Teknolijia ya TV inaonekana kuongoza kwa sasa kwenye mkutano wa CES 2018, hivi karibuni wateja wa Samsung kwa mara nyingine tena wamepata matumaini mapya baada ya kuona tena TV ya The Wall kutoka kampuni ya Samsung sasa ikiwa imeboreshwa zaidi.
Kwa wale ambao hamjui the wall ni TV iliyokuwa kwenye mkutano wa CES 2016 na ni teknolojia ya TV ambayo inaitwa modular yaani unaweza kuunganisha TV mbalimbali za aina moja kuweza kutengeza TV moja. Sasa mwaka huu kampuni hii ya Samsung imeweza kuvunja rekodi kwa kutengeneza TV hii ikiwa na inch 146 pamoja na teknolojia ya MicroLED.
MicroLED hii ni teknolojia ya TV inayokaribiana kidogo na OLED lakini sasa MicroLED yenye pixel zake zinajitengenezea mwanga wake zenyewe hii inamaanisha kuwa unaweza kuzima na kuwesha pixel moja moja hivyo TV hii inauwezo wa kutengeneza picha bora angavu na kubwa zaidi.
Kwa upande wa Samsung wanatumia teknolojia hiyo kuweza kuunganisha TV mbalimbali kutengeneza TV moja. Yani TV hii ya The Wall inaweza kuongezeka ukubwa na kuwa kubwa zaidi kwa kuongeza TV nyingine, kwa sasa haijatajwa kama kuna mwisho wa idadi ya TV unazoweza kuunganisha kwenye TV hii ya The Wall.
Kwa sasa bado haijajulikana ni lini TV hii itakuja kwa wateja, lakini labda pengine hizi ndio teknolojia za TV zinazokuja zikikupa uwezo wa kuongeza au kupunguza ukubwa wa TV yako kwa size yoyote unayotaka. Kwa habari zaidi za TV, hii endelea kutembelea Tanzania Tech pamoja na ukurasa maalum wa CES 2018 kujua yote yatakayojiri mwaka huu 2018.