Jinsi ya Kupunguza Mwanga wa Kompyuta (Njia Bora Sana)

Utaweza kupunguza mwanga zaidi kwenye kompyuta yako Windows
Jinsi ya Kupunguza Mwanga wa Kompyuta (Njia Bora Sana) Jinsi ya Kupunguza Mwanga wa Kompyuta (Njia Bora Sana)

Kupitia mdau kwenye group letu la Telegram aliuliza njia bora ya kupunguza mwanga kwenye laptop au kompyuta yoyote inayotumia mfumo wa Windows, sasa kupitia makala hii natumaini yeye pamoja na wewe utaweza kufahamu njia hii bora ya kupunguza mwanga kwenye kompyuta.

Ni wazi kuwa laptop au kompyuta nyingi zinakuja na sehemu ya kupunguza mwanga, lakini ni wazi kuwa kuna wakati unahitaji kupunguza mwanga zaidi ya uwezo wa kompyuta yako.

Advertisement

Kuliona hili leo nimeona ni shiriki na wewe njia bora ambayo binafsi natumia kuweza kupunguza mwanga kwenye laptop ambayo mara nyingi nafanyia kazi na imekuwa msaada mkubwa sana kwangu.

Kwa kuanza moja kwa moja pakua programu kupitia link hapo chini, programu hii ni ndogo sana na ina kiasi kisichozidi MB 1.

Download App Hapa

Baada ya kupakua programu hii fungua kwenye kompyuta yako na utaletewa widget kama hiyo hapo chini.

Jinsi ya Kupunguza Mwanga wa Kompyuta (Njia Bora Sana)

Sasa ili kuhakikisha unapunguza mwanga kwa kiasi cha chini hakikisha unafanya settings zifuatazo. Kwenye sehemu ya Manual bofya au weka tiki sehemu ya Disable auto-adjust kama inavyo onekana hapo juu.

Hatua ya pili rudisha kwa kwenda kushoto sehemu ya Brightness na utaona mwanga unapungua kwa kiasi kikubwa. Hii itasaidia kupunguza mwanga kulingana na laptop au kompyuta yako.

Baada ya hapo bofya Hide na programu hii itajificha kwenye sehemu ya tool icon inayokuwa karibu na saa kulia kwenye mfumo wa Windows.

Jinsi ya Kupunguza Mwanga wa Kompyuta (Njia Bora Sana)

Bofya kitufe cha mshale unao angalia juu na moja kwa moja utaona alama ya taa na bofya hapo kufungua Menu kama hiyo hapo juu.

Kwa kufuata hataua hii utaweza kupunguza mwanga kwenye kompyuta yako kwa kiasi kikubwa sana na utaweza kutumia kompyuta yako kwa muda mrefu bila kuumia kichwa au macho yako.

Pamoja na hayo ili kuwa salama zaidi hakikisha unatumia sheria ya 20, 20, 20 unaweza kusoma zaidi hapa kuhusu sheria hii muhimu kwa watumiaji wa kompyuta.

Kama unalo tatizo lolote au mada ya teknolojia unayotaka kujua zaidi unaweza kutuandikia kupitia Tanzania Tech Telegram Group na tutaweza kukujibu swali lako kwa mfumo wa makala hatua kwa hatua kupitia hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use