Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatarajia kufanya biashara mtandaoni kwa namna moja ama nyingine ni muhimu kujua kuwa yapo mambo ya muhimu sana ya kufahamu kabla ya kuanza kupokea pesa kutoka nje ya nchi.
Kupitia makala hii tutaenda kuangalia mambo kadhaa ambayo ni muhimu sana pale unapo hitaji kupokea pesa kutoka nje ya nchi. Kumbuka makala hii inalenga zaidi wale wanaoishi kwenye nchi za Afrika (Tanzania) na nchi nyingine na wanatarajia kupokea pesa kutoka kwenye kampuni za matangazo kama vile Google Adsense, Propeller Ads na kampuni nyingine za matangazo.
Kama nilivyo kwambia hapo juu, kupitia makala hii tutalenga zaidi kupokea pesa kutoka kwenye makampuni ya matangazo ambayo mara nyingi yamekuwa yakitumia njia ambazo zinafanana hivyo kwa kusoma makala hii natumaini utaweza kupokea pesa zako kwa urahisi na haraka. Lakini kwa kuanza hebu tuangalie kwa ujumla mambo unayo hitaji ili kupokea pesa kutoka nje ya nchi.
TABLE OF CONTENTS
Namba ya Akaunti ya Benki
Ni kweli kwamba unaweza kuona kama benki hazina umuhimu sana hasa kwenye kipindi hichi ambacho unaweza kufanya karibia kila kitu kwa kutumia simu yako ya mkononi, hii inaweza kuwa ni kweli lakini kama wewe ni mmoja wa watu wanao tarajia kupokea pesa mtandaoni au nje ya nchi basi hii ni sehemu ya muhimu sana na ya lazima.
Jina Kamili la Benki Yako
Kitu cha muhimu ambacho utaulizwa pale unapojaza fomu ya kupokea malipo kutoka nje ya nchi ni pamoja na jina kamili la benki yako. Naposema jina kamili la benki sina maana kwa mfano CRDB au NMB hapana, hapa nina maana jina ambalo linatambulisha benki yako kimataifa, kwa mfano kama unatumia benki ya CRDB basi jina kamili litakuwa “CRDB Bank PLC Tanzania” kama ni NMB basi itakuwa ni “NMB Bank PLC”. Kujua majina kamili ya benki yako ni muhimu kuuliza au unaweza kutafuta kupitia Google.
Swift Code au Bic Code
Moja kati ya kitu ambacho kinaweza kufanya ufanikiwe au uweze kuchelewesha kupata pesa zako ni Swift Code au Bic Code. Hizi ni namba za utambulisho ambazo ni muhimu sana kuzifahamu pale unapotaka kupokea pesa kutoka nje ya nchi au kutoka kwenye kampuni kama Google Adsense na nyingine, kila benki inakuja na Swift Code au Bic Code za aina tofauti zipo benki nyingine zinakuja na namba hizo zikiwa tofauti kwa kila tawi la benki na nyingine huwa zinatumia namba moja tu ya utambulisho. Zifuatazo ni Swift Code au Bic Code za benki mbalimbali hapa nchini Tanzania.
Unaweza kusoma list nzima kwa urahisi hapa.
Majina yako kamili
Hitaji la mwisho na la muhimu ni kuwa tayari kujaza majina yako matatu au majina kamili kama invyo onyesha kwenye kitambulishi chako cha taifa. Ni muhimu kujaza majina sahihi kwani kama kuna tatizo lolote la malipo, kampuni husika inaweza kuhitaji copy ya kitambulisho chako ambacho kina majina hayo kamili.
Barua Pepe
Ni wazi kuwa hili ni moja kati ya jambo ambalo watu wengi sana wanasahau kufanya, Ni muhimu sana pale unapo fungua akaunti yako ya benki kuweza kuunganisha akaunti yako pamoja na barua pepe yako hii itasaidia kupata ujumbe pale pesa zako zinapo ingia kwenye akaunti yako kutoka nje ya nchi ikiwa pamoja na kupokea (bank statement) au taarifa za kibenki kuhusu akaunti yako.
App ya Benki Unayo tumia
Moja kati ya vitu ambavyo binafsi yangu hufanya sana ni kutumia app za benki yangu kwa ajili ya kufanya miamala mbalimbali, hii inanisaidia sana kwani pia huwa natumia app hizo kufuatilia kama malipo yame ingia kwenye akaunti yangu pale napo tegemea kupokea pesa kutoka nje ya nchi. Hii inaweza isiwe muhimu kwako kama unaweza kuangalia barua pepe kila wakati.
Kwa kukamilisha hayo yoye sasa utakuwa uko tayari kupokea pesa kutoka kampuni kama Google Adsense na kampuni nyingine ambazo zinatumia njia ya money transfer kuweza kufanya malipo kwa mtu au kampuni yoyote.
Kama bado huja anza kutengeneza pesa mtandaoni basi unaweza kuanzia hapa, kwani unaweza kuipata tovuti ambayo ilinisaidia hapo awali kutengeneza zaidi ya milioni 20 mtandaoni. Kwa maujanja zaidi ya jinsi ya kutengeneza pesa mtandaoni basi hakikisha unatembelea channel yetu ya YouTube hapa, kwani mara kwa mara tunajifunza kwa vitendo njia mbalimbali za kutengeneza pesa mtandaoni.
Yes
Iko poa