Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Njia ya Kusuluhisha Matatizo ya Simu na Kompyuta Mwaka 2017

Njia rahisi ya kusuluhisha matatizo mbalimbali ya kiteknolojia
Tanzania Tech Forum Tanzania Tech Forum

Kama unasoma makala hii bila shaka kwa muda sasa umekua ukitafuta sehemu ya kupata suluhisho la matatizo mbalimbali ya teknolojia iwe simu, kompyuta, mtandao, programu na mengine mengi yahusuyo teknolojia.

Kwa kuanza mwaka huu wa 2017 Tanzania tech kupitia Digital webbase inakuletea namna rahisi kabisa ya kusuluhisha matatizo yako ya kiteknolojia ambayo kwa muda sasa imekua ni tatizo kubwa kutokana na kukosa mahali ambapo patakupa msaada wa kusuluhisha matatizo hayo.

Advertisement

Tanzania tech leo inakuletea Tanzania Tech Forum hii ni sehemu ya tovuti ya tanzania tech ambapo hapa utapata msaada wowote wa kiteknolojia kutoka kwa watu mbalimbali kutoka nje na ndani ya Tanzania. Kizuri zaidi Tanzania Tech Forum inaendeshwa na watu wenye ujuzi mkubwa sana kwenye mambo ya teknolojia. Kuanzia ukarabati au utengenezaji wa vifaa mbalimbali mpaka kwenye utengenezaji wa tovuti au programu mbalimbali.

Vile vile Tanzania Tech Forum inakupa nafasi ya kuweka matangazo mbalimbali ya kiteknolojia, ili mradi iwe ni tangazo kuhusu simu, kompyuta au mambo mengine yahusuyo teknolojia. Mipango yetu ya mwaka 2017 ni kuhakikisha unapata msaada pamoja na taarifa zote za teknolojia kwa urahisi na bila kutumia gharama yoyote, pia tunategemea kupata ushirikiano kutoka kwa wahusika mbalimbali wa mitandao na makapuni ya teknolojia ili kusogeza karibu huduma mbalimbali zinazo tolewa na makampuni hayo.

Kwasasa unaweza kujiunga na Tanzania Tech Forum kwa kuijisajili kisha unaweza ukatengeneza Topic yako hapo hapo, tunategemea kuboresha zaidi mtandao mzima wa Tanzania tech ili kukupa huduma inayotakiwa. Unaweza kujiunga sasa na Tanzania Tech Forum kwa kubofya kwenye Menu hapo juu au kwa kubofya hapa Tanzania Tech Forum.

4 comments
  1. Hakika ndugu zangu mmenigusa sana kuhusu mambo ya teknolojia hapa nchini juhudi zenu na maarifa yenu kwa watanzania juu ya umuhimu wa teknolojia lazima tuelewe.
    Pia naomba mtupe masomo zaidi na zaidi ili tutambue yale ambayo hatukuyatambua kuhusu teknolojia hapa nchini
    MUNGU AWABARIKI WOTE KWA KAZI KUBWA YA KUJITOLEA KWENU KWA WATANZANIA

  2. Naona mambo makubwa sana yamenivutia sana na mko vizuri nimependa kujifunza ni nyie kimtandao ahsante

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use