Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram

Utaweza kurudisha picha ua video ulizofuta ndani ya siku 30 zilizopita
Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram

Mtandao wa Instagram hivi karibuni umefanya maboresho mbalimbali ikiwa pamoja na njia mpya ya kuficha views na likes ambapo watu hawatoweza kuona idadi ya views au like kwenye profile yako ya Instagram, Unaweza kuzuia watu kuona kwenye ukurasa wako mzima au kwenye picha moja moja.

Mbali na hayo, Instagram hivi karibuni pia ili tambulisha sehemu mpya ya kurudisha picha au video ambazo umezifuta kwenye akaunti yako, kupitia sehemu hiyo unaweza kurudisha picha au video za hadi siku 30 nyuma, yaani kama umefuta picha ndani ya siku 30 zilizopita basi utaweza kuirudisha moja kwa moja kwa kupitia njia hii.

Advertisement

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kurudisha picha ambazo ulizifuta kwenye akaunti yako ya Instagram basi unasoma makala sahihi. Bila kuendelea kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye makala hii.

Rudisha Picha ulizofuta Instagram

Kwa kuanza hakikisha una sasisha au una-update app ya Instagram kupitia Play Store au App Store, baada ya ku-update app yako moja kwa moja endelea kwenye hatua zifuatazo.

Fungua profile yako ya Instagram kisha bofya sehemu ya Menu iliyopo upande wa kulia juu, mara nyingi sehemu hii huwa na vimikato vitatu vilivyopo kwa mlalo.

Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram

Baada ya hapo bofya sehemu ya Settings ambayo inapatikana mara baada ya kubofya Menu kwenye hatua iliyopita.

Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram

Baada ya hapo moja kwa moja bofya sehemu ya Account ambayo inapatikana mara baada ya kubofya sehemu ya Settings.

Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram

Baada ya hapo moja kwa moja kwenye ukurasa unaofuta ambao umefunguka baada ya kubofya Account, mwisho kabisa utaona sehemu mpya ya Recently Deleted, bofya hapo kuendelea kwenye hatua inayofuata.

Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram

Kwenye ukurasa unaofuata utaweza kuona picha au video ambazo umezifuata ndani ya muda mfupi wa siku 30 zilizopita.

Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram

Chagua picha au video unayotaka kuirudisha na moja kwa moja baada ya picha hiyo kufunguka endelea kwa kubofya vitufe vitatu vilivyopo juu upande wa kulia na moja kwa moja chagua sehemu ya Restore.

Jinsi ya Kurudisha Picha au Video Ulizofuta Instagram

Kama unataka kuondoa picha hiyo kabisa unaweza kubofya sehemu ya Delete ambapo picha yako au video itafutika kabisa na hutoweza kuipata tena kupitia Instagram.

Na hiyo ndio njia rahisi ya kuweza kurudisha picha au video ambazo umezifuta kwenye profile yako kupitia kwenye mtandao wa Instagram. Kwa sasa inasemekana kuwa sehemu hii inaweza kuja kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp, hivyo endelea kutembelea Tanzania tech kujua zaidi jinsi ya kutumia sehemu hii pale itakapo kuja kwenye programu hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use