Kama wewe ni mfuatialiji wa tovuti ya Tanzania Tech basi utakuwa unajua kuwa tulishawahi kuongelea jinsi ya kubadilisha simu yako kuwa Mic.
Kama bado hujasoma makala hiyo unaweza kusoma hapa, lakini kama uliona njia hiyo ni ngumu kwa namna moja ama nyingine basi unaweza kutumia njia hii ambayo itakusaidia kugeuza simu yako kuwa Mic kwa urahisi.
Kitu cha muhimu ni kuwa njia hii inafanya kazi kwa watumiaji wa simu za Android na utaweza kufanya hatua hizi kwa urahisi kama unayo bluetooth speaker au spika ambayo ipo mbali kidogo na wewe. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye hatua hizi.
Kwa kuanza chukua simu yako ya Android kisha unganisha simu yako na bluetooth speaker, unaweza kutumia aina yoyote ya bluetooth speaker, pia unaweza kutumia spika za waya ambazo unaweza kuunganisha kupitia sehemu ya headphone kwenye simu yako.
Baada ya hapo endelea kwa kubofya sehemu ya Settings kwenye simu yako, kisha endelea kwa kutafuta sehemu ya Accessibility.
Baada ya hapo bofya sehemu hiyo endelea kwa kubofya sehemu ya Hearing enhancements, sehemu hii inaweza kuwa tofauti kwenye simu yako hivyo unaweza kutafuta kwa kusearch Settings.
Baada ya hapo, tafuta sehemu nyingine iliyo andikwa Amplify ambient sound na bofya hapo kisha washa sehemu hiyo.
Baada ya hapo anza kuongea kwenye simu yako na moja kwa moja utaweza kuanza kusikia sauti kwenye spika zako za bluetooth. Kumbuka usiwe karibu sana na spika zako kwani utasikia kelele sana au mwangwi.
Njia hii haija tengenezwa kwa kufanya simu kuwa Mic bali ni sehemu kwa ajili ya kufanya usikie vizuri, hivyo tengemea sehemu hii inaweza isifanye kazi vizuri.
Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech, pia tembelea hapa kama unataka kupata habari za simu mpya zinazotoka kila siku.