Wakati programu za Facebook na WhatsApp zikiwa na matarajio ya kuboreshwa zaidi Instagram nayo haipo nyuma kwenye kuleta sehemu mpya. Hivi karibuni kumekua na habari mbalimbali za kuwa instagram inategemea kuleta uwezo wa kupost picha nyingi kwa wakati mmoja.
Katika ripoti zilizotolewa na tovuti za Droid Life pamoja na The next web zinasema kuwa sehemu hiyo mpya ilionekana kwa mara moja na baadae kupotea hii ikiwa inamaanisha yalikua ni majaribio yaliyo husisha watu wachache.
Kwa mujibu wa tovuti hizo sehemu hiyo mpya itakuruhusu kupost picha zaidi ya moja na baadae kuonekana kama post zile za picha zaidi ya moja kwenye mtandao wa Facebook, ili kupost utaweza kuchagua picha zako unazotaka kupost na baada ya hapo picha hizo zitajiweka zenyewe kwenye mtindo wa ‘carousels‘ kisha utaweza kuweka filter tofauti kwenye kila picha kwenye post hiyo.
Bado haijajulikana tarehe rasmi ya kutoka kwa sehemu hiyo ila kwa mujibu wa tovuti mbalimbali za teknolojia sehemu hiyo inategemewa kuja kabla ya mwisho wa mwaka huu 2017.
Kwa habari zaidi kuhusu sehemu hiyo na lini itatoka endelea kutembelea tovuti Tanzania Tech kila siku au unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store ili kupata habari kwa haraka pindi tu zitakapo toka.