Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kupata Simu Iliyopotea kwa Kupiga “Mluzi”

Pia utaweza kupata simu yako ya Android kwa “kupiga makofi”
Jinsi ya Kupata Simu Iliyopotea kwa Kupiga "Mluzi" Jinsi ya Kupata Simu Iliyopotea kwa Kupiga "Mluzi"
©apkpure.com

Kwa kuanza ningependa uelewe kuwa njia hii ni kwa ajili ya mtu ambaye amepoteza simu kwenye mazingira ya nyumbani au mazingira ambayo anayafahamu.

Kwa lugha nyingine njia hii itakusaidia kama umeweka simu yako mahali ambapo umesahau, kama unataka kujua jinsi ya kupata simu ambayo imepotea unaweza kusoma makala hii hapa kama unatumia simu ya Android, na kama unatumia iOS unaweza kusoma hapa.

Advertisement

Jinsi ya Kupata Simu iliyopotea

Baada ya kusema hayo moja kwa moja unacho takiwa kufanya ni kudownload app kupitia link hapo chini. Baada ya kudownload endelea kwenye maelezo hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii, moja kwa moja endelea kwa kuhakikisha una ruhusu app hii kutumia Mic kwenye simu yako.

Jinsi ya Kupata Simu Iliyopotea kwa Kupiga "Mluzi"

Baada ya hapo utaletewa maelezo mengine unaweza kubofya Done kwenye kila maelezo kisha moja kwa moja endelea kwa kufuata hatua hizi.

Kwenye ukurasa wa kwanza utaruhusiwa kutafuta simu yako kwa kupiga Mluzi. Swipe kwenda kulia mwisho wa kioo cha simu yako kuwasha sehemu hiyo.

Jinsi ya Kupata Simu Iliyopotea kwa Kupiga "Mluzi"

Baada ya kuwasha sehemu hii unaweza kubofya sehemu ya Flashlight na Vibrate ili kuongeza uwezekano wa kupata simu yako pale inapo potea kwenye mazingira unayo yafahamu. Baada ya kuwasha sehemu hiyo unaweza kufunga app hii na kisha piga mluzi na utaona simu yako ikitoa sauti kila mara unapo pia mluzi.

Pia unaweza kutumia njia ya kupata simu yako kwa kupiga makofi. Kuwasha sehemu hii bofya sehemu iliyo chorwa makofi, kisha endelea kwa kuwasha sehemu hii kama ilivyo kwenye hatua ya awali hapo juu.

Jinsi ya Kupata Simu Iliyopotea kwa Kupiga "Mluzi"

Baada ya hapo unaweza kuendelea kwa kubadilisha sauti inayo tokea wakati unapiga mluzi au wakati unapia makofi, unaweza kufanya hivyo kwa kubofya sehemu ya Configurations.

Jinsi ya Kupata Simu Iliyopotea kwa Kupiga "Mluzi"

Kwa kufuata hatua hizo moja kwa moja utaweza kupata simu yako ya Android iliyopotea kwa kupiga mluzi. Kumbuka kuwa njia hii ni muhimu kwa mtu ambaye amepoteza simu kwenye mazingira ambayo anayafahamu.

Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu njia mbalimbali za kupata simu yako iliyopotea basi hakikisha unajiunga kwenye channel yetu ya Tanzania Tech hapa. Kwa habari zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use