneza email mwanzoni wakati unafanya Installation.
Naweza je kutengenezewa application ambayo itamtaka mteja anapo jiunga au kuweka tangazo alipie kabla haja login