Kutana na “Project Linda” Badili Simu ya Razer Phone Kuwa Laptop

Utaweza kubadili simu hiyo ya Razer Phone kuwa Laptop
Razer Project Linda Razer Project Linda

Mkutano wa CES 2018 bado unaendelea huko nchini Las Vegas, kampuni ya Razer ambayo ni maarufu kwa utengeneza wa vifaa ambavyo ni maalum kwaajili ya Game nayo pia imeudhuria mkutano huo ambapo kwa mwaka huu imekuja na Project Linda.

Project Linda hii ni aina mpya ya laptop ambayo hutumia simu ya Razer Phone iliyozinduliwa hivi karibuni kubadilisha simu hiyo kuweza kuwa laptop kamili.

Advertisement

Sasa tofauti na laptop nyingine, laptop hii ya Project Linda yenye kioo cha inch 13.3-inch chenye teknolojia ya quad-HD display inatumia simu hiyo ili kuweza kufanya kazi kamili kama laptop.

Tofauti ni kuwa utaweza kuongeza uwezo zaidi kwa kupata uwezo wa kutumia simu yako kama jinsi inavyo kuwa laptop. Kwa kutumia project linda una uwezo wa kuongeza ukubwa zaidi wa simu yako na kuifanya kuwa na terabyte 1 zaidi na kuongeza uwezo wa simu hiyo zaidi.

Kwa sasa bado haijajulikana ni lini laptop hii itawafikia watumiaji, lakini pengine labda kampuni zingine za simu zinaweza kuiga teknolojia hii na labda miaka inayokuja tunaweza tukawa hatuna haja ya kuwa na laptop bali kuwa na smartphone pekee.

Kwa taarifa zaidi za mkutano wa Consumer Electronic Show (2018), unaweza kufuatilia ukurasa wetu maalum wa CES 2018 na utapata taarifa zote kuhusu mkutano huu pamoja na yote yatakayo jiri.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use