Katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia, usalama wa mtandao na kasi ni mambo muhimu sana kwa watumiaji wa kompyuta na vifaa vingine vya kidijitali. Mojawapo ya njia bora za kuhakikisha unapata mtandao wa haraka na salama ni kutumia huduma bora za DNS au (Domain Name System).
Kupitia makala hii nitaelezea jinsi ya kuongeza kasi na usalama wa mtandao wako kwa kutumia huduma za bure za DNS kama Quad9, Cloudflare, na nyinginezo.
TABLE OF CONTENTS
DNS ni Nini na Kwa Nini ni Muhimu
DNS ni kama “kitabu cha simu” cha mtandao, kazi kubwa ya DNS ni kupokea ombi lako unapojaribu kufikia tovuti na kuelekeza kwenye anwani sahihi ya IP ya tovuti hiyo. Yani unapo andika tanzaniatech.one kwenye Browser yako DNS kutafsiri jina hili kuwa IP na hivyo kupeleka ombi lako kwenye tovuti unayohitaji. Hatua hizi ndizo kufanywa na DNS.
Kwa sasa zipo aina mbalimbali za DNS, kuna DNS ambazo huongeza kasi zaidi bila kukupa ulinzi, na nyingine uongeza kasi na kukupa ulinzi huku nyingine zikikupa ulinzi pekee. Pia zipo kwenye makundi mawili yani huduma za Bure na Kulipia.
Huduma Maarufu za Bure za DNS
Zifuatazo ni huduma bora za bure za DNS unazoweza kutumia kuboresha kasi na ulinzi wa kompyuta yako:
Quad9
- Inazuia tovuti hatarishi kwa kutumia taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya ujasusi wa mtandao.
- Hailogi au haiweki taarifa za watumiaji, hivyo inalinda faragha yako.
- Rahisi kutumia kwa watu wa kawaida na biashara ndogo.
Cloudflare DNS
- Inajulikana kwa kasi ya juu zaidi.
- Inatoa chaguo la ziada kama `1.1.1.2` (huzuia programu hatari) na `1.1.1.3` (huzuia programu hatari na maudhui ya watu wazima).
- Hailogi au kuweka data za watumiaji.
Google Public DNS
- Inaaminika kwa kasi na utendaji bora.
- Haizuii tovuti hatarishi moja kwa moja lakini inatoa huduma ya kuaminika.
AdGuard DNS
- Huzuia matangazo na kufuatilia mtandaoni.
- Inatoa ulinzi dhidi ya programu hatarishi na maudhui yasiyofaa.
OpenDNS
- Ina chaguo la kuchuja maudhui kwa familia.
- Inazuia tovuti za wizi wa taarifa (phishing) na programu hatari.
Jinsi ya Kubadilisha DNS Kwenye Kompyuta Yako
Kama unataka kuongeza Speed au ulinzi kwenye kompyuta yako unaweza kufuata hatua hizi ili kubadilisha DNS kwenye kompyuta yako:
Kwa Windows:
Unganisha Internet kwenye kompyuta yako kisha moja kwa moja kwenye bofya sehemu ya Contro Center, sehemu hii ni katikati ya Icon za Network na Speaker. Baada ya hapo bofya kwenye Jina la Wi-Fi unayo tumia kwenye kompyuta yako, hakikisha ni kwenye sehemu ya mshale unao elekea kulia.
Hatua ya pili baada ya kufungua jina la Network uliyo jiunga nayo moja kwa moja bofya alama ya i au info ili kufungua Properties.
Baada ya kufungua sehemu hii moja kwa moja tafuta sehemu iliyo andikwa DNS Server assignment kisha bofya kitufe cha Edit kilichopo mbele yake. Kwenye mfano huu mimi nimesha weka DNS za Quad9 lakini wewe utaona sehemu hii ipo kwenye Automatic.
Kwenye hatua zinazo fuata bofya sehemu ya kwanza kuwa Manual kutoka Automatic, kisha moja kwa moja chagua IP kulingana na hufuma unayotaka kwa mfano mimi natumia Quad9 hivyo IP yangu ni 9.9.9.9 unaweza kuona IP zote hapo chini za DNS zote ambazo tumetaja hapo juu na nyingine za ziada.
DNS Service | IPv4 Address | IPv6 Address |
---|---|---|
Quad9 | 9.9.9.9 |
2620:fe::fe |
Cloudflare DNS | 1.1.1.1 , 1.0.0.1 |
2606:4700:4700::1111 , 2606:4700:4700::1001 |
Google Public DNS | 8.8.8.8 , 8.8.4.4 |
2001:4860:4860::8888 , 2001:4860:4860::8844 |
AdGuard DNS | 94.140.14.14 , 94.140.15.15 |
2a10:50c0::1:ff , 2a10:50c0::2:ff |
OpenDNS | 208.67.222.222 , 208.67.220.220 |
2620:119:35::35 , 2620:119:53::53 |
CleanBrowsing | 185.228.168.168 , 185.228.169.168 |
2a0d:2a00:1:: , 2a0d:2a00:2:: |
Comodo Secure DNS | 8.26.56.26 , 8.20.247.20 |
(No IPv6 support) |
Yandex.DNS | 77.88.8.8 , 77.88.8.1 |
2a02:6b8::feed:0ff , 2a02:6b8::feed:1ff |
DNS.Watch | 84.200.69.80 , 84.200.70.40 |
2001:1608:10:25::1c04:b12f , 2001:1608:10:25::9249:d69b |
Kwenye sehemu ya Preferred DNS weka IP Address unayotaka, hii ni IPV4 Address unaweza kuchagua kulingana na huduma unayotaka kwa mfano kama unachagua Quad9 utaweka 9.9.9.9.
Kisha sehemu ya DNS over HTTPS chagua On (automatic template). Kisha kwenye sehemu ya chini kabisa ambayo imeandikwa IPV6 chagua IP ambayo ipo kwenye jedwali hapo juu, kulingana na huduma unayotaka. Kwa Quad9 utachagua 2620:fe::fe au 2620:fe::9.
Kisha kama kwenye IPV4 sehemu ya DNS over HTTPS chagua On (automatic template) kisha malizia kwa kubofya sehemu ya Save mwisho kabisa wa box hilo.
Kwa kufanya hivyo utakuwa umeweza kuwasha sehemu hii muhimu ambayo itaweza kukupa ulinzi na kasi ya Internet kwenye kompyuta yako. Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta ya Mac unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kubadilisha DNS kulingana na mfumo unaotumia.
Faida za Kutumia DNS Bora
- Ulinzi Dhidi ya Tovuti Hatarishi: Huduma kama Quad9 na AdGuard huzuia tovuti hatari kabla ya kuzifikia.
- Kasi ya Mtandao: Huduma hizi huongeza kasi ya kutafuta na kufungua tovuti.
- Faragha Bora: DNS kama Cloudflare na Quad9 haziingilii faragha yako kwa kuhifadhi data za mtumiaji.
- Ufikiaji wa Maudhui Salama: OpenDNS na CleanBrowsing hutoa chaguo za kuchuja maudhui yasiyofaa kwa familia.
Kubadilisha DNS ni hatua rahisi lakini yenye faida kubwa kwani inasaidia kuongeza kasi na usalama pale unapotumia mtandao au kompyuta yako. Kitu cha muhimu ni kuhakikisha unachagua huduma ya DNS inayokidhi mahitaji yako.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kubadilisha DNS kwenye simu yako ili kuongeza kasi ya Internet pamoja na ulinzi pale unapo tumia mtandao.
je hiyo programu ya dns ipo ya simu za android