Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanakuwa wanatumia kompyuta mara kwa mara basi makala hii ni kwa ajili yako, kupitia makala hii nitaenda kuonyesha hatua kwa hatua jinsi unavyoweza kutumia simu yako ya Android kupitia kompyuta yako.
Njia hii ni rahisi sana na ni fupi sana hivyo huna haja ya kupoteza muda mrefu zaidi ya kuangalia video hapo chini na kujifunza hatua zote mwanzo mwisho. Kumbuka ni muhimu kuwa na kivinjari cha Google Chrome kwenye kompyuta yako ili kuweza kukamilisha hatua zote hizi kwa urahisi.
- Download programu ya Android ya Vysor kupitia hapo chini.
- Download Extension ya Vysor Hapa chini
- Download Driver kwa ajili ya kompyuta yako (Windows) kumbuka kama unatumia Samsung chagua ( Samsung official Android USB Driver 15.3 MB) kama unatumia simu nyingine yoyote chagua ( ADB Driver Installer 9.0 MB ).
Kwa kufuata njia zote hizo utakuwa umeweza kuunganisha simu yako na kompyuta kwa urahisi kabisa, kama kuna mahali ambapo utakuwa umekwama tuambie kwenye sehemu ya maoni hapo chini. Kama ungependa kutumia kompyuta yako kwenye simu yako ya Android unaweza kujifunza hatua kwa hatua kupitia makala hii hapa.
Kwa maujanja zaidi hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku, pia hakikisha una subscribe kwenye channel yetu hapa ili kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo.