Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Yaja na Njia Mpya ya Kusaidai Kupata Pesa Mtandaoni

Sasa unaweza kupata njia zaidi za kupata pesa mtandaoni
Youtube pesa mtandaoni Youtube pesa mtandaoni

Kupata pesa mtandao ni moja kati ya mada ambayo hapa Tanzania Tech tumefikiria kuichukua kwa upana zaidi, lakini kwa sababu hii ni mada ya siku nyingine, leo nataka kukuhabarisha kuhusu ujio wa njia mpya kabisa ya kupata pesa mtandaoni iliyoletwa na mtandao wa YouTube.

Hivi karibuni kupitia mkutano wa Vidcon, YouTube imetangaza ujio wa njia mpya ambayo itakusaidia kuweza kupata pesa zaidi kupitia mtandao wa YouTube. Sehemu hiyo itakuwezesha kupata pesa kwa kuweka kiwango cha pesa ambacho mtazamaji ataweza kulipia ili kuweza kuangalia video ambazo utakuwa umeziweka maalum kwa watazamaji wanaolipia.

Advertisement

Hata hivyo YouTube imeweka kiwango cha pekee cha dollar za marekani $4.99 kwa mwezi ambayo ni sawa na Tsh 11,500 kwa mwezi, kiwango ambacho ndio utaweza kulipisha watazamaji watakaopenda kuangalia video zako ulizoweka maalum kwaajili ya watazamaji wanaolipia. Kuwezesha sehemu hiyo kupitia mtandao wa YouTube ni lazima channel yako iwe na Subscribe kuanzia 100,000 au zaidi.

Mbali na hayo YouTube pia imeleta njia mpya ya kuweza kupata pesa kupitia kuuza bidhaa moja kwa moja kupitia video zako za YouTube. Sehemu hiyo itakuruhusu kuweka bidhaa ambazo zitatokea chini ya video na utaweza kupata pesa kutokana na kuuza bidhaa hizo moja kwa moja.

Kwa sasa sehemu hii itakuwa inapatikana kwa watumiaji wa mtandao wa YouTube wenye Subscribe zaidi ya 10,000 na hii ni kwa wale watumiaji wa mtandao huo wa wanaoishi nchini marekani pekee kwa sasa.

Vilevile Youtube imetangaza kuja na sehemu mpya inayoitwa Premieres, sehemu hii ni maalum kwaajili ya video za mubashara Live Streaming. Sehemu hii inakuwezesha kuweka video ya kawaida iliyo rekodiwa kabla ya kuanza kwa video ya mubashara, Hii itafanya ukurasa wa video kutengenezwa na kuruhusu watu kuweza kuchati wakati wakisubiri video ya mubashara kwenda hewani.

Vilevile YouTube wameleta viwango vya pesa kwenye sehemu hiyo pia ambapo utaweza kununua kifurushi ili kusaidia meseji yako kuonekana sana na kuweza kujibiwa kwa haraka zaidi. Sehemu hii kwa sasa inapatikana kwa watu wachache na inasemekana kuja kwa watu wote baadae mwaka huu. Kujua zaidi kuhusu Sehemu hizi mpya unaweza kusoma hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use