Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu Yako Ina GB 64.? Ongeza Storage Kwa Kutumia Njia Hii

Ongeza Storage kwenye simu yako hadi asilimia 30 kwa kufuata njia hizi rahisi
Simu Yako Ina GB 64.? Ongeza Storage Kwa Kutumia Njia Hii Simu Yako Ina GB 64.? Ongeza Storage Kwa Kutumia Njia Hii

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanamiliki simu yeye nafasi au Storage zaidi ya GB 64 basi makala hii haikuhusu sana kwani ni wazi kuwa mpaka sasa bado simu yako inayo nafasi au ROM ya kutosha.

Lakini kama unayo simu ya Android yenye nafasi au storage chini ya GB 32 basi makala hii inakuhusu kwani najua utakuwa umewahi kukutana na tatizo la simu yako kuishiwa na nafasi. Hii inatokea sana hasa kwenye simu zenye ROM GB 16.

Advertisement

Kuliona hili leo nimekuandalia makala ambayo itakusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kuongeza nafasi au storage kwenye simu yako ya Android. Kupitia makala hii utaweza kuongeza nafasi kwenye simu yako kwa asilimia 30 au zaidi kama ukifuata maelezo yangu hadi mwisho.

Pakua App ya G File

Kama unatumia simu yoyote yenye ROM chini ya GB 16 basi hatua ya kwanza ni kuhakikisha una pakua app ya G File, app hii ni muhimu sana na itakusaidia sana kuweza kuondoa mafile ambayo hayatakiwi kwenye simu yako.

Download App Hapa

App hii mbali ya kuondoa file hizo pia itakwambia pale simu yako inapokaribia kufikia kiwango cha mwisho cha nafasi au storage. App hii ni bure na ni muhimu sana kama unataka kuongeza nafasi kwenye simu yako ya Android.

Hamisha App Kutoka Kwenye Simu Kwenda Kwenye SDCard

Kama simu yako inayo sehemu ya kuweka memory card basi unaweza kuongeza nafasi ya simu yako kwa kuhamisha apps zilizopo kwenye ROM na kuziamishia kwenye memory card ya simu yako. Japokuwa sio apps zote zenye uwezo wa kuhamishiwa kwenye memory card lakini apps nyingi zinakuja na uwezo huo.

Kurahisisha hili unaweza kutumia app ya APPtoSD, app hii inaweza kusaidia sana kuweza kufanya hatua za kuamisha apps kwa haraka na urahisi.

Download App Hapa

Fahamu Kuhusu Google Photos

Simu zote za Android zinakuja na app ya Google Photos, app hii inaweza kuhifadhi picha zako zote zilizopo kwenye simu na wakati mwingine app hii huifadhi picha zote bila hata wewe kujua.

Kama unayo simu ya Android moja kwa moja tafuta app ya Google Photos na fungua app hiyo unaweza kukuta picha zako zote zikiwa zimepangwa kwa tarehe ndani ya app hiyo. Kama picha zako zote zipo na umeakikisha hilo basi unaweza kufuta picha zote ambazo ziko kwenye simu yako kwani tayari unazo picha hizo kwenye akaunti yako ya Google Photos.

Simu Yako Ina GB 64.? Ongeza Storage Kwa Kutumia Njia Hii

Kama kwa namna yoyote umekuta hakuna picha zako kwenye app hiyo (hii inatokea mara chache sana) hivyo basi unaweza kuwasha app hiyo kuruhusu iweze kuhifadhi picha kwenye app hiyo. Unaweza kufungia app hiyo kisha bofya Menu – Alafu bofya – Settings – kwenye Backup & Sync bofya na washa kwa kuchagua sehemu ya On.

Jaribu App ya File Cleaner

Kama simu yako haina nafasi, lakini inayo nafasi ya ku-install app yenye angalau MB 2.8 basi unaweza kujaribu app hii ya Big File Cleaner, app hii itakusaidia sana kuweza kuondoa mafile yoyote yenye ukubwa mkubwa kupitiliza.

Download App Hapa

Kama ushawahi kupakua movie kwenye simu yako na kusahau kufuta au kuna app au kitu chochote kinacho hifadhi data kubwa kwenye simu yako basi app hii itakusaidia kugundua kuhusu app hizo au file hizo. Pia uzuri wa app hii haiondoi file lolote mara moja na badala yake huonyesha kwanza file hizo au apps hizo na baadae kukupa uwezo wa kufuta apps au file hizo ambazo ni kubwa.

Futa Cache Kwenye Simu Yako

Najua ukisikia cache unahisi nitakwambia kuhusu kupakua app mpya ya kufuta cache, lakini kutokana na ripoti mpya hakikisha hupakui app yoyote ya kufuta cache kwani app hizi mara nyingi zinasemekana kuwa hazifanyi kitu chochote.

Simu Yako Ina GB 64.? Ongeza Storage Kwa Kutumia Njia Hii

Badala yake tumia app za kufuta cache ambazo zinakuja kwenye simu moja kwa moja, Samsung inakuja na app yake ya kufuta cache, TECNO pia inakuja na app ya kufuta cache pamoja na Infinix pia inakuja na app ya kufuta cache. Hakikisha unatafuta sehemu ya kufuta cache kupitia settings kisha tumia sehemu hiyo moja kwa moja kuongeza nafasi kwenye simu yako.

Kwa kufuata hatua hizo naamini utakuwa umeongeza nafasi kwenye simu yako kwa hadi asilimia 30 au zaidi. Kama kwa namna yoyote utakuwa umekwama unaweza kuuliza swali kupitia sehemu ya moani hapo chini. Kama unataka kujifunza kwa vitendo hakikisha una subscriber kwenye channel yetu ya YouTube Hapa.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use