Ni wazi kuwa dunia kwa sasa inaamia kiganjani, japo kuwa bado kuna uwezekano wa kompyuta kuendelea kuhitajika lakini ni wazi kwa simu kwa sasa zimekuwa zikifanya kila kitu ambacho zamani kilikuwa kunafanywa na kompyuta.
Kuliona hili leo nimekuandalia makala ambayo itakupa maelezo ya tofauti ya jinsi ya kutengeneza video bora kwa kutumia simu yako ya mkononi. Kumbuka hakikisha unapitia makala nzima ili kusudi uweze kujua hatua kwa hatua hadi mwisho jinsi ambavyo unaweza kutengeneza video bora kupitia simu yako na hatimaye kuiweka kwenye mtandao wa YouTube.
TABLE OF CONTENTS
Tengeneza Intro
Mara nyingi video bora ni lazima kuwa na muhtasari baada ya muhtasari ni vyema kuwakumbusha watu kuhusu brand yako. Hapa ndio ambapo inakuwa ni muhimu kuwa na Intro, Intro inaweza kuwa ni maneno mafupi kuhusu brand yako na kama unataka kutengeneza hilo usiwe na wasiwasi.
Kupitia hapo chini utaweza kupakua app ambayo itakusaidia kutengeneza Intro mbalimbali ambazo unaweza kutumia kwenye video zako na hata kwenye channel yako nzima. Jinsi ya kutumia app hiyo ni rahisi na utaweza kupata Intro bora sana kwaajili ya kutumia kwenye video zako kwenye mitandao yote ya kijamii.
Kurekodi Video
Kama unataka kurekodi video zipo njia mbalimbali ambazo unaweza kutumia, kama unataka kutengeneza video za maelekezo ambazo ni kama ambazo Tanzania tech tunafanya basi unaweza kurekodi kioo cha kifaa chako, unaweza kufanya hivyo kwa kutumia app hapo chini.
Lakini pia kama unataka kurekodi video ya kawaida kwa kutumia simu yako basi unaweza kusoma hapa kujua hatua bora ambazo zinaweza kukusaidia kurekodi video kwa kutumia simu kwa urahisi na haraka na kuweza kupata video yenye ubora wa hali ya juu ambayo unaweza kushiriki kwenye mitandao yako ya kijamii.
Kuedit Video
Baada ya kurekodi moja kwa moja ni wakati wa kuediti video yako, mahali hapa ni muhimu kwani kupitia sehemu hii ndipo utaweza kufanya video yako ivutie zaidi na iwe bora kwa muonekano na sauti. Kama unataka kuedit video kisasa unaweza kutumia app bora kupitia hapo chini.
Nyimbo za Bure (No copyright)
Pia wakati wa kuedit ni vizuri kuwa na nyimbo za bure ambazo unaweza kuzitumia bure kabisa bila kulipia, nyimbo hizo zina takiwa kuwa hazina copyright hivyo unaweza kuzitumia kwenye mtandao wa YouTube na mitandao mingine bure kabisa bila kulipia gharama yoyote ile, unaweza kupata nyimbo hizo za bure kupitia tovuti hapo chini.
Pakua Nyimbo za Bure (No copyright)
Video za Bure (No Copyright)
Mbali na hayo kama unatengeneza video ambayo ina onyesha matukio mbalimbali inawezekana ukawa unahitaj clip za video ambazo unaweza kuzitumia bure kwenye video zako. Unaweza kupata clip za bure kabisa ambazo unaweza kutumia bila kupata tatizo la copyright kupitia kwenye tovuti hapo chini.
Pakua Video za Bure (No copyright)
Tengeneza Picha za Video (Thumbnail)
Kwa mujibu wa YouTube, picha za video au Thumbnail ni moja kati ya vitu vinavyo vutia watu zaidi kuweza kuangalia video yako. Kama unataka kutengeneza Thumbnail itakayo vutia watu wengi zaidi basi hakikisha unatumia app hapo chini. App hii itakupa uwezo wa kutengeneza picha bora sana na ambazo zinavuti na utashangaza watu sana.
Upload Video
Baada ya kumaliza kutengeneza intro, kurekodi video, kuedit video na kuweka picha ya video yako, sasa ni wakati wa ku upload video yako kwenye mtandao wa YouTube. Unaweza kufanya hivi kwa umakini kupitia app ya mtandao wa YouTube maarufu kama YouTube Studio. Unaweza kupakua app hiyo kupitia link hapo chini. App hii pia itakupa fursa ya kujibu maoni kwenye video zako na kuangalia idada ya views pamoja na mambo mengine mengi.
Kwa kufuata hatua zote hizo utaweza kutengeneza video zako ikiwa pamoja na kuweka kwenye mtandao wa YouTube kwa urahisi na haraka. Pia unaweza kuangalia kiasi cha mapato yanayo tokana na video zako ikiwa pamoja na kusoma maoni na vitu vingine mbalimbali. Kwa kupitia hatua zote hizo moja kwa moja utaweza kutengeneza video za YouTube kwa urahisi na haraka.
Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua njia bora ya ku skip matangazo ya YouTube bila kubofya sehemu yoyote. Unaweza kusoma hapa kujua zaidi.