Najua kuwa ni watu wengi sana wana ndoto ya kupata pesa hasa kwa kutumia mtandao wa YouTube. Ukweli ni kwamba sio kazi rahisi hata kidogo kwani unatakiwa uwe na vifaa pia unatakiwa uwe ni mtaalamu wa ku-edit video zako, pia unatakiwa kuwa na wasaidizi wa kuweza kuweka video hizo kupitia mtandao wa YouTube na kitu cha msingi zaidi unatakiwa kuwa na muda wa ziada wa ziada kwenye maisha yako.
Sasa yote haya ni marahisi sana kwako kama umejipanga kufanya YouTube kama kazi, kwani ni ukweli usioficha kuwa YouTube inauwezo wa kubadilisha maisha yako ndani ya miaka miwili au mitatu kama ukifanya kazi hii kwa usahihi.
Kwa mfano, ukijaribu kuangalia kwenye mtandao wa Socialblade, kupitia channel kama ya Millard Ayo kwa makadirio channel ya Millard Ayo ina tengeneza kiwango cha makadirio ya hadi Tsh Milioni 11 au zaidi kwa mwezi.
Pesa hiyo inatosha kuendesha maisha yako kila siku na kuweza kununua baadhi ya vifaa unavyoweza kuhitaji kwajili ya kuweza kufanya Youtube kuendelea kuingizia pesa zaidi. Lakini je inakuaje kama unataka kupata pesa na huwezi kutengeneza video..?.
Leo tunaenda kujifunza njia rahisi sana ya kuweza kuanza kupata pesa kwenye mtandao wa YouTube bila kutengeneza video.. infact unaweza kufanya hatua hizi kwa kutumia simu ya mkononi tu.
Sasa najua kuwa YouTube imebadilisha vigezo na masharti ya kuweza kupata matangazo kwenye channel yako, lakini kwa kutumia njia hii ukifuata kwa usahihi hatua hizi basi nakuhakikishia ndani ya mwezi au miezi miwili utaweza kuanza kutengeneza kipato kupitia mtandao wa YouTube. Sasa bila kupoteza muda twende tuka jifunze hatua hii.
- Kwa kuanza unatakiwa kuwa na channel ya YouTube kama bado huna unaweza kutembelea hapa kuweza kutengeneza channel, kumbuka unatakiwa kuwa na Google Account kabla ya kufanya hivyo. Kama tayari unayo YouTube akaunti hakikisha una tengeneza channel yako vizuri kwa kuweka profile picha ya channel pamoja na Cover photo, pia ni muhimu kuweka kwenye sehemu ya about kuhusu channel yako.
- Sasa kama tayari umeshafanya vitu vyote hivi sasa ni wakati wa kuweka video, ingia kwenye mtandao wa YouTube na nenda kwenye sehemu ya kutafuta kisha tafuta video inayolingana na mada uliyodhamiria kwenye channel yako, kwa mfano kama unataka kutengeneza channel ya hadithi unawea kutafuta neno “simulizi za sauti” sasa baada ya kutafuta na baada ya video kutokea nenda kwenye sehemu ya Filter kwenye simu yako sehemu hii inapatikana juu upande wa kulia kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.
- Baada ya kubofya hapo utaona baadhi ya menu zime tokea, angalia mwisho kabisa utaona kuna maneno kama yamezungushiwa duara, chagua sehemu iliyo andikwa Creative Common na malizia kwa ku-bofya Apply.
- Baada ya kubofya hapo sasa utaweza kuona video mbalimbali zimetokea, sasa video hizo zilizotokea hazina Copyright yani unaweza kuzitumia kwenye channel yako bila kupata tatizo lolote kutoka YouTube. Unaweza kudownload video hizo na kuziweka kwenye channel yako bila tatizo lolote na bila youtube kufunga akaunti yako na pia utaweza kuweka matangazo bila tatizo.
Sasa unachotakiwa kufanya ni kutafuta video yenye View nyingi baada ya kufuata hatua hizo hapo juu. Download video hiyo kisha tengeneza kishwa cha habari kizuri tofauti na kichwa cha habari ulicho kikuta kwenye video hiyo kisha upload video hiyo kwenye channel yako.
Kwa sasa hauto kuruhusiwa kuweka picha kwa sababu channel yako ni mpya, endele ku-upload video kwa kutumia njia hii kila siku na utaweza kuruhisiwa kuweka picha kwenye video zako siku sio nyingi.
Hakikisha unafuatilia hatua hizi bila kupotea hata kidogo, kwani endapo uta download video ambayo ina copyright youtube wataweza kufuta akaunti yako au kufungia channel yako isiweze kutumia huduma za YouTube kwa muda.
Njia hii guys nimefundisha watu wengi sana na inafanya kazi kwa asilimia 100. Pia zipo channel nyingi ambazo nazijua zikiwa zinafanya njia hizi hizi na kuweza kujipatia kipato kwa urahisi bila kutengeneza video kwa namna yoyote.
Kumbuka Download video zikiwa kwenye mfumo wa MP4 pia hakikisha una download video zenye muonekano mzuri. Unaweza kutumia programu mbalimbali za kudownload ambazo zinapatikana kwenye mtandao. Unaweza kutafuta Free Youtube Video Download APK na utapata link mbalimbali za programu za kuweza kudownload video.
Kama unatumia kompyuta unaweza kutumia programu ya IDM kuweza kudownload video za YouTube, pia sehemu ya Filter kwa upande wa kumpyuta inapatikana juu upande wa kushoto baada ya kutafuta video. Thats it guys unaweza kutumia njia hii kila siku jitahidi kuweka angalau video moja kila siku na utakuja kuniambia matokeo yake.
Nnavyofahamu mimi ili YouTube waanze kukulipa pesa Ni lazima uwe umefikia idadi ladhaa ya subscribers yaana Kama elfu 1 hv. Je kwa njia hiyo kuna uwezekano gani Wa kukulipa na haujaikia idadi hiyo ya subscribers?
Ndio njia hii itakusaidia kupata subscriber kwa haraka sana.
mbn filter haionekan kweny YouTube
Ukidownload inakaa offline sasa unawezaje ku upload
Baada ya youtube kuanza kukulipa je utatumia njia gani kuzipata hizo pesa?
Mimi nina channel yangu lakini haina subscaber ata ishiri je nikifuta iyo njia itanisaidi
Naomba kujua kwanini haitapewa copy right claim? Wakati sio yako?
Hujashoot wewe then usiambiwe umeiba kazi ya watu usipate copryt strike kivipi hapo fafanua please by 0716762765
hallo
mbona icon ya filter haionekani utube app
Asante kwa somo zuri naomba kujua jinsi ya kuweka matangazo na jinsi malipo yanavyo fanyika.
napenda kuuliza malipo yanafanyikaje? 0746485419
Malipo ni kupitia bank yako au kupitia Western Union.
Je baada ya kukamilisha vigezo vyote vya kuripwa ,je nitaripwa shingap kwa viewers 1000?
Mimi nimsanii wa bongo flevar lakini sijui mbinu nyingi zakuweza kufanya ilinipate pesa naomba msaada
Maoni*mi na subscriber elfu 2k lakini si lipwi ni fanyaje
Unatakiwa kufikisha views au watch time inayotakiwa